Umewahi kufanya ukauzu gani kwa mpenzi wako?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umewahi kufanya ukauzu gani kwa mpenzi wako?!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NasDaz, Apr 1, 2012.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  SIMULIZI hii ni ya ukweli, ukizani uongo basi shauri yako; hususani wewe mwanaume mwenzangu upendae kujikweza mbele ya vidosho!!

  In short ni kwamba, siku hizi nimechoka mbaya lakini enzi zile ilikuwa ni TOO MUCH!! Basi kipindi kile cha msoto wa kutisha, nikabahatika kukutana na msichana mmoja..…mzuri wa haja; mama Mnyamwezi, baba Masalia ya Waarabu! Hebu pata picha, huyo kinda linalotoka hapo litakuwaje!! Hata hivyo, yule shori hakuwa mwenyeji sana hapa Dar…ni product ya Nzega, Tabora!

  Basi bwana, tukaachiana contacts! Ikawa mara kwa mara tunawasiliana hadi penzi likachanua na kukomaa!!
  Siku moja, nikiwa sina hili wala lile; binti wa watu akaenda hewani! Bila kutarajia, akaniambia anataka kuja ghetto! Kucheki saa, nikakuta inakaribia saa 11.30 jioni! NIKASHANGAA! Nikashangaa kwavile aliniambia anaishi Pugu wakati mimi naishi Temeke! Nikajiuliza, mida yenyewe ni jioni kabisa inayokaribia machweo…na Pugu na Temeke ni mbali ile mbaya! Nikajiuliza kwao atarudi saa ngapi! Nilipomuuliza atarudi saa ngapi wakati mida imeenda sana, akajibu anakuja kulala kwangu!

  Liudenda likanimwagika, na kijasho chembamba nacho kikanitiririka kidume cha watu! Nilipoingia mfukoni, nikajikuta nina buku unusu (TZS 1,500/=) pekee! Kwa mida ile, nisingeweza kufanya makaratee yoyote! Nilipoenda kwenye friji, nikakuta kumbe maharage yangu niliyopika mchana bado yapo! Kucheki kwenye kindoo change, nikakuta kuna mchele wa kutosha! Nikajua hapa anasa hamna lakini kulala njaa vile vile hakupo!

  Kuona hivyo, nikaenda hewani, ile binti kupokea nikampa full data..!! Nikamwambia wazi, kwamba hapa nipo alosto ile mbaya kwahiyo kama ana mpango wa kuja akae akijua nini atakutana nacho! Nikamwambia wazi kwamba nilikuwa na buku unusu tu ambayo ndo bajeti yangu ya siku inayofuata!

  Sina hakika kama alizani natania au vipi! Akajibu kwa kujiamini, kwamba POA TU! Kama masihara vile, binti akapanda daladala na akaniambia nimfuate TAZARA. Hivyo basi, ile kufika TAZARA tu, nikajikuta nimeshatumia TZS 300/- na hivyo kubakiwa na TZS 1,200/=! Muda kidogo, binti akafika! Kwa sababu ninazozijua mwenyewe, nikakata shauri la kupanda magari ya kwenda Posta badala ya kuchukua ya moja kwa moja! Ile kufika Posta, kidume nikajikuta nimebakiwa na TZS 600/- tu! Toka posta, tukachukua daladala za TMK…ile kufika ghetto, sina hata thumuni….!!!

  Kilichomtoa kwao, akakipata!

  Siku ya pili akabaki ghetto hadi mchana! Ile anajiandaa kuondoka, nikajikooza na kujiweka sawa!! Huku nikiwa na macho makavu, nikamwambia:

  “Don’t forget ile jana nilikuambia nilikuwa na 1,500/- tu ambayo ilikuwa ndo bajeti yangu ya leo! Hata hivyo, hivyo, ela yote iliishia kwenye nauli na hapa sina hata senti tano!”
  “Kwahiyo?” Binti wa watu akaniuliza!
  “inabidi uniache angalau na buku!”

  Bibti yule alicheka hadi basi…kasha akazama kwenye kipochi chake na kuniacha na gwala (5,000/=)! Kidume nikaua ndege wawili kwa kajiwe kamoja!!

  Nilizani binti yule asingekuja tena; kumbe wapi!!

  MWANAUME MWENZANGU vipi, yashawahi kukuta haya?! Kama hapana, je kama yangekukuta katika situation ambayo nilikuwa nayo ungefanya nini?! Ungeenda kukopa au ungejifanya umesafiri?! Au ungejifanya leo ghetto kuna mgeni kwahiyo aje siku nyingine?! Au na wewe ungeyafanya haya niliyofanya mimi?! Usisahau, hiyo ilikuwa ndo mara yetu ya kwanza kukutana faragha!

