Umeshawahi kuachana na mpenzi wako kwa sababu umeona mahusiano yenu "hayatofika mbali" (hamjagombana kabisa)

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,985
Kwa mimi nimeshawahi kukatisha safari baada ya kuona hili gari hili sitoboi nalo Kigoma, safari lazima iishie njiani tu maana sio kwa ma mushkeli haya.

Nilipata mpenzi huko nyuma tukapendana vizuri tu, maisha yakawa yanaendelea. Si unajua tena mnapokuwa wapenzi lazima kila mtu ajue ratiba za mwenzake hata kama hatupo pamoja ila akiulizwa sasa hivi CONTROLA yuko wapi anajua cha kujibu kadhalika na kwangu.

Jumapili ni siku ya ibada yeye yupo kwao na mimi kwangu kila ikifika Jumapili mimi naenda zangu kanisani nikirudi namcheki mwenzangu namuuliza vipi za ibadani, ananijibu kuwa hakwenda, ukimuuliza kwanini anakwambia alikosa nguo, basi unauchuna.

Ikifika Jumapili ijayo hivyo hivyo haendi sababu yake ni nguo/uchovu/kuumwa aseee nilimwambiaga ukweli mkavu kabisa ila bado tabia ikawa ile ile, nguo za kutoka mitoko anazo kama 100 na ushee ila za kanisani hana. Ikikaribia Jumapili nguo zote zinachafuka.

Yule dada nilimpiga chini maana nilijihisi na-date na pepo maana hata tukiwa pamoja ukimwambia ombea chakula "hataki" ukimlazimisha ataishia kuanza kula bila kuomba, nikaona isiwe kesi nikaachia nafasi wengine.

Another one

Alikua ni mpenzi wangu tulipendana haswaa. Siku moja nilikuwa zangu nimekaaa nacheki Tv nikamuuliza "Hivi una salio kwenye simu yako, nataka kumtumia mama" akaniambia simu haina hata salio kuna 5000 tu", nikamwambia hiyo hiyo mtumie mama kwa vocha itamtosha sana akanijibu "Aisee unawezaje kumtumia mama Tsh. 5000 ya vocha mwanaume mzima?

Nikamuuliza swali "eti umeniulizaje?" akarudia swali lake "unamtumiaje mama 5000 ya vocha mwanaume mzima?" nikamwambia huo ndio uwezo wangu kuliko nisimpe hiyo 5000 akae bila vocha si bora nimtumie hiyo najua atajiunga vifurush kidogo kidogo na hatoitumia yote,ila yule mwanamke alinikatalia katu katu.

Akaniambia wewe mtumie mama hata 10,000 kidogo ita leta maana, nikamsisitiza siwezi tuma zaidi, akasema basi mwache akae hivyo hivyo au kakope hata kwa mtu umtumie, aseee tukiacha masihara yule dada nilimwambia live pale pale "naomba uondoke kwako niache kidogo" kweli akaondokaa.

Sikumtafuta tena na ndiyo ukawa mwisho wangu na yeye, kiufupi nina list ya magari kadhaa niliyositisha nayo safari kutokana nakuona huko mbeleni hatutokuja kuwezana kabisaaa, so nikaamua tu kujiongeza.

SweetieLee Ulishawahi anzisha thread fulan hivi ya kumkinai "crushie" wako sasa ile situation ebu fanya hakua just a crushie ila mliendelea hadi mkawa wapenzi then baada ya wiki mbili au mwezi unamkinai au inatokea tu kitu anakufanyia "kinakuchefua kabisaaa"

Kuna dada nilimuuliza hili swali akaniambia yeye pia kashawahi muacha mtu, kisa ilikuwa kampenda jamaa vizuri jamaa alikuwa mtu mstarabu kupita maelezo ila hakuamini siku wanafanya mapenzi jamaa akawa anasisitiza anataka TIGO asee yule dada akaniambia CONTROLA nilimuangalia yule kaka juu mpaka chini kisha nikainuka nikavaa nguo nikasepa na ndiyo ikaawa mwisho wa mazoea na yule mkaka.

Haya na wewe tuambie ilikuaje ukamuacha ukasitisha safari.

Note: sababu isiwe UGOMVI au mkwaruzano wa aina yeyote ile
 
Kuna mmoja huyo alikuwa ni vizinga tu mwanzo nilikuwa nampa kama anavyotaka nikihisi ataona aibu kwa vizinga vya kila mara.

