Umeshindwa kabisa kuacha kujichua?

Umeshindwa kabisa kuacha kujichua?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
KARIBUNI sana rafiki yangu katika uwanja wetu ambao kwa namna moja ama nyingine umebadilisha maisha ya wengi. Inawezekana hata wewe umepata kitu fulani kupitia hapa, maana kila kukicha nimekuwa nikiandika mbinu mpya za kukabiliana na changamoto zilizopo katika uhusiano.

Hebu niambie...umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi, umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? Najua unaona aibu, hasa kama una tabia hiyo. Usiogope rafiki yangu, leo nitazungumza na wewe taratibu halafu mwisho kabisa nitakuacha na tabasamu la nguvu!

Ndugu zangu, wakati mwingine kuna mambo magumu kidogo ambayo baadhi ya watu wanayaonea aibu, lakini yanaendelea kuwa tatizo kwa watu wengi. Leo tutazungumza. Amini usiamini, asilimia 90 ya wanaofanya mchezo huo, hawapendi hata kidogo.

Kila wanapomaliza kujiridhisha huahidi kuacha, lakini baada ya saa kadhaa kupita, wanarudi kule kule. Kama una tabia hiyo, utakuwa unanielewa vizuri zaidi juu ya kile ninachokizungumzia hapa. Hebu twende tukaone.

KUJICHUA NI NINI HASA?
Kwa Kiingereza tendo hili linaitwa ‘masterbation’ likiwa na maana ya kupiga punyeto. Hapa nimetumia kwa ulaini kabisa; kujichua. Lugha nyepesi na rahisi kufikika kwa wengi ni kujiridhisha! Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake.

Namna ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia (artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo zinafanana na sehemu pacha!

Wengine wanatumia njia wanazojua wenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha.

INAWEZEKANAJE KUJIRIDHISHA?
Ni rahisi sana kumaliza tendo la huba kwa kujifanyisha mwenyewe. Silaha kubwa inayotumiwa na waathirika ni kuwavutia hisia watu wa jinsi pacha wakati tendo husika likiendelea kufanyika.

Habari mbaya kwa watu wenye mchezo huu ni kwamba, kwanza wakishaanza, inakuwa vigumu sana kuacha. Inashindikana kwa sababu ni jambo la aibu. Si rahisi kupata ushauri kutoka kwa watu maana ni aibu pia kumweleza rafiki yako juu ya mchezo huo.

Kutokana na hilo sasa, kinachotokea ni kwamba ‘waumini’ wa mchezo huu wanaendelea kuwa watumwa kwa maisha yao yote. Hapa chini tutaona kwa undani jinsi tatizo hili linavyoumiza vichwa vya wengi.

Pamoja na kwamba lina ugumu kujadilika, lakini hapa katika All About Love kwa kutumia lugha nyepesi ya kirafiki bila kuchafua hali ya hewa tutakwenda sawa. Swali lako la kujiuliza kabla hujaendelea kusoma, ni je, upo tayari kuacha lakini unashindwa?

Ni kweli hutaki kuwa mtumwa wa mchezo huu hatari? Zipo athari nyingi sana rafiki yangu ambazo nitazieleza hapa chini. Kama ni kweli unataka kuacha au huna mchezo huo lakini unatambua kwamba, mwenzi wako anafanya, endelea kusoma ili upate elimu hii ambayo huwezi kuipata mahali popote zaidi ya kupitia gazeti hili la Risasi Mchanganyiko.

CHANZO NI NINI HASA?
Jambo la kushangaza ni kwamba, hakuna mdau wa mchezo huo ambaye amefundishwa jinsi unavyofanywa. Wengi wameanza wenyewe, tena wengine bila kujua nini kitakachotokea, lakini baada ya matokeo kuonekana, ndiyo mwanzo wa kutopea huko.
Kwa vijana wa kiume, wengi huanza tabia hii wakiwa kwenye umri wa kubalehe. Mara nyingi hutokea asubuhi wakati wa kuamka, usiku wakati wa kulala au bafuni wakati wa kuoga.

Kwa kawaida, mtu anapokuwa katika sehemu ya utulivu kwa maana ya kupumzika, wakati mwingine mkono unaweza kutembea huku na huko kwenye mwili na mwisho wake bila kutegemea mhusika anajikuta ameshaingia kwenye mchezo huo.

