Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 3,716
- 11,704
Serikali tuliyonayo kwa sasa ndio serikali ya kibinafsi zaidi na iliyojaa umimi kuliko nyingine zote zilizopata kutokea.
Ukifungilia vyombo vya habari muda wote utasikia "rais katoa pikipiki.......", "rais kajenga hospitali........", "rais anajenga SGR.........", "tunakushukuru rais kwa hiki au kile..…..", yaani kila kitu ni kumtukuza na kumsifu rais tu.
Haya hayatokei kwa bahati mbaya, binadamu wanajua ku 'survive', kwasasa wamemsoma rais na wanajua kuwa anapenda kutukuzwa na kusifiwa hivyo basi wanampta anachokitaka.
Madhara yake kwa taifa ni kuwa wananchi hawana 'sense of ownership' na kinachoendelea nchini mwao, hawaoni kuwa wao ni sehemu ya maendeleo ya nchi, wao hawana mchango wowote kwenye maendeleo ya nchi, ni kama vile rais anatoa hela zake binafsi mfukoni kufanya yale anayodaiwa kuyafanya.
Hali hii haina afya kwa umoja na mshikamano wa Taifa hili, serikali imeajiriwa na wananchi na ni muhimu kwa viongozi kulikumbuka hilo, wakati wa vita ya Kagera nchi nzima tulisimama pamoja, watu walijitolea kutoka vijijini huko wajiunge na jeshi ili wakaipoganie nchi yao, wengine walijitolea vyakula na hata magari yao, wale waliokataliwa kujiunga na jeshi labda kwa sababu za kiafya walilia machozi kwa kuikosa nafasi ya kwenda kuipigania nchi yao, haya yalitokea kwasababu mwalimu alikua na uwezo wa kuwafanya wananchi waione nchi kuwa ni yao, magumu ni yetu sote na mafanikio ni yetu sote.
Mnaolipwa mishahara ili kumshauri JPM fanyeni kazi yenu vizuri, adui wa nje mwenye nia mbaya anapata wasaa mzuri zaidi wa kuishambilia nchi pale ambapo hakuna umoja.
Tujiulize, leo hii JPM akifa (God forbid), au akikamatwa na ICC kimabavu, je kuna wananchi watafurahia mioyoni mwao au hata kufurahia waziwazi? Kama ukiona jibu ni ndio basi ujue tuko pabaya, matukio ya namna hiyo yanaposhindwa kuiunganisha nchi basi ni wazi kuwa nchi hiyo ina tatizo kubwa.