Umeme wa TANESCO kupanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme wa TANESCO kupanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BASIASI, Aug 14, 2011.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,109
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Umeme wa Tanesco kupanda

  Na Cosmas Mlekani
  14th August 2011
  • Hautawagusa wananchi wa kawaida
  Serikali imesema kuwa italiruhusu Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kupandisha bei ya umeme baada ya bidhaa hiyo kupatikana kwa uhakika.

  Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja wakati akiwasilisha Bungeni mpango wa dharura wa wizara yake wa kukabiliana na mgawo mkali wa umeme unaoendelea nchini kote.

  Awali, bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2011 na 2012, iliwasilishwa Bungeni Julai 18, mwaka huu kabla ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuiondoa hoja ya wizara hiyo baada ya kupingwa na wabunge na kutakiwa kuwasilisha mpango wa dharura wa kukabiliana na mgawo wa umeme.

  Pinda wakati akiondoa hoja hiyo alisema kuwa Serikali inakwenda kusaka pesa na ingelazimika kupunguza posho za watumishi wake ili kukomesha tatizo hilo la umeme nchini.

  Hata hivyo, Ngeleja jana akiwasilisha mpango huo wa Wizara ya Nishati na Madini alisema kuwa marekebisho hayo ya bei hayatagusa wananchi wa kawaida na badala yake watagusa watumiaji wakubwa, wazalishaji wakubwa na migodi ya madini.

  Alisema kuwa wameitaka Tanesco kupeleka mapendekezo kwa Mamlaka ya Udhitibiti wa Nishati na Maji (Ewura), kuhusu marekebisho hayo ya bei, huku Shirikisho la wenye viwanda nchini (CTI), likiridhia hatua hiyo endapo umeme utakuwa wa kuridhisha.

  Alisema kamwe marekebisho hayo hayatawaumiza wananchi wa kawaida hata kidogo.

  "Hatutagusa bei za wananchi, hatutawaumiza wananchi hata kidogo, "alisema Ngeleja huku akisisitiza kuwa hatua hiyo itafanyika baada ya kupatikana kwa umeme wa uhakika.

  Pia, Ngeleja alisema mpango mwingine wa wizara yake kuhakikisha tatizo la mgawo wa umeme linapungua au kumalizika kabisa, Serikali imesamehe kodi zote katika mafuta yote yatakayotumika kuzalisha umeme.

  Mpango mwingine ni ule wa Serikali kuiwekea dhamana Tanesco, ili iweze kukopa benki, huku wizara hiyo ikiondoa kiasi cha sh. bilioni 3.8 kilichowekwa kwa ajili ya kujenga ofisi ya Kanda ya Mashariki, ambapo sasa fedha hizo zimeingizwa katika mpango huo wa dharura wa kumaliza mgawo wa umeme.

  Kiasi kingine cha sh. bilioni 1.8, ambacho kiliwekwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi huko Songosongo Kilwa mkoani Lindi, nacho kimeondolewa na kuingizwa katika mpango huo wa dharura, na wameondoa sh. bilioni 10 zikiwa ni posho mbalimbali.

  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), nalo limepewa kibali cha kuingiza mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 150, ambapo Oktoba wataanza kuzalisha megawati 50 Novemba 50 nyingine na kukamilisha kiasi hicho cha umeme.

  Alisema miradi yote ya dharura inayotarajiwa kutekelezwa inatarajia kuzalisha jumla ya megawati 1,032, zikiwemo 572 kati ya sasa na Desemba mwaka huu na zile za megawati 460 zaidi ifikapo Desemba mwaka 2012.

  Alisema kuwa gesi itakapotumika kuzalisha umeme, itasaidia kupunguza gharama za nishati hiyo kwa karibu asilimia 60.

  Alisema kuwa mpango huo wa dharura wa kumaliza tatizo hilo la umeme hautaishia mwezi Desemba peke yake, bali utakwenda hadi Machi mwakani.

  Jumla ya wabunge 258 waliochangia kwa maandishi na wengine kupata muda wa kuzungumza wakati wa kuchangia hoja katika bajeti hiyo ya Wizara ya Nishati na Madini.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Wenye viwanda wanawauzia wenye viwanda wenzao au wananchi wa 'kawaida'!?
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nadhani alikusudia tufidie takrima walizopekea katika mpango wa dharura.
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Madhara yatatufikia watumiaji kutokana na bidhaa wanazozalisha watazipandisha bei.
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Km wana nia ya dhati kwa mwananch wa kawaida WASIMAMIE BIDHAA HATA 1 ISIPANDE BEI NA SIJUI NI KIWANDA KIPI KITAKUBALI KUJIENDESHA KWA HASARA vinginevyo WANANCH TUTAENDELEA KUUMIA MARA DUFU
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Ninavyokumbuka ni kuwa tanga cment hawalipii umeme, huenda kunawengine wengi. Kwa hiyo wataanza kulipia umeme.
   
 7. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Walalahoi wa Tanzania tunafanywa mazuzu sana,sasa iweje gharama ya nishati viwandani ipande alafu bidhaa ziuzwe kwa bei ya zamani?hapa hata kayumba anaelewa kitakachofata nini,haiitaji hesabu za BODIMAS wala 11r2/7 kupata jawabu
   
Loading...