Umewahi Kwenda hijja? Swali lililomchanganya Lipumba

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Salamu wanajamvi!
Kwahakika swali hili lilimfanya Professor Lipumba awe anatafakari kwa kina majibu anayotoa kwa maswali mbalimbali aliyoulizwa Umewahi kwenda Hijja? Swali hili siyo tu lilimchanganya lakini pia lilimfanya mnyonge na kuanza kuwa mpole.

Natamani Swali hili angeulizwa pia ndugu Hamphrey Polepole kuwa AMEWAHI KWENDA HIJJA? Najua Polepole siyo muumini wa dini ya kiislam, lakini pia linaweza kuwa na nguvu ileile iliyo mwingia Prfessor Lipumba. Polepole anatulaghai. Ulaghai ulianzia siku ile alipo sema Kinana hakuandaa press conference Lumumba! Ukweli ni kwamba Kinana aliandaa press conference ili kutolea ufafanuzi mambo kadhaa ya kisiasa na ndio maana waandishi walienda .Kama angekuwa siyo mlaghai angeujulisha umma kuwa bosi wake ametumwa kwenda kutibiwa India!

Je, inawezekana Kinana anaumwa? Haiwezekani Kinana aumwe akae nyumbani halafu kusiwepo na mtu hata mmoja miongoni mwao aliyetamani kwenda kumpa pole. Hata majambazi wenye moioyo migumu huhitaji kufarijiwa nyakati za dhiki na mateso kama kuumwa sembuse Kinana? Polepole umewahi kwenda kuhijji?

Rai yangu kwa waandishi habari za uchunguzi ni kwamba, jamii inahitaji ukweli, na jambo hili la Kinana siyo gumu kufahamu ukweli wote.kuna watu tunahitaji kwenda kumpa pole ndugu yetu.Binafsi namtakia apone haraka, arudi kazini.
 
Sasa Polepole na kuhijj wapi na wapi ? Lipumba limemgusa kwa sababu ya imani yake ,...sasa Polepole hata kuihijj kwenyewe pengine hajui ni nini sasa unategemea aguswe ?
 
Pumba, post angeulizwa, ulishawahi kuoa japo kwa wiki moja tangu umebalehe?
 
Sijapata kujua kua Prof Lipumba akiamka au anapovua nguo za kazi ili alale anafikiria nini kichwani mwake.

Najitahidi sana kupima anayoyaongea mdomoni na anayofikiri kichwani mwake nabaki kusikitikia vizazi vijavyo vitakavyo pata shida kutuelewa baada ya miaka 100.
 
Ninachoona ni watu wa nyumba moja wameamua kufanya maigizo, waendelee tu na maigizo yao kwa sababu kuna mwezi utafika Nape, Kinana, Makonda, Magufuli, Mkapa, Kikwete, Mwinyi wote watakua upande mmoja na hawatosimama popote kwa chochote mpaka wapate ushindi.
Fumbo kubwa sana hili!!
 
Tukimuuliza Mbowe uliwahi kwenda Hijja? Then tukamuuliza kwanini Kampeni za Urais 2015 zilitumika Pesa za Lowassa na Rafikize lakin Vitabu vya Fedha za Chadema vinaonesha ni Fedha za Chama ndizo ziligharamia Uchaguzi atakosa raha kabisa kwny Jibu lake!
 
Kwenda hijja au kutokwenda kuna tofauti gani, mbona waovu wakirejea huwa ndo waovu zaidi.Lipumba amejibu alienda mara mbili sasa tazama matendo yake kabla na baada ya kwenda hijja huko Mecca na Madina.
 
Tukimuuliza Mbowe uliwahi kwenda Hijja? Then tukamuuliza kwanini Kampeni za Urais 2015 zilitumika Pesa za Lowassa na Rafikize lakin Vitabu vya Fedha za Chadema vinaonesha ni Fedha za Chama ndizo ziligharamia Uchaguzi atakosa raha kabisa kwny Jibu lake!
Kweli wewe popoma!
 
"often the greater our ignorance about something, the greater our resistance to change" By Marc Bekoff

Kinana anapitia mazingira magumu kwa sasa. Angekuwa chama cha upinzani ccm wangempa ulinzi na airtime ya kutosha ili aongee ya moyoni kama walivyowahi kufanya kwa Dr Slaa na Pro - Pesa (prof). Kwa kuwa serikalini ni yao, hadithi za mara india, mara Likizo zinasikika. Kwa taarifa yenu wajanja tumeshaujua ukweli. Jopo la kumbembeleza liko mezani, nyie kama hambabaishi na yeyote mwacheni awachane muone kama mtabaki njia kuu.
 
Ninachoona ni watu wa nyumba moja wameamua kufanya maigizo, waendelee tu na maigizo yao kwa sababu kuna mwezi utafika Nape, Kinana, Makonda, Magufuli, Mkapa, Kikwete, Mwinyi wote watakua upande mmoja na hawatosimama popote kwa chochote mpaka wapate ushindi.
Tena kwa faida yao na familia zao na wala si kwa faida ya nchi.
 
Kwa usaliti anaofanya ilo swali limfanya profesa afikiri hakwenda hija ila alienda haja
 
Back
Top Bottom