Kunashida sanaa mm nilipima nikaambiwa na hydronephrosis nikaenda hospital nyingine wakasema sinaaNapenda kujua ni kwa nini kuna utofauti wa taarifa ya majibu ya vipimo vya ultrasound kati ya hospital moja na nyingine kwa mgonjwa yuleyule hasa wajawazito! Je ni hali ya kibahatisha tu, au ni utofauti wa ujuzi wa watalam ama!!
Tumbi Hosp walimwambia wife ana mapacha tumboni, MNH wakasema ni mmoja! Hatimae akajifungua mtoto mmoja!
Napenda kujua ni kwa nini kuna utofauti wa taarifa ya majibu ya vipimo vya ultrasound kati ya hospital moja na nyingine kwa mgonjwa yuleyule hasa wajawazito! Je ni hali ya kibahatisha tu, au ni utofauti wa ujuzi wa watalam ama!!
Sio kila infiltration ni TBNitaendelea kuiamini USS zaidi ya chochote ukikuta kasoro jua skills ya mpimaji tu hakutulia mfano:maabara wanaweza Pima makohozi wakasema negative lakini mgonjwa huyo akija idara ya radiology tukapma chest XR tutakuta infiltration features za kutosha ambazo ni indication za Tb kama kawa
Maelezo yako yako sahihi pia kwa kiasi fulani.Tatizo wanao order kipimo cha ultrasond wengi hawajui. Unakuta mtu ana andika history. Had. Osophagus CA alafu provisional dx anakuandikia Abn uss. Unategemea uletewe nn hapo. Mtaendelea kuandika form nyingine afanye mtu mwingine ila utajikuta unatafta tatizo ambalo hata ww hujui kulichunguza.
Mwingine anaandika Abn uss alafu hakuambii kwenye abn uangalie nn. Ni kama unamwambia mtu nenda sokoni,sokon kununua nn. Unaposema nenda uss lazima uandike aangalie nn liver,kidney au spleen kwa Abn.
Jifunzeni kuomba vipimo vya uss. Sikatai it depend with concentration ,skill of opperator
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi wako mzuriDisadvantage kubwa ya kipimo cha ultra sound ni kwamba inategemea sana kiwango cha umakini, uzoefu na elimu ya huyo anaekufanyia hiyo ultra sound. Wataalamu wenyewe wanasema kuwa kipimo hiki ni very subjective, kwamba inategemea na uwezo wa ung'amuzi wa huyo mfanyaji hicho kipimo.
Hivyo basi, si ajabu kabisa kuwa na majibu mawili tofauti endapo utafanyiwa kipimo hiki na wapimaji wawili tofauti.
Lakini pia, kuna vitu vingine ambavyo vinaweza kuathiri na kusababisha majibu ya ultra sound kutofautiana. Mfano, teknolojia ya mashine ya ultra sound iliyotumika; kwa sababu pia hizi mashine ziko matoleo mbali mbali yenye ubora tofauti tofauti kama vile zilivyo kamera (e.g. ukipimwa hospitali A, na mashine ya ultra sound ambayo inatumia teknolojia ya 2D, kisha ukapimwa hosiptali B ambayo ina ultra sound inayotumia teknolojia ya 3D, uwezekano wa kuwa na majibu tofauti ni mkubwa tuu. Pia, kwa mfano ulipopimwa hospitali A ulikuwa umebanwa na mkojo, ila ulipoenda hosp B ulikuwa umeshakojoa tayari, inaweza pia kusababisha utofauti wa majibu (japo si kwa kiwango kikubwa).
Nilipokuwa nafanya medical practice hospitali moja ya rufaa ya kanda nchini, ilikuwa kama mnapita raundi wodini, mkiwa mnasoma majibu ya ultra saundi ya mgonjwa, kitu cha kwanza mnaangalia ni nani aliefanya hiyo ultra saundi? Kuna baadhi ya majina ilikuwa ukiyaona tuu kwenye karatasi ya ultra saundi, hata hujIhangaishi kuisoma hiyo ripoti, maana unajua its useless, cha kufanya unaandika upya request ya ultra saundi, ili kipimo kirudiwe, na kuandika kabisa kwenye ile fomu kuwa ultra saundi hii aifanye "fulani".
GeeM
Tumbi Hosp walimwambia wife ana mapacha tumboni, MNH wakasema ni mmoja! Hatimae akajifungua mtoto mmoja!