Kadri navyo mpa ndivyo anaongeza moto walahi nilikimbia mahusiano.

Walahi yule alikuwa hana aibu si kwa vizinga vile karibia kila siku.

Hata papuchi sikugusa maana sikutaka aseme nimechakata papuchi ndio nimekimbia.

Nilikimbia kiroho safi ila si kwa vizinga vile.
 
Kuna mmoja huyu Juzi Juzi nimeona niachane nae maana niliona Safari ya kuanzia Mtoni kwa azizi ally mpaka Mbagala Tu haiwezekani

Kisa kiko hivi beibe nimeichoka IPhone yangu 7+ nataka XR, nikamwambia Mfuko wangu unaweza ku Afford 8+ hiyo XR siwezi si kwamba sina ila siwezi weka bajeti huko kwenye mambo ya fashion na luxury ambazo Kimsingi hazina mwisho na kila siku zinatoka mpya

Majibu yake sasa ooooho hauwezi kunipangia choice unayotaka wewe mimi natumia brand ninayotaka Mimi, nikajisemea Dooh hapa gari haiwezi kufika Safari nikashuka njiani

Nb; Sikulalamika nikamuacha na Maisha yake, Jaribu kumbadilisha mwenzi wako ukiona haiwezekani Walk away Don’t kill yourself
 
Silence kills it silently and diplomatically, no arguments no explanation nothing and there won't be ever...

Chapter closed, another one is opened...

Aluta Continual....

K' Matata.
even a single word?

seriosly...
 
Cole Williams,
kuna vyakum'badilisha ila mwanamke mwenye tamaa huwezi mbadilisha nakwambia

Huyo macho yake ni juu juu tu

Ungekua nae ukaja nunua ka I.S.T atakwambia "sasa hako kagari gani na wewe"

mwanamke mwenye macho juu juu mimi sim badilishi "namuacha"

Ntakubadilisha vitu vingine.....
 
CONTROLA

Naomba usinikumbushe, niliwahi date mwanaume ana maneno huyo..!! Yaani ukikosea usiombe vichambo vyake utajuta!! anakuchamba mpaka unahisi uchizi, vile ukijishusha kuomba radhi ndo kama unachochea moto wa kuchambwa, na vile I hate offensive words niliondoka kimya kimya hata sikuaga.! Mpaka Leo I can't date mtu wa kunitukana hata kidogo maana hiyo ni ticket ya one way to the 'delete button'..!!

Mwingine huyo alikuwa ana wivu huu wangu hauoni ndani, in fact huu ukasome, let say mnaongea ukamuambia I got to do something, anakuambia how long will it take? unajibu only 10 minutes sababu nataka kukosha vyombo, After a while anapiga, unajibu umemaliza ila unadeki, haha' utajuta unaambiwa ulisema tu vyombo hukusema kama kuna kudeki.!! Hapo ujue kashamaindi muda sana, yakanifika haaaapa.!! Jamani nilikimbia speed mfanowe hakuna.!!
 
SweetieLee,

Umenikumbusha mbali pia my dear, iliwahi nikuta mkaka anachamba kama muimba taarabu na ana wivu sio mchezo siku moja alipiga bahati mbaya nikawa mbali na simu aliongeaaa, alitukanaaa alichonikera ni kunitukania mama angu nilijibu jibu moja tu nikamwambia hapa hujanioa ukinioa si utanitukania ukoo mzima?? Nilinyala kimya kimya mpaka leo
 
SweetieLee kumbe watu mna mapito yenu ya kimya kimya

pole sanaaaa

huyo jamaa ako wa kwanza sikua mimi kweli jamani

maana nimejirekebisha hata wiki sina,na hayo malamiko ndio yale yale yaniiii
 
Watu Mungu mnampenda kumbe ila kwa nini amri zake hamfuati? Back to topic, unaweza kumwacha mtu kwa kuwa eti hamtofika mbali kumbe yeye hana mpango wa kwenda huko mbali kwa hiyo ni vema ukaendelea kujiburudisha tu
muda wa kujiburudisha huwa ni mchache

hamna anaependa kujiburudisha kwenye miili ya wadada kila leo

labda ziro aikyuuu ila wengine sisi tuna wish kama Lait angepatikana mmoja tu halafu tuendane Daaah

Amri 10 unaziona chache eee,ila usiombe kujaribu zifatisha kwenye matendo,unaeza jihisi uko JELA (Gwantanamooo)
 
Back
Top Bottom