Umejiandaaje kuwa Baba/mama mkwe

Umejiandaaje kuwa Baba/mama mkwe

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
5,632
Reaction score
8,311
Hili swali nakuuliza wewe ambae bado hujafika umri wa kuozesha binti/kijana wako, je umejiandaa kuwa Baba/mama mkwe wa aina gani

Je ni kitu gani sasa hivi unakifanya ila ukifikia hatua ya kuwa Baba/mama mkwe utakiacha? Kwanini karibu utupe mtazamo wako
 
Ni kweli nimeshuhudia marafiki zangu wakiachika kisa hao mama wakwe hasa! Ndio nataka kujua wasipojihusisha na maisha ya wanandoa hao wanapungukiwa nini?
Wewe utakuwa waaina gani, je nawewe utajihusisha na mahusiano ya binti/kijana wako au utakaa mbali hata kama hafanyi maamuzi sahihi katika uendeshaji wa treni yake ya mahusiano
 
Wewe utakuwa waaina gani, je nawewe utajihusisha na mahusiano ya binti/kijana wako au utakaa mbali hata kama hafanyi maamuzi sahihi katika uendeshaji wa treni yake ya mahusiano
Nitakaa mbali aisee kazi yangu ni kuwasaidia na kuwasapot watakapokwama, nitasuluhisha migogoro kwa hekima bila upendeleo, especially kama mtoto wa kiume ni wa kwangu nitajitahidi kutomkandamiza mkewe..
 
Tatizo wanatoaga taarifa za uongo kwa wazazi wao ukute kosa la kwake analimanupulate na kukujaza upepo na chuki kwa mkweo na uhisi maumivu anayoyapata au aliyotendewa hapo utafanyaje
 
Tatizo wanatoaga taarifa za uongo kwa wazazi wao ukute kosa la kwake analimanupulate na kukujaza upepo na chuki kwa mkweo na uhisi maumivu anayoyapata au aliyotendewa hapo utafanyaje
Kwa kawaida kama unapenda mahusiano yako ya ndoa yadumu mkeo akikosea msemee kwao na yeye akusemee kwenu! Ila ukitaka kuharibu kila kitu peleka makosa ya mkeo kwenu! Utajenga chuki kiasi kwamba ata siku mmeelewana bado kwenu watakuwa na kinyongo! Sasa kama huyo atapeleka taarifa za uongo kwao tayari hapo ni mgogoro wa kinafsia unaanza kujengwa! Ata siku umempiga kofi tu wanaibua na ya tangu zamani!
 
Back
Top Bottom