Umaskini ni laana

Umaskini ni laana

jamaikatz

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2023
Posts
369
Reaction score
1,255
Habari wanaJF,

Siku zote UMASKINI haufurahishi, unatesa, unadhalilisha na unaumiza sana unamfanya mtu adharauliwe, achukiwe na wakati mwingine hata kutengwa maskini hana rafiki.

Na pia kutokana na hali ngumu ya maisha ya umaskini wetu kuna muda huwezi kuzuia machozi yasitoke kutokana na majaribu unayopitia ila jambo moja la muhimu ni kwamba machozi yasibabaishe kwenye hiyo safari yako ukaishia njiani, lia kisha uchungu ukiisha futa machozi, simama endelea na safari yako mpaka kieleweke.

Usije ukatishwa na maisha mazuri ya wengine mtandaoni, mtandaoni mtu ata kuonyesha kile anachotaka ukione ila hataki kuonyesha uhalisia wa maisha yake.

Na hatukupewa maisha mazuri au mabaya, Mungu alitupa maisha tu,ni chaguo letu kuyafanya yawe mazuri au mabaya.

Na pia nisisahau kuna walio andaliwa na wazazi wao maisha bora alafu kuna akina sisi tunao waandalia wazazi wetu maisha bora, hatufanani kikubwa kuheshimiana tu.

Tusichoke kupambana ili tuu tokomeze umaskini.
 
Umenena vyema,Mfalme Suleiman aliwahi mujomba mwenyeziMungu ampe Utajiri sio mkubwa sana,lakini pia asimpe umaskini asije akaiba akatenda dhambi,!Kataa umaskini kubali NDOA.
 
Back
Top Bottom