screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,792
- 15,693
Hii tabia sijui tuseme ni ya waafrika au nini, tuna roho ya kwanini pale mtu fulani kwenye jamii anapoonekana wa tofauti, yaani kapiga hatua fulani kuliko wengine, tunatamani wote tuwe sawa, anapotokea fulani anakuzidi ndipo chuki zinaanza.
Mi nakumbukuka mamaangu (mfanyabiashara) waliwahi mzushia kashfa ya uchawi/ushirikina mtaani kisa ana duka ambalo linauza sana, majirani walisambaza uzushi eti analeta waganga kila siku na watu waliamini.
hawakutaka kufikiria kwamba pengine anauza sana kuliko wengine kutokana location aliyopo (njia panda) na ana vitu vingi vinavyoshawishi wateja, wao akili yao iliwapeleka kwenye uchawi tu, lakini nashukuru Mungu huo uzushi haumkumrudisha nyuma aliendelea kuchapa kazi na wakaacha wenyewe kusema.
Je, umewahi kukumbana na uzushi (kashfa) za namna hii kwenye jamii/ masomo/ biashara/ makazini kutokana na kupiga hatua fulani?
Na je uliweza vipi kukabiliana nao?
Sent using Jamii Forums mobile app