Umeshawahi kuona Waafrika wakienda kusimamia uchaguzi Ulaya?

terrat

JF-Expert Member
May 6, 2015
204
100
Ulishawahi kuona nchi yoyote ya afrika imetuma waangalizi wa uchaguzi wakasimamie uchaguzi Ulaya na Marekani?

Je kuna jumuia au taasi ya aina yoyote iliyowahi kwenda kusimamia uchaguzi Ulaya na Marekani?

Kwanini?

Wao ndio walioasisi mambo ya siasa na uchaguzi tangu enzi za dola ya Athens.

Afrika ilikuwa nchi moja ikiwakilisha jina la kitongoji kimojawapo ambacho leo kinaitwa nchi ya Tunisia, ilikuwa na miundo yake ya utawala wa kitemi, mtawala aliteuliwa na mtawala naye kuteua mtawala na kumteuwa mtawala na nchi (koo,Kabila,jamii) ambazo kwahakika zilikuwa tuli. Lakini vita baina yao haikuepukika kwani iliasisiwa tangu ulimwengu kuumwa.

Demokrasia ya Afrika haitaletwa na Magharibi, bali ukoloni utadumishwa na magharibi kwa mgongo wa demokrasia.

Kuukwepa ukoloni wa mabeberu leo ni ngumu sawa na kumkwepa Azam Bakhresa Tanzania
 
Ulaya ndio wanagharamia chaguzi zetu, lazima waje waangalie pesa yao ilivyotumika.
 
Hata wakienda kusimamia uchaguzi, hizo kasoro watakazozikuta watazipeleka wapi? Ndio maana namkubali sana Mugabe, sasa hivi anapigania angalau kwa bara la afrika tuwe na mataifa mawili yenye kura ya veto katika umoja wa mataifa.

Ulishawahi kuona mwiz anaenda kumsimamia asie mwiz!?? Huoni huyu mwiz atampotosha aise mwiz awe mwiz japo haiwezekan kwa mzungu kumwelewa??
 
Kwa akili za wasimamizi wa chaguzi zetu tuendelee kudhulumiana sisi wenyewe tena kwa hili napongeza sana majitu meusi tunadhulumiana kwenye chaguzi hata mtu afe lakin lazima mshindi awe fulani
 
Wataendaje na wakati waho hawagaramii garama ya uchaguzi wa nchibza ulaya
 
Back
Top Bottom