Umekata Tamaa! Sema maneno haya

Nov 2, 2020
68
90
Changamoto unazopitia zinakuumiza na kukuhangaisha.
Hii ni sehemu ya maisha ambayo kamwe haiepukiki Wala haizuiliki.
Kuna wakati unajiuliza,Mungu uko wapi na hata mimi naandamwa na kusumbuliwa na dhiki.

Mungu kama unanisikia ,nakuomba mitihani hii mbali kwangu izidi pitia.
Mbaya zaidi ni pale lile ulilolipambania kwa muda mrefu ukiamini linafanikiwa na kukutoa kimaisha,Ndio kwanza linaharibika na kukufanya urudi chini kuliko ulivokuwa hapo awali.

Ni hali haielezeki ,Ni hali haitabiriki,Ni hali ambayo Kila saa uitamani kuishuhudia lakini Ndio kwanza inakulazimisha katika Maisha yako kukutokea.
Hakuna maana kamili ya uchungu wa yale magumu unayoyapitia,Kwani wa pembeni ni rahisi kuyarahisisha asijue ni ugumu kiasi gani ulionao.

Wakati mwingine unaweza kushindwa kutoka ulipo kwa kusubiri wa pembeni ajue maumivu unayopitia.

Au akuonee huruma ya maneno na hisia Ndio ujue kuwa Sasa unapaswa kuchukua hatua.

Wewe unayopitia hali hiyo,Ndio unatakiwa kuwa wa kwanza kusema na wewe mwenyewe.

Sema nawe polepole ,jiliwaze na jiambie kuwa,Lazima nipitie hali hii,na nitakomaa kadiri ya uwezo ili nifike nitakapo.

Najua nitateseka,najua nitahangaika,najua nitataabika,Lakini hapa bado Nina jukumu la kujipangusa,ili hatime mbele niendelee.

Nakubali nimewapoteza marafiki wa muhimu,Mpenzi aliyekuwa karibu nami na hata ndugu ambao mwanzo kwao mi nilionekana na thamani.

Nawaona wanavyonikimbia,Lakini sitaki kujilaumu kwa kuwa sehemu ya msaada na mchango wa hapo walipofika ,Kwani wao kukataa kuwa nami,sio kigezo Cha kufuta mazuri yangu kwao yaliyowafanya kuwa na muelekeo.

Sio jukumu lao kuitafuta furaha yangu.

Hili ni jukumu langu mwenyewe.

Cheko langu ni mini,huzuni yangu ni mimi.

Mafanikio yangu wao ni Kama wananisaidia,Lakini ni mimi ukweli wa kiasi gani nabaki nikiujua.

Pembeni yangu Niko mimi,mbele na hata nyuma kote niko mimi.
Najiona Mimi katika kuvuka wakati huu,Na msaada wa aliyeniumba naamini hata malaika wake wataendelea kusimama nami.

Najua nitavuka, Najua nitainuka,najua Kuna siku yanayonisumbua yatafutika,najua Kila lilolofungwa kwa uwezo wa Mungu na hakika litafunguka.
Nahitaji juhudi,nahitaji maombi, nahitaji uthubutu, nahitaji jipa muda ili nifike niendako na nipate nitakacho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom