Umewahi kumpa makavu / kumchenchia bosi wako pale alipovuka mipaka

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,407
19,061
Wahanga wengi wa manynyaso ya mabosi ni kwenye kampuni binafsi, biashara za watu binafsi, kuajiriwa kwa baadhi ya wahindi na wachina, n.k

Mkasa wangu

Kuna kipindi fulani nikiwa mtaani baada ya kumaliza chuo nilipewa connection sehemu ya kujishikiza kampuni binafsi mshahara laki 2, yani kulikuwa na huyo msimamizi wetu wa kazi (supervisor) ambae ni kero tupu, hakuweza kuona lolote zuri nalofanya hata nipige kazi kwa bidii namna gani.

Alikuwa ana lugha kali sana lakini bado hakuwahi kuitumia kwangu maana nilifanya kazi kwa uadilifu, sasa kuna siku moja muda wa lunch nilichelewa kufika kazini kama kwa dakika 10 hivi, nilimkuta msimamizi akiwa ananisubiria mlangoni na amenipania si mchezo.

Akaanza kunigombeza na kunitolea lugha chafu, alintukana tusi moja zito kidogo lililonifanya nimrudishie fadhila, nilimpiga bonge la kibao,, paaaaa!!! kimyaaaa, vimaneno maneno vyote vimemwishia!! muda huu wote niliwasha voice recorder ya kwenye simu yangu.

Tuliitwa ofisini kwa bosi, yeye ndie aliyeanza kuongea basi akaanza kutia chumvi kwamba wala hakunitukana ila nimempiga, mimi muda wa kujitetea niliweka simu mezani nika play kilichorekodiwa ile lugha yake ya kunigombeza, tusi na kibao matata nilichomnasa.

Bosi alinionya kitu hicho nisurudie na kwamba siku nyingine nilalamike kwake.

Yule msimamizi kwa ile lugha yake kali + tusi alisimamishwa kazi mwezi mzima, mimi nilifanya kazi mpaka nilipopokea mshahara wa mwezi huo nikandoka ili kuepusha makubwa ambayo yangetokea endapo angerudi, nilikuja kuambiwa kwamba alishushwa cheo.

Kuna siku nikiwa kwenye gari yangu nilimuona, nilimpigia honi nikampungia mkono huku nikitabasamu
 
Wewe upo kada ya ualimu?
 
Nakumbuka kipind napga kaz BRAC ofisini wafanyakaz wengi walikua wanawake siku hiyo nmetoka nje kuongea na mlinzi narudi ofisini nakuta wananiongea nilileta noma sana tembeza vibao wale wakubwa zangu maza zangu nikawakanya sana ilikua noma hadi kwa boss.
 
Chai online siku ipite
 
Sijawahi kugombana na bosi lakini nimewahi kufanya kazi na mabosi wanyampara, wengi tu. Nilipogundua hivyo nilitafuta kazi nyingine kimya kimya na kuaaga na kuondoka.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…