Umasikini unachangia ukahaba D'Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umasikini unachangia ukahaba D'Salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 21, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  UMASIKINI na kukata tamaa kwa baadhi ya wasichana wenye umri mdogo, vinachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la kasi la wasichana hao kujiingiza katika biashara ya ngono mkoani Dar es Salaam.

  Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi, umegundua kuwa wasichana wengi wanakabiliwa na umasikini unaowafanya kushindwa kujipatia mahitaji yao ya msingi.

  Baadhi ya wasichana wenye umri mdogo wamejiingiza katika biashara hiyo katika maeneo mbalimbali ya jijini la Dar es Salaam na kwa nyakati tofauti, wanasema wanalazimika kufanya hivyo, ili kupata fedha za kuwawezesha kujikimu.

  "Mimi sina wazazi, baba na mama wamefariki na tumekuwa tunalelewa na bibi naye hana uwezo. Nilikuwa nakaa Tabora na wazazi wangu hawakunipa msingi mzuri wa elimu, sasa
  nimekuja Dar es Salaam kutafuta.

  "Nilipata nauli ya kuja Dar es Salaam kutafuta kazi na nilipofika hapa, nilikutana na dada mmoja maeneo ya Ubungo ambaye aliniambia ana rafiki yake Magomeni anatafuta msaidizi wa ndani.

  "Nilikaa kwa yule dada, alikuwa ananitesa, hanipi chakula nikaamua kuondoka. Sikuwa na pa kulala na nilihangaika sana. Kule nyumbani sijui wadogo zangu wako vipi, sijafanikiwa bado," anasimulia msichana mmoja akiwa katika Baa ya Kimboka By Night Buguruni.

  Mwingine aliyekutwa katika Kituo cha mabasi Ubungo,alisema amekuwa akijiuza kwa baadhi ya madereva wa mabasi ili aweze kupata fedha japo si za kutosha kwani wakati mwingine baadhi ya madereva wanawadhulumu fedha zao licha ya kuwapa
  huduma.

  Akizungumzia hali hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kulea Wasichana wanaoishi katika Mazingira Magumu ya Kiwohede, Yustus Mwaituka, alisema njia ya kukabiliana na hali
  hiyo, ni kwa serikali kuzipa uwezo taasisi za kuwasaidia wasichana wa aina hiyo.

  "Unajua kama serikali itazijengea uwezo wa fedha ama kuzipa ruzuku taasisi kama yangu, wasichana watapata mafunzo, watakwenda shule na haya ya kujiuza hayatakuwepo au yatapungua.

  "Mtu anafiwa na wazazi au mlezi, anakosa uwezo wa kwenda shule atakuja huku na atapata kile anachokikosa huku atapata mafunzo, atakwenda shule na wapo tunaowabadilisha na wakaweza kujitegemea," anasema.

  Kiwohede ambayo iko katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Arusha, hupokea wastani wa wasichana 10 kwa siku lakini katika vituo vyake ina jumla ya wasichana wanaofikia 300 hadi 350.

  Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania, TAWLA, AnnMarie Nkalame alisema jamii inapaswa kuwazungukia na kuwapa elimu juu ya hicho wanachokifanya.

  Katika mahojiano, Nkalame aliyesikitikia hali hiyo, alisema biashara ya ngono haina tija na mwisho wa siku wasichana hao wanapata maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo HIV/AIDS na wanawake kupoteza utu wao.

  "Jamii iko karibu na wasichana hawa, kuna ndugu wa karibu wanaoweza kutoa taarifa za wasichana sasa hapa ni jamii na si suala la taasisi, tuanze kujipanga wenyewe kabla ya kufika mbali," alisema.

  Akizungumzia hali hiyo, mmoja wa waelimisharika kutoka taasisi ya Triace, Albert Mwale anasema kuna haja ya serikali kuwajengea uwezo wasichana ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za kijamii vijijini waweze kujitegemea.Chanzo Umasikini unachangia ukahaba D'Salaam

  Ni kweli umasikini unachangia sana mambo ya ukahaba hapo kwetu Dar.
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ukimuuliza mhe. JK nini kinasababisha ukahaba dar es salaam yeye atakwambia ni viherehere vyao ndo vinasababisha haelewi kabisa tatizo la umasikini linavyoleta changamoto za mimba kwa wanafunzi na pia kongeza maambukizi ya ukimwi kwa shughuli za ukahaba.
   
Loading...