VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kama kuna sehemu CCM haipo tayari kuachia kidemokrasia,basi ni Urais wa Zanzibar na Umeya wa Dar. Zitapigwa pasi,chenga na danadana hadi UKAWA wasuse. Na wakisusa,sisi tutakula!
Nilikuwa Zanzibar,nimejionea ukweli. Kwamba, CCM ilikataliwa kuliko CUF. Sisemi hapa kuwa CUF walishinda. Hayo ni mambo ya Jecha na ZEC yake. Lakini,hadi leo,kuna danadana za maana kule. Hadi CUF wamesusa. Ingawa hawataondolewa majina yao,sisi kama CCM tutashinda kiulaini uchaguzi wa marudio.
Hapa Dar,idadi ya Madiwani wa UKAWA ni kubwa kuliko ile ya CCM. Kimahesabu,UKAWA watatoa Meya wa jiji. Lakini,kimaziombwe ya demokrasia,CCM yaweza kuibuka na ushindi. Acha sarakasi ziendelee. Hadi UKAWA wasuse. Korogakoroga yaendelea kunoga. Ipo siku,italipa.
UKAWA mkisusa,CCM yala!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam