Umdhaniaye Ndiye Kumbe Siye....

Umdhaniaye Ndiye Kumbe Siye....

ludoking

Senior Member
Joined
Oct 5, 2008
Posts
124
Reaction score
71
Katika kusherehekea miaka 10 ya ndoa yao, Salma aliamua kumpeleka mumewe John kwenye 'strip' club mpya iliyofunguliwa miezi mitatu tu iliyopita.

Sababu kubwa iliyomfanya aamue kumpeleka mumewe kwenye club hiyo iliyojaa machangudoa, ni ushawishi wa marafiki zake wa kazini ambao (wote watatu) walifanya hivyo wakati wa kumbukumbu za ndoa zao.

Aidha, Salma alikuwa anat...aka na yeye apate la kusimulia kwani alikuwa amechoshwa na simulizi za rafiki zake kuhusu club hiyo.

Alipomwambia mumewe (John) offer hiyo, hakukubali ki urahisi. Alipinga sana kwenda club hiyo kwa madai kwamba ni sehemu ya kihuni isiyomfaa mtu mwenye familia kama yeye. Hata hivyo baada ya mkewe kumbembeleza sana hatimae akakubali.

Walifika Club kiasi cha saa nne hivi usiku. Wakati walipokuwa wakiingia, mlinzi wa mlangoni (baunsa) akamlaki John kwa shangwe sana. "Ohooo wee umekuja! karibu tena Mwanangu" Alisema baunsa huyo huku akimpiga piga John ngumi kifuani.

Kwa mshangao Salma akamuuliza mumewe "Vipi mnafahamiana?" Bila wasiwasi John akamwambia "Ooo yeah! tulikuwa wote Dojo pale Zanaki enzi ya Sensei Bomani".

Baada ya jibu hilo Salma hakuuliza swali lingine, kimya kimya wakaingia club na kukaa mezaya pembeni kabisa. Mara tu baada ya kukaa mhudumu wa kike akaja haraka na kuwakaribisha. "Sema John, Mambo? naona uko na totozi, nimletee kinywaji gani? maana najua wewe utakunywa ndovu ya baridi"

Bila kusita John akamjibu "Mletee mvinyo mwekundu (red wine)". Wakati mhudumu huyo akiondoka Salma akaja juu! "Niambie una uhusiano gani na huyu binti kiasi cha yeye kujua kinywaji unachokunywa kila siku?" Kwa upole John akamwambia "Huyu ni mke wa Abdallah, yule fundi aliyeweka vigae kwenye nyumba yetu ya mbezi. Kila nilipokuwa nikimpitia Abdallah ili twende saiti, alikuwa akimwambia mkewe anipe ndovumoja baridi kabla hatujaondoka".

Salma akashusha pumzi nzito ya kupata nafuu "Maskini Abdallah, kwa nini anamruhusu mkewe kufanya kazi sehemu kama hii?" John hakujibu??..

Dakika kumi baadae (wakati wakiendelea kunywa vinywaji vyao) 'striper' mmoja aliyevaa 'kufuli' tu! akaja mezani hapo na kumkalia John, kisha akaanza kucheza (kukata kiuno) huku akimwambia " John mpenzi siku hizi husomeki kabisa...imekuwaje
baby?" Kabla John hajajibu Salma akainuka kwa hasira na kumsukuma 'striper' huyo kwa nguvu, kisha akaanza kuondoka kuelekea mlangoni.

Haraka John akamkimbilia na kumshika mkono ili kumzuia.
Salma hakukubali, akamrushia kibao kikali kilicho mpata John Begani.

Kwa kutotaka kuanzisha vurugu John akawa mpole kuliko kawaida, akamvuta mkewe na kumkumbatia kwa nguvu huku akimnong'oneza sikioni "Salma mpenzi, usiwe na hasira, weweunadhani mimi naweza kutembea na 'striper' acha mbali changudoa wa kawaida! Yule msichana tulisoma wote..."

Kabla hajamaliza maelezo Salma akamsukuma na kukimbilia nje mahali zilipoegeshwa taksi. Akafungua mlango wa nyuma wa taksi iliyokuwa karibu na kujitupa kwenye siti huku akitweta kwa hasira.

John nae kwa haraka akafungua mlango wa upande wa pili na kukaa pembeni ya mkewe. "Nimekwambia sitaki... umeshanidhalilisha vya kutosha, niache niache! Salma aliongea kwa sauti ya juu huku akianza kulia. "Nisikilize kwanza baby mbona unakuwa na hasira hivyo?

John alijitahidi kuongea kwa kubembeleza ili mkewe ampe nafasi ya kutoa maelezo zaidi. Lakini kabla Salma hajasema lolote yule dereva taksi akadakia " John achana nae changudoa mbovu huyo; Ndiyo zake, huyo na hatosheki kwa siku bila kulala na wanaume zaidi ya 5 na wewe kila siku mimi huwa nakwambia usichukue machangudoa wa hapa wanajifanya bei mbaya sana hawa lakini hamna kitu, tatizo lako wewe unawaona mali"

Salma akapoteza fahamu.

#Ungekuwa wewe ungefanyaje?#
 
Hii stori imerudiwa lakini ikiwa na ukarabati fulani! i.e Siyo mpya.
 
Back
Top Bottom