Umeona nini kwenye maziko ya yule tajiri wa Kibaniani, Patel tokea mwanzo hadi mwisho?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Asilimia 99 ya waliohudhuria wamevaa barakoa, hili mliliona? Na kujiuliza kulikoni, jamii ya mabaniani ndio karibia wote wamevaa hizo barakoa na sisi tuliokoza rangi ya kiza baadhi walikuwa hawakuvaa kitu, kwenye wafanyakazi wote wamevaa?

Bado unaamini yule kimelea hayupo Tanzania? Na hivi karibuni kumeongezeka vifo vya wazee wazee na tunaopata matangazo tu ni hawa matajiri au vingunge na walio kwenye jamii maarufu kama wasanii, tulio wengi pangu pakavu hutusikiki.

Sasa rudia kuangalia kideo ya mazishi ya Patel, Je, alikumbana na vimelea huko South Africa? Sababu gani jiulize iliyofanya wahudhuriaji kuibuka na barakoa ghafla bin vu?

Anza leo kuvaa barakoa usisikilize redio vifua.
 
1. Tafuna tangawizi kila siku asubuhi na jioni.

2. Kunywa maji ya uvuguvugu yaliyotiwa binzari mbichi (turmeric) ama ukikosa tumia ya unga pamoja na mdalasini wa magome wa India, kila asubuhi na jioni.

3. Kula matunda ya kutosha kutwa nzima, ikiwezekana mlo mmoja kati ya milo yako 3 ya siku uwe matunda tu.

4. Kunywa maji ya kutosha walau lita 2 hadi 3 kwa siku, vyema yakawa ya vuguvugu.

5. Fanya shughuli ambayo itakutoa majasho kila siku walau kwa dakika 20 hadi 30.

Afya njema ni maamuzi ya mtu binafsi.

Kasinde Matata.
 
Yupo lakini miili yetu ina mu-undertaker kama kawaida. Tunaugua mafua hatuend hospita yanapona tu, hata malaria inaweza kuja ikapona tu, yani sisi miili yetu ishazoea shuruba ngumu ngumu. Maj tunakunywa ya bomba mengine ya kariakoo, yamefungwa fungwa tu na bado tuna survive. Corona naye atakumbana na miiili hii hii.

Ila haya yote haimaanishi uwa hakuna wanaokufa, wapo hata mimi bibi yangu alikufa kwa sababu ya mafua mwaka 2005. Wapo ambao Corona itaondoka nao tu kama inavyoondoka na baadhi kwa Malaria , au kipindupindu. Chukua hatua ila isiwe sababu ya kutufungia ndani. Tutaishi nayo tu kiakili.
 
Corona ni mpango wa kuwafanya watu watumie teknolojia za mawasiliano zaidi kuliko kukutana uso kwa uso. Na hii inawanufaisha sana makampuni yanayojihusisha na teknolojia hizo. Ukichunguza kwa makini unakuta wamiliki wa makampuni haya ndo wako bize kweli kuhusu kupiga propaganda za uwepo wa corona hata sehemu ambapo haupo. ( Nawaza!)
 
Doh! Nimeandika na kufuta zaidi ya mara tano!!
Ngoja niandike hivi Kwa kujiamini kabisa kwamba, Mleta Uzi ni mpumbavu!!!
Umejiamini sana mpaka baba yako unamuita mpumbavu,sawa mwanangu ila kutahadharisha kupo,halafu tuna misemo mingi sana,ya kilugha kama kinga ni bora kuliko tiba.

Jihadhari kabla ya athari. Kama haitoshi mliangaliza vizuri kuna maji chiririka na sanitaizha kila sehemu ya kuingilia,nilishangaa sana ,nikaona sio bure.

Na nikifikiri misemo yetu mingine kuitamka yataka ini mfano mficha uchi hazai,je tunaficha ,kubwa ninaloliona Serikali yetu haijamzuia mtu kuchukua tahadhari wala kupiga marufuku kuvaa barakoa.

Hili gonjwa lipo sasa mpaka kufikia waizraeli kuchukuwa kinga basi ujue mdude upo. Msemo wetu ule wa kama halipo linjiani linakuja.
Tuzidishe kujifukiza na vile vibanda virudi wapita njia tusioweza kwenda south tubaki hapapa kando ya equator na dawazetu asilia,japo mtu akienda sokoni na vihela vyake anaweza kutumia.

Kuna kitu nimesikia si vibaya nayo ni kunywa chai iliyomoto sana iwe ni kawaida tena mara nyingi unazoweza na kabla hujakunywa basi vuta ule mvuke kiasi cha umoto unaoweza kuuhimili.
 
Corona ni mpango wa kuwafanya watu watumie teknolojia za mawasiliano zaidi kuliko kukutana uso kwa uso. Na hii inawanufaisha sana makampuni yanayojihusisha na teknolojia hizo. Ukichunguza kwa makini unakuta wamiliki wa makampuni haya ndo wako bize kweli kuhusu kupiga propaganda za uwepo wa corona hata sehemu ambapo haupo. ( Nawaza!)
Ndugu ondokana na upotoshaji huo wala usiuamini,huyu kimelea kama nungunungu yupo,chukua wakati wako guguli yuchubu kwenye habari uone watu wanavyopata uzoefu wa kupigwa kabari ndugu ni shida usiombe,ulimuoa Boris alivyotoka unahisi kabisa jamaa alichungulia kifo.
 
Nina wasiwasi na hawa wanaotoa kiburi na kusema huyu kimelea aliekaa kama bomu la baharini kulipuwa meli ni hadithi za paukwa na pakawa,na dharau nyingi kujiona wao wanapeeeeeehndwaa na Mungu,ukijiuliza kwa mema gani unawakuta hawana,jeuri zao hizi hazifai watubu.
 
Unadhani

Unadhani hayo yote billionea hakushauriwa/ hakuambiwa...?
 
Back
Top Bottom