Umafia CCM ya JK; Lowassa, Rostam na Chenge njia panda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umafia CCM ya JK; Lowassa, Rostam na Chenge njia panda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 14, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  na Waandishi wetu, Dodoma  VIKAO vikuu viwili vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kile cha Kamati Kuu na cha Halmashauri Kuu ya Taifa vilivyomalizika mjini Dodoma juzi nyuma ya kivuli cha dhana ya chama hicho kujivua gamba viliendeshwa kwa staili ya kijajusi na Kimafia, Tanzania Daima Jumatano limethibitisha.
  Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa gazeti hili kwa siku kadhaa kabla ya kuanza kwa vikao hivyo, wakati vikifanyika na hata baada ya kumalizika umethibitisha pasipo shaka kwamba Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, aliviandaa na akaviendesha vikao hivyo katika misingi ya asili ya namna vinavyoendeshwa vyama vya kisoshalisti duniani.
  Kwa mujibu wa uchunguzi huo ambao ulifanywa na gazeti hili kwanza kwa kuzungumza na baadhi ya waliokuwa wajumbe wa sekretarieti na wale wa Kamati Kuu (CC) zilizovunjwa unaonyesha kwamba hata ile hoja ya kutaka vikao hivyo vivunjwe iliandaliwa mapema na mbinu mbalimbali zikabuniwa ili kufikia malengo yaliyotarajiwa.
  Kauli aliyoitoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yussufu Makamba, wakati akiwaaga wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambao amewaongoza tangu mwaka 2006 kwamba alikataa pendekezo la kumtaka ajiuzulu peke yake ili kupisha uteuzi wa mtu atakayerithi mikoba yake ni ushahidi wa kwanza wa namna mkakati huo ulivyoandaliwa mapema.
  Mmoja wa wajumbe wa iliyokuwa Kamati Kuu (CC) iliyovunjwa alilieleza gazeti hili wiki mbili kabla ya kuanza kwa vikao hivyo kwamba alikuwa akikusudia kwenda Dodoma na kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya ujumbe kama njia ya kumsaidia Rais Kikwete kuunda upya timu yake.
  “Nakwenda Dodoma nikiwa na wazo moja tu la kujiuzulu ujumbe wa Kamati Kuu kwa kuwa naamini katika kipindi chote nilichokuwa mjumbe mimi pamoja na wenzangu tumeshindwa kumshauri ipasavyo mwenyekiti wetu Rais Kikwete,” alisema mjumbe huyo kwa kujiamini.
  Mwandishi wa gazeti hili alipomueleza mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM kwamba uamuzi wake wa yeye binafsi kujiuzulu unaweza ukapingwa na wajumbe wenzake, alisema atakapofikia kuchukua uamuzi huo, basi atawaomba wajumbe wenzake kufanya hivyo hivyo ikiwa ni pamoja na kumshauri mwenyekiti wa taifa Rais Kikwete kuridhia uamuzi wa kuzivunja Kamati Kuu na sekretarieti ya chama hicho.
  Mawazo hayo ya mjumbe huyo wa zamani wa kamati kuu ndiyo ambayo yaliakisiwa barabara na matukio yaliyotokea ndani ya kikao hicho ambacho mjadala wake ulichukua siku mbili badala ya siku moja iliyopangwa kutokana na kuibuka kwa mivutano mikali ya hoja.
  Habari kutoka ndani ya Kamati Kuu zinaeleza kwamba baada ya hoja ya namna kujivua gamba kuibua mivutano mikali, alikuwa ni Abdulrahman Kinana mmoja wa wanasiasa wanaoheshimika ndani ya CCM aliyesimama na kutoa pendekezo la kutaka wajumbe wa Kamati Kuu na wale wa Sekretarieti kujiuzulu wote kama njia ya kumsaidia mwenyekiti wao kuunda upya uongozi mpya.
  Dalili za wazi zinaonyesha kwamba, hoja hiyo ya Kinana ama ilikuwa na baraka zote za Kikwete au iliungwa mkono naye moja kwa moja hasa baada ya yeye kuwa miongoni mwa wajumbe wachache wa kamati kuu iliyopita kupendekezwa tena na kurejea kwa kishindo katika kikao hicho baada ya kujiuzulu.
  Uchunguzi zaidi wa Tanzania Daima Jumatano umebaini pia kwamba ripoti ya uchunguzi kuhusu afya ya CCM iliyofanywa na kamati timu maalum ya wanazuoni walioongozwa na Dk. Mihanjo na kuwasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu ambayo pamoja na mambo mengine ilipendekeza kuchukuliwa kwa hatua za haraka za kukisafisha chama dhidi ya tuhuma za kukithiri kwa vitendo vya rushwa na kwa kuwakumbatia watuhumiwa mbalimbali wa ufisadi ni moja ya mambo ambayo ndiyo yaliyozaa wazo la CCM kujivua gamba.
  Kwa mara ya kwanza dhana hii ya kujivua gamba, ilitangazwa hadharani na Rais Kikwete mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM, Februri 5, 2011 ambapo aliwataka viongozi wa chama hicho kujiandaa kwa ajili ya mabadiliko makubwa.
  Mwelekeo huo wa mambo ndiyo ambao umewafanya baadhi ya wadadisi wa siasa za ndani ya CCM walio ndani ya vikao vya CC na NEC ya chama hicho kuziona hatua hizo za Kikwete kutangaza kujivua gamba kuwa zilikuwa zikilenga kuwaweka kando baadhi ya wanasiasa wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali ndani ya chama hicho.
  Kiongozi mmoja wa siku nyingi za CCM aliyezungumza na Tanzania Daima Jumatano anasema, hoja ya Kinana ya kutaka Kamati Kuu na Sekretarieti nzima kujiuzulu kwa kiwango kikubwa ililenga kuwatema makada wa aina ya Rostam Aziz, Andrew Chenge ndani ya vikao hivyo vyenye nguvu kwa njia ambayo ingemuepusha Rais Kikwete katika lawama za moja kwa moja.
  Kwa mujibu wa kiongozi huyo, hatua hiyo pia ilikuwa ikilenga kutekeleza moja ya maamuzi yaliyokuwa yakionekana kuwa ni magumu kuchukuliwa na Kikwete mwenyewe kabla ya mwaka 2012 ya kumuondoa katika nyadhifa ya Katibu Mkuu, Yussufu Makamba ambaye alishatangaza mapema kwamba alikuwa akikusudia kuondoka rasmi kwa kustaafu mwakani, wakati utakapofanyika Uchaguzi Mkuu wa ndani ya chama hicho.
  Mwingine anayeonekana kuwa alilengwa kuondolewa katika Kamati Kuu nap engine sekretarieti ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye alikuwa Mkuu wa Idara ya Siasa na Mahusiano ya Kimataifa katika uongozi uliojiuzulu.
  Kuwekwa kando kwa Membe, mtu anayetajwa kuwa karibu kifikra na kimaamuzi na Rais Kikwete katika wadhifa huo wa kichama, umeibua maneno mengi ya chini chini kuhusu sababu hasa ya kukosekana kwake katika nafasi hiyo.
  “Haikuwa rahisi kwa Kikwete mwenyewe kuitikia wito uliokuwa ukielekezwa kwake muda mrefu wa kumtoa Makamba katika nafasi yake kabla ya mwaka ujao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wanasiasa wa aina ya Rostam na Chenge. Kwa sababu hiyo mkakati wenye sura ya kistaarabu uliandaliwa ili kuwajengea mazingira ya kutoka,” alisema kada huyo wa CCM wa siku nyingi.
  Habari zaidi kutoka ndani ya vikao hivyo zinaeleza kuwa, mkakati wenye mwelekeo huo huo ulipangwa kufanywa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) safari hii walengwa wakiwa watu wa aina ile ile ambao baadhi yao wana nguvu kubwa.
  Hoja iliyojengwa na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya ndani ya NEC ya akisema iwapo dhana ya kujivua gamba ndani ya chama hicho ilisababisha wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti kujiuzulu nafasi zao, basi kulikuwa na haja kwa wana CCM wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi ambao ni wajumbe wa NEC kupima wenyewe uzito na ikibidi wajiuzulu inatafsiriwa kuwa na mwelekeo huo huo.
  Hoja hiyo ya Mwandosya ambayo iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ilibeba uzito zaidi hasa pale alipomtaka Rais Kikwete kuhakikisha majina ya watuhumiwa wa ufisadi, Chenge na Rostam kutoyarudisha ili yapigiwe kura ya kuwa tena wajumbe wa Kamati Kuu.
  Hatua ya Rais Kikwete kutoyajumuisha majina hayo katika mapendekezo yake ya wajumbe wa Kamati Kuu ilithibitisha mwelekeo wa kimawazo wa mwenyekiti huyo na maana halisi ya ajenda yake nzima ya kutaka chama hicho kujivua gamba.
  Inaelezwa kuwa, mwelekeo huo wa hoja ya Makongoro, uliwakumbusha wajumbe wa NEC waliokuwa katika kikao cha Kamati Kuu kauli aliyoitoa Kikwete siku moja tu ya kuwataka wajumbe kujadili kwa mapana na marefu tatizo la ufisadi wakizungumza kwa uwazi na ukweli kabla ya kutoka nje ya kikao hicho na kumlaumu yeye kwa kile ambacho wamekuwa wakidai kuwalinda marafiki zake.
