Umasikini wa watanganyika umesababishwa na CCM sio wazanzibar

tpmazembe

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
2,469
581
Umasikini mkubwa wa watanganyika , ambao wanamiliki rasilimali nyingi sana zisizohamishika kama mbuga za asili,milima na maziwa makuu barani afirka, pamoja na madini na mabwawa makubwa na mabonde maarufu umesababishwa kwa asilimia kubwa na UFISADI ndani ya ccm, viongozi wamekuwa wakitafuna rasilimali hizi kiasi cha kufikia kubeba twiga kwenye ndege, wamekuwa wakiuuwa mali asili na meli za viongozi wa ccm kukamatwa na meno ya tembo, wamkuwa wakiuza nchi kwa kuingia mikataba ya ovyo na kuhongwa mabilioni ya shilingi na kwenda kuyaficha nje.

Umasikini wetu watanganyika haujatokana na kulipa wabunge wa znz mishahara kwa vile majimbo yao madogo, wala haujatokana na kulipa wanajeshi na polisi ambao tunatumia sehemu zote nchini huku znz haichangii. znz tunaweza kuihudumia vizuri tu sisi kama watanganyika bila kuchukua chochote kwao na bado maendeleo pande zote yakawa mazuri.

Leo hii tunaagiza mafuta ,malawi wanachukulia bandari yetu lakini kwao bei nafuu kuliko sisi, uganda waagiza nguo kwa bandari yetu alafu kule nafuu kuliko kwetu na kujikuta wafanyabiashara wakienda uganda kununua nguo au malawi kununua mafuta.YOTE HII NI UKUBWA WA KODI TUNAYOTOZWA.huku pesa zote za rasilimali zikitaifishwa na wachache mbaya zaidi baada ya kuziweka katika mzunguko huchukua mabilioni hayo kwenda kuyaficha nchi za ulaya au sa na wengine hufa na pesa kupotelea huko.

Umasikini wetu wakutupa haijasababishwa na waznz bali UONGOZI MBOVU WA CCM.
 
Kweli kabisa. na ni vizuri tusichoke kuihidumia znz hata kama itakuwa na mamlaka kamili lakini ulizi na usalama uendelee kubaki wa pamoja maana ni ngumu kwa znz kuwa na stable government nje ya muungano. wote tunaona kila mara rais hushinda kwa chini ya 2% yaani mmoja ana 50% wa pili na 49%. mmoja anashinda kisiwa kimoja chote na na wawakili wote na na bado anakuwa hajashinda urais. hapo kuna hatari kubwa sana.
 
kama tanganyika itarudi. huu ufisadi utapungua sana maana itajulikana ni kiasi gani kinakusanywa.kwa sasa inakuwa ngumu. nadhani ndio maana mafisadi hawataki serikali tatu.
 
ni kweli kabisa kwamba UMASIKINI huu haukuletwa na zanzibar , lakini kuendelea kuihudumia zanzibar ni UTUMWA WA KUJITAKIA .
 
Umasikini mkubwa wa watanganyika , ambao wanamiliki rasilimali nyingi sana zisizohamishika kama mbuga za asili,milima na maziwa makuu barani afirka, pamoja na madini na mabwawa makubwa na mabonde maarufu umesababishwa kwa asilimia kubwa na UFISADI ndani ya ccm, viongozi wamekuwa wakitafuna rasilimali hizi kiasi cha kufikia kubeba twiga kwenye ndege, wamekuwa wakiuuwa mali asili na meli za viongozi wa ccm kukamatwa na meno ya tembo, wamkuwa wakiuza nchi kwa kuingia mikataba ya ovyo na kuhongwa mabilioni ya shilingi na kwenda kuyaficha nje.

Umasikini wetu watanganyika haujatokana na kulipa wabunge wa znz mishahara kwa vile majimbo yao madogo, wala haujatokana na kulipa wanajeshi na polisi ambao tunatumia sehemu zote nchini huku znz haichangii. znz tunaweza kuihudumia vizuri tu sisi kama watanganyika bila kuchukua chochote kwao na bado maendeleo pande zote yakawa mazuri.

Leo hii tunaagiza mafuta ,malawi wanachukulia bandari yetu lakini kwao bei nafuu kuliko sisi, uganda waagiza nguo kwa bandari yetu alafu kule nafuu kuliko kwetu na kujikuta wafanyabiashara wakienda uganda kununua nguo au malawi kununua mafuta.YOTE HII NI UKUBWA WA KODI TUNAYOTOZWA.huku pesa zote za rasilimali zikitaifishwa na wachache mbaya zaidi baada ya kuziweka katika mzunguko huchukua mabilioni hayo kwenda kuyaficha nchi za ulaya au sa na wengine hufa na pesa kupotelea huko.

Umasikini wetu wakutupa haijasababishwa na waznz bali UONGOZI MBOVU WA CCM.

Pamoja na hoja yako nzuri naomba unisaidie hapo kwenye red. Hivi Tanganyika inachangia kiasi gani katika muungano, hebu tupe takwimu taadhali kwa faida ya wanajamii.
 
Pamoja na hoja yako nzuri naomba unisaidie hapo kwenye red. Hivi Tanganyika inachangia kiasi gani katika muungano, hebu tupe takwimu taadhali kwa faida ya wanajamii.

wahasibu wanatuambia kuwa znz ilikuwa ikichangia kwenye muungano kwa miaka mitatu tu 1965,1966 na 1967. baada ya hapo znz haikuweza tena kuleta mchango kwenye serikali ya muungano.
 
Mleta mada ni mzembe anategemea misaada hata kununua mswaki tu hawezi
 
Pamoja na hoja yako nzuri naomba unisaidie hapo kwenye red. Hivi Tanganyika inachangia kiasi gani katika muungano, hebu tupe takwimu taadhali kwa faida ya wanajamii.

Tanganyika ipi hiyo inayochangia? au ni wahisani ndio wanaotoa pesa kusaidia Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
 
wahasibu wanatuambia kuwa znz ilikuwa ikichangia kwenye muungano kwa miaka mitatu tu 1965,1966 na 1967. baada ya hapo znz haikuweza tena kuleta mchango kwenye serikali ya muungano.

Inawezekana ikawa kweli walikuwa wanaleta chao miaka hiyo kwa vile walikuwa wakikusanya vyao wao wenyewe lakini inapofika kuwa TRA anakuja asubuhi Zanzibar na kuondoka na makusanyo ya kodi kwa boti ya saa 10 kurudi Tanganyika , unafikiri wachange kwa mapato gani?

Na hizi pesa zinazokusanywa zinakwenda wapi kama si kuijengea Tanganyika?
 
CCM KICHEFUCHEFU CHEFUA
Wakati kukiwa na harakati za kuondoa matatizo yanayoikabili Tanzania kipo chama kinachofikiria kukuza propaganda. Wakati ndani ya miaka hamsini ya muungano wa Tanganyika na Zanzibari, ambao una kila aina ya kero na sintofahamu, na wakati muarobaini ukitafutwa, wapo viongozi wa chama wanaendeleza sera za chuki, kashfa, matusi na dharau. Tukiwa ndani ya mijadala mizito juu ya mustakbali wa Tanzania tunayoitaka, Tanzania ya wananchi na sio viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, wapo wanaoneza propaganda kuwa katiba haitoleta maendeleo. Viongozi na makada wa CCM kila uchao wanaeneza propaganda za kuhadaa wananchi. CCM imekuwa na nguvu kuliko watendaji wa serikali na serikali yenyewe, na hiki ndicho kichefuchefu chefua.
Serikali ya CCM imeacha kutekeleza matakwa ya wananchi inatekeleza sera zake ingawa ni mbovu, chakavu, zenye kila aina ya uvundo. Serikali ya CCM inayojidai ni sikivu kwa wananchi inaburutwa na sera za chama, haitaki kusikiliza hoja na maoni ya wapinzani au wanaharakati. Wananchi tunahoji, mamlaka ya Kinana kukagua miradi ya serikali tena akiambatana na mkurugenzi anayelipwa mshahara na serikali ameyapata wapi?
Tunashangazwa na kujiuliza je, Kinana ana madaraka katika chama au serikali? Iweje mkurugenzi atoke ofisini kwa amri na utashi wa kiongozi wa chama, gharama hizi zinabebwa na nani?.
Zaidi ya hayo, mwanasheria mkuu wa serikali ana madaraka ya kutumikia chama au wananchi? Iweje kiongozi huyu mkubwa anayetambua sheria, wajibu na maadili ya uongozi autukane umma? Inakuwaje Spika akae kimya? Jawabu ni kuwa wanatekeleza sera za chama, sera kichefuchefu zaidi ya mtizamo wa matapishi machoni mwa waungwana.
Ingawa kuna nguvu kubwa inayotumiwa kuzima harakati na ukombozi wa wananchi, harakati hizi hazitokoma.
CCM itambue kuwa mabavu hayata dumaza akili za wananchi, wasidhani kuwa, wananchi wataendelea kuwa “mbwa kwa chatu” la abadani, kilio kimefika kwa wananchi kuitwa mahindi, hatutoendelea kulia, tutafuta machozi kwa kuidondosha CCM kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa na kuikataa katiba ya CCM.
Tunatoa wito kwa wananchi kukataa waziwazi mchana kweupe au usiku mbalamwezi kichefuchefu hiki, wanaharakati na wadau wote wanaoitakia mema Tanzania waendelee kuelimisha na kuhamasisha harakati hizi ziwe endelevu na hatimaye Tanzania iondokane na pingu ya kichefuchefu hiki. Hii ndio TANZANIA TUNAYOITAKA. Tanzania isiyokuwa na viongozi wenye dharau, kejeli, matusi na kashfa za ufisadi.
Kilio chetu nikuona bunge linakuwa chombo cha uwakilishi, watanzania tunahitaji kuona bunge linajadili wanyonge wanaoteseka, kupitia mchakato wa katiba mpya ambayo Kinana anadai eti haileti maendeleo kwa watanzania kuwa kinyume chake, wapinzani waoneshe udhaifu na kichefuchefu cha CCM na hatimaye waweze kuiokomboa Tanzania kutoka katika makucha ya simba CCM.
Tunahitaji bunge la kujadili matatizo ya walalahoi na kuhakikisha watumishi wanalipwa stahiki zao kwa wakati. Sote ni mashuhida kuwa serikali imeshindwa kulipa madai ya watumishi, hadi leo baadhi ya waliokuwa watumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hawajalipwa stahiki zao chini ya serikali ya CCM.
Mwisho wa siku tunataraji tuwe na utawala bora wenye kujali maslahi ya wote na hii ndio TANZANIA TUNAYOITAKA, TANZANIA ISIYOKUWA NA CHAMA KICHEFUCHEFU. HELO HELO TANZANIA HELO HELO AMANI NA UPENDO.
 
Back
Top Bottom