Huwa kama mzaha, akiwa hajui hatma yake, lakini msisimko anaoupata ndiyo unaomchanganya na mwisho wake anashangaa kila kitu kimemalizika. Unajua atakachosema? Sikia: “Mh! Kumbe ndiyo mwisho wake ni hivi? Lakini kama nimesikia starehe hivi...”
Hiyo hutokea pia wakati wa kuoga, ambapo wakati wa kujisugua kwa dodoki, msisimko ukitokea, madhara yanakuwa kama nilivyoeleza hapo juu.

Wenye umri mkubwa au wa kati, huanza tabia hii hasa baada ya kuanza mchezo wa kuangalia video za kikubwa wakiwa peke yao. Kwa sababu wanachotazama kinahusisha msisimko wa mapenzi, basi bila kutarajia hujikuta tayari!
Hii inafanana pia na kwa watoto wa kike, vyanzo nilivyoeleza hapo juu pia husababisha kwa karibu sana.

Sababu nyingine ni kunyimwa au kutotoshelezwa kimahaba na mwenzake. Marafiki bila shaka mnanielewa vizuri...kama nilivyosema lugha inayotumika hapa ni ya kirafiki zaidi, hivyo kama kuna jambo hujalielewa sawasawa, usisite kuniuliza kwa mawasiliano yangu yaliyopo hapo juu.

Ni hamu yangu kuendelea kuelekezana juu ya tabia hii, lakini kutokana na ufinyu wa nafasi, naomba niweke kituo kikubwa hapa. Usikose wiki ijayo, maana ni muhimu zaidi kwako.
 
Umeshindwa kabisa kuacha kujichua?-2-



MJADALA ni mkubwa sana juu ya mada hii.
Wengi imewagusa, lakini kuna makundi mawili; wapo waathirika ambao wanatamani kuachana na utumwa huu na wengine wameathirika zaidi, kiasi kwamba hawana mpango wa kuacha.

Wengine wameenda mbali zaidi, kwa vile hawafikirii kuachana na mchezo huu, wamefikia hatua wanasema kwamba hakuna madhara kwa mtu anayejichua! Nimepokea simu nyingi sana, meseji nyingi na wengine wamejadiliana pamoja na marafiki wengine kwenye ukurasa wangu wa facebook.

Katika mtandao wetu wa globalpublisherstz.com, mjadala ulikuwa mkubwa zaidi.

Watu wanatetea wazi wazi, kwamba kujichua hakuna madhara. Sikia rafiki yangu, hata anayevuta sigara anajua kwamba ina madhara kwa afya yake, lakini ili kujifariji, atajenga hoja kwamba, haimdhuru na badala yake inamsaidia sana kuondoa baridi na haina kilevi.

Wakati mvuta sigara akisema hivyo, mlevi naye atakuja na hoja kwamba, pombe inamsaidia sana kupunguza mawazo. Kila mmoja atatetea upande wake. Ni jambo la kawaida kabisa.

Nikiwa naelekea kuendelea na mada yetu, rafiki yangu mpendwa kama wewe ni ‘muumini’ wa tabia hiyo, unatakiwa kufahamu kwamba unafanya jambo HATARI sana, si tu kwa afya yako, kisaikolojia na dhambi ya uzinifu ambayo hiyo itatokana na uhusiano wako mwema na imani ya dini yako, NDOA yako ipo/itakuwa hatarini.

Nadhani mnakumbuka wiki iliyopita nilieleza maana ya kujichua, namna tendo linavyofanyika na jinsi mtu anavyoanza mchezo huo bila kutegemea. Sasa rafiki, hebu tuendelee kwenye namna tatizo linavyokua.

UKUAJI WA TATIZO
Mwathirika akishazoea, hufanya tendo hilo kama sehemu ya maisha yake. Alianza bila kujua matokeo yake, lakini sasa amejikuta akianza kuupenda na idadi ya ufanywaji wa tendo huanza kupanda, baada ya siku tatu, siku mbili, kila siku na hatimaye kwa siku zaidi ya mara moja.

“Kaka Shaluwa, najichukia sana, yaani nimekuwa mtumwa kabisa wa kufanya huu ujinga.
Kwa siku nafanya mara mbili au zaidi, lakini si chini ya hapo,” alisema rafiki mmoja, aliyenipigia simu baada ya kusoma sehemu ya kwanza ya mada hii wiki iliyopita.