  “Tukiwa katika CC, ilipofika hatua ya kulijadili tatizo la ufisadi ndani ya chama, mwenyekiti (Kikwete) alitueleza bayana kwamba tulijadili kwa uwazi suala hili ili tusije tena tukatoka nje ya kikao na kuanza kumtuhumu kwamba yeye analinda marafiki zake,” alisema mtoa habari mmoja aliyezungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.
  Mjumbe mwingine wa NEC alilieleza gazeti hili kwamba, dhamira na mwelekeo wa kikao hicho kutaka kuwakabili baadhi ya watuhumiwa wakubwa wa ufisadi iliibua wasiwasi baada ya watu walio karibu na Rostam na Lowassa kuanza kupenyeza taarifa kwamba hoja hiyo haiwezi kuwaacha wana CCM wengi zaidi salama.
  Kwa mujibu wa mjumbe huyo, hoja iliyosababisha kauli za Mwandosya na ile ya Makongoro kukosa mashiko ilitokana na hoja ambayo ilishatolewa awali na mjumbe mwingine awali katika CC ambaye alikumbusha orodha ya kwanza ya watuhumiwa wa ufisadi iliyosomwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam, Novemba 15 mwaka 2007.
  Miongoni mwa viongozi ambao Dk. Slaa aliwataja kwamba ni watuhumiwa wa katika orodha yake maarufu ‘The List of Shame’ ambao ama ni wajumbe wa Kamati Kuu na wengine Halmashauri Kuu ni Nimrod Mkono, Lowassa, Rostam, Rais Kikwete mwenyewe, Chenge na Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
  Kada mmoja wa CCM ambaye yuko karibu na baadhi ya wana CCM wenye tuhuma za ukosefu wa maadili anasema hatua ya Mkuu wa Idara ya Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye kutangaza mbele ya waandishi wa habari kwamba, NEC katika maazimio yake imewapa watuhumiwa wa ufisadi muda wa miezi mitatu kupima wenyewe na kujiuzulu kabla ya kupokonywa nafasi za uongozi inaweza ikazusha kelele kubwa.
  “Kwanza kauli hiyo ya Nape imetushtua sana, haikuwa sehemu ya maamuzi ya NEC tuliyoyapitisha jana na juzi. Tunasubiri hiyo miezi mitatu ifike tuwasikie hao watuhumiwa wa ufisadi wakiwajibishwa kwa nguvu kwani miongoni mwa watuhumiwa hao wako hata viongozi wetu wa juu. Nadhani wakati wanapoyasema hayo wanakumbuka kwamba hata jina la Rais Kikwete limekuwa likitajwa.
  “Hivi wanasahau kwamba Rais Kikwete, Rais mstaafu Mkapa walitajwa katika orodha ya Mwembeyanga ya Dk. Slaa? Nao wanatakiwa kujiuzulu baada ya miezi mitatu? Watu hawa wanasahau kwamba jina la Kikwete kabla hajawa rais limewahi kutajwa hata katika sakata la IPTL na akatumia muda mrefu kujisafisha wakati akisaka urais mwaka 2005?” alihoji kada huyo wa CCM.
  Baadhi ya wajumbe wa NEC waliozungumza na Tanzania Daima Jumatano wanasema ingawa wanakubaliana kimsingi na hatua ambazo chama chao kinatakiwa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi, wanashangazwa na hatua ya Nape kutangaza azimio ambalo si sehemu ya mambo yaliyojadiliwa na kukubalika ama kwa kura au kwa kauli moja na wajumbe wote.
  Mjumbe mwingine wa NEC alilieleza gazeti hili kwamba katika siku za hivi karibuni na hususan hata wakati John Chiligati akiwa Mkuu wa Idara ya Uenezi na Itikadi, kumekuwa na malalamiko kadhaa kwamba kile kinachotajwa kuwa sehemu ya maazimio ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu kuwa tofauti na kile kilichojadiliwa ndani ya vikao hivyo. Akitoa mifano mjumbe huyo anasema, Chiligati alipata kulalamikiwa kwa kutoa taarifa potofu kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu kuhusu uamuzi wa ama kulipa au kutokuilipa fidia kampuni ya uzalishaji umeme ya Dowans ambayo inaidai Tanzania karibu shilingi bilioni 100. Chiligati anatajwa pia kupata kutoa maazimio ya kupotosha wakati aliposoma maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu utata ulioibuka baada ya kukatwa kwa jina la Hussein Bashe katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM kwa jimbo la Nzega katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
   
 2. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,699
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  picha la kidosi ndio limeshaanza halafu ni refu mno yaani tutaliangalia kwa cku 90 cjui stearing atakufa au atapona!
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ndio kusema hiyo kauli ya Nape ilikuwa danganya toto au"the impossible mission"? Iwapo maamuzi ya vikao sio yanayotangazwa basi hicho chama kimeoza kuliko tulivyofikiri. Uchakachuaji wa humo kwa humo. duh
   
 4. M

  MVUA GAMBA Senior Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Magamba mengine unaweza yavua leo kesho yanaota na kukomaa vile vile na mengine hayavuliki na hii ni kwa uzoefu wangu kama mvua magamba
   
 5. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  tandandaaaaa.....picha ndio linaanza.....

  Napata picha baada ya miezi mi-3 wakina EL hawatoki kwenye chama, then wanapata msukumo kwa wananchi kutekeleza ahadi yao, mara msukumo unawafanya kuwavua uanachama...

  Movie inaendelea timu ya El na RA wanaamua kumchomea JK na kutoa majibu mengi ya maswali tata ambayo mengi yanahisiwa kuwa tata kwa kuwa yanamgusa mkulu;;-- Mara unasikia au unaona document zinazagaa JF


  1. Kikwete alihusika kwa namna hii ndani ya Dowans/Richmond
  2. Huu ndio ukweli wa Balali na JK
  3. Hivi ndivyo JK alivyowaibia watanzania kura 2010 uchaguzi mkuu
  4. Hivi ndivyoooooooooooooooooooooo...hivi ndivyoo......

  Sitafumba macho yangu after these three months kuona mwisho wa ngoma hii nijue nani Sterling nani Jambazi
   
 6. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  MKUU,
  Nimependa post yako, yote uliyosema naongezea KUBASHIRI yatatimia. Kuna mvurugano mkubwa wa kuumbuana mbeleni, JAPO MENGI WALIANDIKISHIANA KUTOPAKAZIANA MAJUKWAANI.
   
 7. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Mbona mwandishi kama vile anajaribu kukatisha tamaa kwa weledi mkuu. Nikiangalia uandishi wake ni kama anayetoa tahadhari kwa JK kutowagusa akina RA, EL na Chenge kwa hoja kwamba hata yeye ni mtuhumiwa. Sioni tofauti ya habari hii na ile ya Mtanzania. Slowly naamini sasa kwamba mhariri wa Tanzania Daima ameshatekwa!
   
 8. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katika mikutano yote ya CCM maazimio ya vikao hayafikiwi kwa kupigiwa kura, isipokuwa sekretariati uandaa orodha ya mambo inayotaka yajumuishwe kwenye orodha ya maazimio ya kikao husika, baada ya orodha hiyo kupata muafaka wa mwenyekiti, wajumbe husomewa tu kuwa hayo ndiyo maazimio ya kikao. Katika hali hiyo, hta safari hii hakuna jambo lolote lililokwenda kinyume na mfumo uliozoeleka. Kwangu mimi naona kuna kasoro za aina mbili katika mchakato huo. Kwanza ni suala zima la kuwatia hatiani wakina E.L; R.A; E.C bila ya kuwapa kwanza fursa ya kujitetea, kinyume na kifungu cha 13(6)(a) cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kasoro hii inatoa mwanya kwa watuhumiwa hao kufutilia mbali hatua zozote zitakazokuwa zimechukuliwa dhidi yao. Kasoro ya pili ni utaratibu mzima namna mjadala huo ulivyoendeshwa. Baada ya majina ya watuhumiwa hao kutajwa wazi wazi kwenye kikao cha C.C ilitakiwa watu hao watolewe nje ya kikao ili wapate kujadiliwa. Kitendo cha kuwajadili wakiwepo kwa maoni yangu kililenga katika kuumaliza nguvu njadala huo.
   
 9. A

  Aman Member

  #9
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo habari hapo inaonyesha jinsi gani the top three fisadiz EL,RA,AC wanavyotafuta draw ili mambo yaishie juu juu!.
   
 10. J

  Joblube JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Siku nyingi wewe uasituka leo
   
 11. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  La kuvunda.....
   
 12. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hapo hata mimi nimestuka sana kama kweli alichoongea sicho walichoamua, basi kuna tatizo tena kubwa sana ndani ya hiki chama!!
   
Loading...