Umeshawahi kujiuliza?

Umeshawahi kujiuliza?

Ukweli1

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
550
Reaction score
333
Kama baba angekuwa baba bora kwa watoto wake na mume mzuri kwa mke wake, mama angekuwa mama bora kwa watoto na mke bora kwa mume wake.

Watoto wangeangalia wazazi na kutamani nao kuishi na kuwa na wenzi wao. Dysfunctional families imekuwa chanzo cha matatizo mengi sana, watoto kuingia katika makundi ya ajabu, wazazi kuchelewa kujua kuwa mtoto keshaharibika.

Mzazi anasoma kwa gazeti kuhusu mtoto wake, hii ni ishara ya kukosekana kwa mawasiliano mazuri katika familia, maana hata kama mzazi angekuwa kapitiwa ndugu zake huyo mtoto wanakuwa wapi? Ujenzi wa Taifa bora unaanzia katika ujenzi wa familia.

Ukishaharibu kwenye familia Taifa linabomoka. Moja ya mambo yanayotokea siku hizi watoto kujiunga magroup hatarishi watu wanajiuliza huyu mtoto ana kila kitu nyumbani, wanasahau kujiuliza je nyumbani kuna upendo, kuna amani, kuna mawasiliano.

Wewe endelea kutokumjali na kumheshimu mzazi mwenzio, kujibizana na makelele mbele ya watoto, kutokujali hisia za watoto, unawapa hela unaamini hayo ndio majukumu yako kama mzazi, unaact kama sponsor na sio mzazi, hauna chochote watoto wako wanachojivunia isipokuwa fedha yaani wakikumbuka baba au mama hasira inawaajia jinsi ambavyo kutwa wewe ni kelele au dharau kwa mzazi mwenzako,

Hauna muda nao na wala hujui ni mangapi wanapitia. Single mother/father naye anaweza lea vizuri kwa kuepuka kupanda mbegu za chuki kwa watoto na kuwa na muda na watoto. Kuna ya kulaumu serikali ila mengine ni sisi wenyewe wazazi tunatengeneza majumbani kwetu.

"Money and Fame are not everything"
 
Unataka kutuambia kwamba Human behaviours should be equal and not as Lord Robins, the master of economics argued?
 
Niliwahi ku argue na mtu kuwa, ndoa na maisha ya ndoa mtu hujifunza akiwa bado mtoto, jinsi wazazi wake wanavyoishi na taratibu anajifunza kadri anavyokuwa. Ukiwa na familia bora, baba anampenda mama nae mama anamheshimu baba....utakuwa katika maadili hayo na hata ukija kuwa na familia yako uwezrkano wa kutaka kuishi maisha ya wazazi wako ni mkubwa.

Tatizo mnaanza kuwafindisha vijana kuhusu ndoa wakiwa 25+. Msitegemee familia bora.
 
Unataka kutuambia kwamba Human behaviours should be equal and not as Lord Robins, the master of economics argued?
I don't know where you are getting all that information, let me rewrite what I said before, it is about good relationship, communication, love and peace at home, there chances that kids can misbehave but if you are close to them as a parent you should be able to foresee, it is only about having a good communication between you parents, between children, and between parents and kids.
 
Niliwahi ku argue na mtu kuwa, ndoa na maisha ya ndoa mtu hujifunza akiwa bado mtoto, jinsi wazazi wake wanavyoishi na taratibu anajifunza kadri anavyokuwa. Ukiwa na familia bora, baba anampenda mama nae mama anamheshimu baba....utakuwa katika maadili hayo na hata ukija kuwa na familia yako uwezrkano wa kutaka kuishi maisha ya wazazi wako ni mkubwa.

Tatizo mnaanza kuwafindisha vijana kuhusu ndoa wakiwa 25+. Msitegemee familia bora.

You nailed it, ni vizuri tubadilike na kuanza nao wakiwa wadogo.
 
Niliwahi ku argue na mtu kuwa, ndoa na maisha ya ndoa mtu hujifunza akiwa bado mtoto, jinsi wazazi wake wanavyoishi na taratibu anajifunza kadri anavyokuwa. Ukiwa na familia bora, baba anampenda mama nae mama anamheshimu baba....utakuwa katika maadili hayo na hata ukija kuwa na familia yako uwezrkano wa kutaka kuishi maisha ya wazazi wako ni mkubwa.

Tatizo mnaanza kuwafindisha vijana kuhusu ndoa wakiwa 25+. Msitegemee familia bora.

Umesema ukweli, aliniambia mtu mmoja kuwa wao kupiga mwanamke ni kitu cha kawaida kabisa, na ukiangilia nyumba nzima kwao hakuna aliyeweza kuishi na mke, nilipochunguza sana nilikuja gundua, enzi za wazazi wake nyumba ilikuwa uwanja wa fujo, baadae wazazi wakaja kuokoka ila ilikuwa too late kwani tayari watoto waliisha adopt hiyo tabia.
 
Back
Top Bottom