Umeme wa upepo kuzalishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme wa upepo kuzalishwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 28, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Serikali imeingia ubia na Kampuni ya East Africa Power Pool wa kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida utakaogharimu zaidi ya Sh. Bilioni 180.
  Akizungumza mjini hapa juzi, Naibu Wazir wa Viwanda na Bishara, Lazaro Nyalandu alifafanua kuwa Serikali imeingia ubia huo kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na kusaini makubaliano hivyo kinachosubiriwa ni uzalishaji wa umeme ambao utaingia katika gridi ya Taifa kuanza.
  " Tangua kuanza kufungwa kwa mitambo itachukua takribani miezi 15 ili umeme uingie katika gridi na hii itakuwa ufumbuzi wa matatizo ya umeme kwa sasa, " alisema Nyalandu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Kaskazini wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
  Alisema katika makubaliano hayo Serikali itakuwa ikimiliki hisa za asilimia 51 na nyingine zitabaki kwa mwekezaji binafsi na kuwa anatarajia kazi ya ujenzi itaanza mara moja.
  Mkurugenzi wa Viwanda Vikubwa wa NDC, Alley Mwakibolwa alisema ujenzi wa mitamboya kutumia upepo itasaidia kuzalisha umeme mapema kwanihuchukua muda mfupi kuwekwa ikilinganishwa na ya maji au gesi.
  " Tutajitahidi mradi huu uende kwa kasi kubwa kwani kwa kuanzia tutazalisha megawati 50 na baadaye tutaongeza 50 ili kuingia katika gridi ya taifa, " alisema Mwakibolwa.
  Alisema kwa kuingia ubia wa namna hiyo itasaidia kupunguza gharama kwa taifa kwani gharama za umeme huo ni rahisi kuliko umeme wa aina nyiongne na kuwa Shirika hilo litalinda maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla.
  " Tuna maeneo mengine ambayo tunaweza kuzalisha umeme ikiwa ni wa makaa ya mawe na kwa mikoa ya kusini katika machimbo ya makaa ya mawe tunaweza kuzalisha zaidi ya megawati 1800 wakati mahitaji ya nchi jkwa sasa ni 800 tu”
  Alisema kwa jinsi hiyo nchi itaanza kuuza umeme kwa nchi za jirani hususan za Afrika Mashariki na tayari viongozi wa nchi hizo wamekubaliana kuiachia Tanzania kuzalisha umeme kwa ajili ya nchi zote tano.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Power Pool East Afrca, Machwa Kagoswe alisema wameagiza mashine zinazoweza kumudu upepo wa Singida kwani kwa kawaida katika nchi za Ulaya wanazalisha umeme wenye kasi ya mita tano kwa sekunde wakati wa Singida hufikia hadi mita 21 kwa sekunde.
  “Huu ni umeme mkubwa ndiyo maana tumeweka oda maalumu ya mitambo itakatoweza kuhimili upepo huu... natumaini hii itakuwa njia rahisi ya kuzalisha umeme mwingi kwa gharama nafuu," alisema.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...