Umeme vijijini: Waziri Muhongo awataka wakandarasi kukamilisha usambazaji umeme

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili kufanya kazi kwa kasi zaidi ili umeme uweze kuwafikia walengwa kabla ya mwezi Juni mwaka huu.

Akizungumza na watendaji kutoka kampuni ya CCC International Nigeria Limited, inayosambaza umeme katika mkoa wa Manyara, Profesa Muhongo alisema kuwa hajaridhishwa na kasi ya kampuni hiyo katika utekelezaji wa miradi ya umeme katika wilaya ya Simanjiro ambapo hakuna wateja waliounganishiwa umeme.

Pia, Profesa Muhongo amelitaka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kufanya kazi kwa karibu na wakandarasi hao katika kutatua changamoto zinazowakabili ili waweze kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Aliwataka mameneja wa TANESCO kuongeza juhudi katika kazi zao ikiwa ni pamoja na makusanyo, utatuaji wa changamoto na uunganishaji wa umeme kwa wateja, na kusisitiza kuwa meneja atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake ataondolewa katika nafasi yake.

Awali, akielezea changamoto katika utekelezaji wa miradi ya umeme meneja mradi kutoka CCC International Nigeria Limited.Zhang Jiangaang, alieleza kuwa wamekuwa wakiibiwa vifaa vyao vya kazi kutokana na kuwepo kwa usalama mdogo hivyo kupelekea kutokamilisha mradi kwa wakati kutokana na hasara wanayoipata.
 
Kumekucha... Mara Nigeria mara Meneja Mchina Mara Vifaa Vinaibiwa Mara Usalama Mdogo? Mara Pesa zimezuiliwa na Marekani Mara Utawala Unaonyima watu uhuru wao... Utawala Huu Hakuna rangi tutakayoacha iona....

Sugu tuletee kile kibao cha Mzuka... Jeni kabanwa
 
Asante Muhongo kwa ujumbe murua kwa watanzania kwamba umeme lazima ufike vijijini no matter what or how!
 
Back
Top Bottom