Ulokole na utajiri

doppla2

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
1,313
2,000
Salaam wakuu

Walokole wenzangu, Bwana asifiwe na hongeleni kwa ibada za kukanyaga mafuta, kupanda na kuvuna na ibada za kufunguliwa kutoka kwenye vifungo mbali mbali.

Kuna kitu leo ntaomba tusemezane kwa roho safi kabisa.

Ni desturi na mazoea kila mwisho wa mwaka kunakua na pilika mbalimbali za mafundisho, semina na makongamano ya kuhitimisha mwaka.

Mnakumbuka mwezi kama huu mwaka jana tulipewa utabiri wa kila namna kuwa mwaka huu 2017 lazima tutoboe kiuchumi. Tuliaminishwa na kutabiriwa spesfically kabisa na wenzetu walipakwa mafuta na kunyweshwa.

Ila kwa utafiti wangu toka Octoba nimekuwa curious kutaka kujua maoni ya wapendwa wenzangu juu ya hili. Je ni kweli tabiri zile zimezaa matunda?

Kwetu kanisani na hata baadhi ya sehemu nazopendaga kuabudu hali ya Wakristo wengi wako choka mbaya, biashara nyingi zimegoma na deal nyingi zimeyeyuka sana mwaka huu. Wale waliohaidiwa kuolewa hadi leo tumebakiza siku chache mwaka uishe bado ni bila bila....

Naomba nijilizishe toka kwako Mpendwa hivi mautabiri yale yote yalikuwa mbwembwe tu?

Je kweli kwa kadiri tulivyo panda tumevuna?


Naanza kupata mashaka, juhudi zetu za kupanda zinawanufaisha wachache sana huku kundi kubwa tukiishi kwa kujifariji tu!!!

Baba wachungaji karibuni pia mtuambie Mmebarikiwa kwa kiwango gani Kwa kupanda kwenu na sio kwa kupewa na kutumikiwa.

Isije kuwa nyie nanyi ni kama mganga asiyejiganga.... Mnatajirisha wengi ila katu nyie hamuwezi pia kutumia njia na kanuni hizo mkafanikiwa.


Karibuni wapendwa
 

Mushi92

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
3,909
2,000
Hebu wale walioenda kwenye inshu kama hizo wake walalamike.
Ila kama huhusiki kaa kimya.
Haya mambo yanaendana na kazi....na imani (kutiwa moyo).
Pamoja na moyo Wa kushukuru
 

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,600
2,000
Yesu hakufa msalabani kwa aibu ili watu wamiliki majumba na magari hapa duniani.
Injili yoyote ile itakayohubiriwa hapa duniani au popote pale kama haimwongozi mtu kuacha dhambi na kumfundisha pamoja na kumwombea muamini ajazwe Roho mtakatifu na badala yake kutia kelele kwenye maspika kuwa mara ooohh utainuliwa!, utatajirika!, utajenga! n.k hiyo ni Injili ya kishetani na muhubiri jehanamu inamngoja
Kuna wahubiri wa kishetani wanaotumiwa na shetani kwa namna mbili;
1.Kwa kujua
2.Kwa kutokujua.
Ukikaa vizuri na Mungu kila kitu kitakuja automatically, hapa simaanishi kuwa ni lazima uwe tajiri.
Hekima ya Kimungu inapokaa ndani yako akili yako inafunguka na kukuonesha fursa ambazo si rahisi mtu mwingine kuziona,na pindi unapotia mkono kufanya Mungu hubariki ile kazi yako.
 

doppla2

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
1,313
2,000
Yesu hakufa ili watu wamiliki majumba na magari.
Injili yoyote ile itakayohubiriwa hapa duniani au popote pale kama haimwongozi mtu kuacha dhambi na kumfundisha pamoja na kumwombea muamini ajazwe Roho mtakatifu na badala yake kutia kelele kwenye maspika kuwa mara ooohh utainuliwa!, utatajirika!, utajenga! n.k hiyo ni Injili ya kishetani na muhubiri jehanamu inamngoja
Kuna wahubiri wa kishetani wanaotumiwa na shetani kwa namna mbili;
1.Kwa kujua
2.Kwa kutokujua.
Ukikaa vizuri na Mungu kila kitu kitakuja automatically, hapa simaanishi kuwa ni lazima uwe tajiri.
Umeandika vyema
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,559
2,000
Siri ya utajiri inapatikana kwenye Kumbukumbu la Rotation sura ya 28
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom