Umeme, umeme, umeme, wapi umeme?

Umeme, umeme, umeme, wapi umeme?

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,580
Reaction score
23,915
Huku bandari, pale bashite, kulee genge limetulia,
Umeme kukosa mteteaji ndio mpango wenyewe,
Wateteaji wako bize kukimbizana na Bashite,
Na wengine wako bize wakikosoa mikataba.
 
Kwa Tanganyika umeme umekuwa anasa.
Kwa vipofu wasioona mwanga ni anasa.
Kwa sasa giza kwetu ni fahari.

Eti wapo wanaolilia umeme...wa nini?
Mbona mababu zetu waliishi bila shida?
Hawakuwa na umeme.

Watanganyika ni watu wa ajabu kweli kweli.
Tunadai kuishi kivyetu hatutaki kusihi kivyao!
Mbona tunalilia mwanga na jua lipo?

Hakika kwa tunavyoishi ndani ya mchi hii.
Heri kulala mchana na kutenda usiku.
Vitendo vyetu hakika ni vya gizani.
 
Back
Top Bottom