  NAWE mdada, ungekuwa ndie wewe….nikakupa ukweli huo, ungekuja tu ghetto au ndo ungekuwa mwisho wa mchezo?!
   
 2. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mi ningekuja kwa sababu sijakupendea hela na si kila siku jumapili kuna siku unazo na kuna siku huna na yote ni maisha,ila ikiwa tabia kwa kweli nakudump mapema,ila ulijikaza wanaume wagumu kweli kushuka namna hiyo,
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwani si alishajuwa huku anakokuja kuko vipi? Nini tatizo sasa?
   
 4. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Hakujua, nilimjulisha !
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  hongera sana.....wapo watu wana story hiyo ya kwako cha mtoto

  ngoja waje..................
   
 6. marrykate

  marrykate JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  ungekuwa mwisho wa mchezo
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  acha nitulie tu
  maana kichowahi nipata ni aibu to the nth degree
  lakini maisha yanasonga, ujana maji ya moto kwa kweli.

  Na ndio maana wazee wana ya kusimulia mengi lol

  keeping it real is the best!
   
 8. wangonyo

  wangonyo Member

  #8
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we nasdaz na wengine wajukuu zangu wote kumbukeni ya kale kwamba mapenzi ni popote kwa hali yoyote, ila ni pale tu kila mtu anapojitoa moyo wake kwa mwenzie, hakuna lishindikanalo katika wapendanao, teh teh teh!!! mmenisoma wajukuu zangu?!!!
   
 9. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Labda upo kibiznez zaidi!
   
 10. marrykate

  marrykate JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  wala, ni dalili mbaya mwanaume kuniomba hela siku ya kwanza, mbona yeye hakuleta shida zake kwako siku hiyo hiyo

  alikuja kukutembelea kwa strehe zake na ndio maana akaja na nauli yake na pengine alikuja ameshiba kabisa, sasa wewe ukajua amekuja kukuchuna ndo maana ukajiwahi kumchuna kwani usingeomba hela siku isinge isha, mwanaume wa type yako sirudiii tena  alijua anakuja kukutembelea kwa starehe zake na ndio maana akaja na nauli yake ili asikupe mzigo,na pengine alikuja ameshiba kabisa hakuwana shida na huo msosi
   
 11. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mi nisingerudi. Lol
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  @maryketi

  kuna kujikuta umechemsha siku ya kwanza bila hata kujua ni kwa nini.

  Bora hata huyu alichemka kwa kukosa hela, wengine tukielezea yalotupata mtasema tulivuta bangi. Things happen, sijui for what reason.
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  sijawahi!
   
 14. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  haijawahi na haitatokea.over
   
 15. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  mimi alishakuja getto nikasonga ugali akajifanya ugali haupandi nimnunulie chipsi si unajua masista duu nikaufinya peke yangu, nikamwambia hela niliyonayo haitoshi chips.
  Akaniomba nauli nikampa 500 alikaa wiki moja hajanipigia simu na mimi nikamkaushia akaona nini sijui akaamua kwenda hewani. Siku nyingine akarudi getto tukapeana mambo
   
 16. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Mie niliwahi kumfanyia ukauzu shoree mmoja! Tulisafiri wote toka arusha kuja dar, siku hiyo nilikuwa njema sana nikawa na vikopo vyangu katoni nagonga kiaina wakati wa safari ndani ya dar express. Katika maongezi binti tukabadilishana namba. Baada ya siku tatu demu tukakubaliana tukutane rose garden, lahaula akaibuka na mwenzie, anakunywa pombe kama maji, niliona hapa watanizidi mfukoni nina hela za kutosha ila sikupanga kuhudumia mangurupembe kama yule asha ngedere aliekuja nae. Nilichofanya ili wasinifilisi, NIKAONGEZA HUDUMA YA POMBE NIKAWA NAZIMWAGA MBILI MBILI THEN NIKAPUNGUZA HUDUMA YA CHAKULA, NIKAAGIZA NUSU KUKU, NDIZI MOJA HALAFU TUKASHEA WOTE. Uroho ukawaisha na ishu nikaondoka nayo lile ngurupembe nikamuunganisha msela wangu alikuwa pale akasepa nalo namie huyoooo nikajisunda kimiani. Then kuanzia siku hiyo nikajua demu ni mlupo so huwa kila akipiga namuambia nipo arusha ila nikiwa na hamu nae nampigia najifanya ndo nimekuja dar! Looools!
   
 17. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  SL njoo ushuhudie visanga vya mmeo,fanya haraka kabla hajadelete!
   
 18. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Hapo uliliwa mkuu pole sana
   
 19. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Kaka acha uchonganishi
   
 20. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Hahahahaha.........
   
Loading...