Umeshawahi kupata kazi kupitia LinkedIn?

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,524
4,276
Hii social network huwa wanapost mara nyingi nafasi mbalimbali za kazi pamoja na namna ya kutuma maombi ikiwa ni pamoja na "Easy Apply". Lakini cha kushangaza tangu nianze kutuma maombi sijawahi kuitwa, mpaka najiuliza huenda ni scams tu.

Labda niulize wenzangu vipi kuna yeyote aliyefanikiwa kupata kazi kupitia jukwaa hili?
 
Katika career yangu sijawahi kupata kazi linkedin ila niliwahi kupata paid internship kwenye Kampuni kubwa ya ICT
 
Hata mimi pia najiuliza hili. Kuna mtu namfahamu aliwahi tafutwa na kampuni alikoapply kazi kupitia linkedIn. Nadhani ni bahati tu.
 
Huko ni kugawa vyeti vyako pasi na kujua.

Amini km hujapata ajira mpk leo na una miaka 7 ulishaaply sehemu tofauti na unaufaulu mzuri.

Kuna watu hawajasoma na wanatumia vyeti vyako na ni untouchable.
 
Huko ni kugawa vyeti vyako pasi na kujua.

Amini km hujapata ajira mpk leo na una miaka 7 ulishaaply sehemu tofauti na unaufaulu mzuri.

Kuna watu hawajasoma na wanatumia vyeti vyako na ni untouchable.
Mara nyingi Unatuma CV tu mambo ya certificate attachment ni baada ya kuwa shortlisted
 
hata mimi pia najiuliza hili. kuna mtu namfahamu aliwahi tafutwa na kampuni alikoapply kazi kupitia linkedIn. nadhani ni bahati tu.
Hongera zake.Kiuhalisia zipo nafasi zinazopostiwa mara kwa mara ila binafsi sijawahi kuitwa
 
Katika career yangu sijawahi kupata kazi linkedin ila niliwahi kupata paid internship kwenye Kampuni kubwa ya ICT
Hiyo internship ulipata kupitia post za matangazo LinkedIn ? Au kulikuwa na namna nyingine?
 
Hii social network huwa wanapost mara nyingi nafasi mbalimbali za kazi pamoja na namna ya kutuma maombi ikiwa ni pamoja na "Easy Apply".Lakini cha kushangaza tangu nianze kutuma maombi sijawahi kuitwa, mpaka najiuliza huenda ni scams tu.

Labda niulize wenzangu vipi kuna yeyote aliyefanikiwa kupata kazi.

Hii social network huwa wanapost mara nyingi nafasi mbalimbali za kazi pamoja na namna ya kutuma maombi ikiwa ni pamoja na "Easy Apply".Lakini cha kushangaza tangu nianze kutuma maombi sijawahi kuitwa, mpaka najiuliza huenda ni scams tu.

Labda niulize wenzangu vipi kuna yeyote aliyefanikiwa kupata kazi kupitia jukwaa hili?
Linkedln ili upate kazi unatakiwa kuwa expart kweli kweli au unatakiwa na experience ya kutosha katika kazi husika unayoomba..., vile vile ile package ya premium ambayo unalipia ndio inaweza kukusaidia kupata kazi, platform yao ya bure utasubiri sana
 
Huko ni kugawa vyeti vyako pasi na kujua.

Amini km hujapata ajira mpk leo na una miaka 7 ulishaaply sehemu tofauti na unaufaulu mzuri.

Kuna watu hawajasoma na wanatumia vyeti vyako na ni untouchable.

Duh
 
1. Ukiona kuna EASY APPLY na kwenye description wametoa Email ya kuwatumia application letter na CV, TUMIA NJIA ZOTE MBILI

2. ukiapply kupitia linkedin, kama application yako ikisomwa utatumiwa notification au hata Email. Kama hupati hii bhasi jua huwa hazisomwi

3. Je, CV yako ipo vizuri na Je inaendana na job description ya kazi husika. Kama unatumia CV moja kwa kazi zote bhasi anza kutwist CV yako iendane na kazi unayoiomba. Ni muhimu sana hata nje ya linkedin

4. Kupata kazi linkedin ni rahisi kama upo active na unaonesha ujuzi wako kupitia posts bila kusahau NETWORKING, kutengeneza personal relationships na wazito baada ya kuonesha value yako, some people watakupa recommendation na recruiters ni rahisi kukupata..
Hii ndio njia effective zaidi niliyoithibitisha mwenyewe, sijui kwa wengine
 
Back
Top Bottom