Ukweli ni kwamba, mfanyaji kwa vile ameshapata ‘mteremko’ wa kutimiza haja zake, kwanza ataanza kuwadharau wanawake/wanaume, kwamba hawawezi kumtisha, kwa sababu ana njia za kujifurahisha mwenyewe.

Pili, hufikia hatua ya kuwachukia watu wa jinsia pacha, akiwaona kama ‘wanaringa’ hasa kama atakuwa amemshawishi kimapenzi na kukatawaliwa.

ATHARI ZAKE
Zipo athari nyingi sana ambazo mwathirika anaweza kuzipata kwa kuendekeza mchezo huu. Hapa nataka nizungumze kwa herufi kubwa kabisa kwamba, ndugu zangu usidanganyike kwamba hakuna madhara kwa kufanya mchezo huu.

Yapo MADHARA makubwa sana ambayo yanapatikana kwa mchezo huo. Achana na propaganda za mitaani, zenye utafiti hewa.

Sikia nikuambie rafiki yangu, hasa wewe ambaye unafanya mchezo huo. Upo kwenye hatari kubwa ya kushindwa kufurahia mapenzi, kwa vile mazoea ya kiungo siri chako ni kwenye vitu ‘artificial’ zaidi ya ‘natural’.


Mwanaume aliyezoea kujiridhisha mwenyewe, akikutana na mwanamke, hana muda mrefu sana, kila kitu kinamalizika.

Siyo hivyo tu, uwezo wa kurudia tendo unakuwa mdogo au unakosekana kabisa. Kinachotokea ni kwamba, kiungo siri chake kinakuwa kimeshazoea, aina nyingine ya ‘hali ya hewa’ hivyo kinapokutana na sehemu siri za kike, ambazo ni laini na zenye ute mwepesi, inakuwa rahisi kumaliza ‘biashara’ mapema wakati wateja bado wanahitaji!

Kiungo siri cha mwanaume huwa kigumu, hivyo kusababisha maumivu kwa mwanamke kutokana na sugu aliyoitengeneza bila kujua. Kwa kawaida viungo siri vyote ni laini sana na vinatakiwa kubaki katika hali hiyo ili kuleta msisimko wenye usawa.

Mazoea yoyote tofauti na yale ambayo yanatakiwa hupunguza msisiko na kusababisha mmoja wa washiriki wa tendo la ndoa kubaki na kiu na mwenzake.

“Najuta kuufahamu huu mchezo, kila siku ninapokutana na mume wangu, ananiacha nikiwa sijatosheka. Kiukweli tangu amenioa, sijawahi kufurahia tendo la ndoa. Nilianza huu mchezo zamani sana, tangu nikiwa kidato cha tano.

“Kuna rafiki yangu mmoja nilikuwa nakaa naye bweni moja alinifundisha. Sikujua kama madhara yake ni makubwa kiasi hiki. Ilikuwa ni shule ya wasichana tupu, kwa hiyo akanidanganya kwamba tuachane na wanaume tujichue...kumbe alikuwa ananisaga!” hii ni sehemu ya ushuhuda mwingine wa mchezo huo.

Athari nyingi ambayo mtu anaweza kuipata kwa kujichua ni kumaliza ‘kazi’ mwenyewe bila hata kwenda kazini. Akipita mtu wa jinsi pacha, ambaye ana mvuto, kazi inaishia hapo hapo!

UPO KUNDI GANI?
Uko wapi rafiki yangu? Nazungumza na wewe ambaye unafanya mchezo huo, bado unataka kuendelea nao au unatamani kuacha? Shika maneno yangu, kwamba ni HATARI kujichua, halafu weka nia ya kutaka kuacha huu utumwa, kisha vuta subira hadi wiki ijayo katika sehemu ya mwisho ambayo haitaacha kitu.

Ningeweza kumaliza mada leo, lakini nafasi ni ndogo rafiki yangu.

Ahsante sana kwa kunisoma, wiki ijayo ni muhimu sana kwako, USIKOSE!
 
Sidhani kama kuna vijana ambao hawapitii kamchezo haka,very sorrowful ndoa mashakani sasa
 
itaendelea lini tena jamani!!!

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom