Wanyonge ndiyo wanaviherehele sana,acha walipe Tena ipandishwe iwe elfu sabini.Hii kodi achana nayo kabisa. Ilileta usumbufu mwingi sana kwa Watanzania Wanyonge enzi hizo, pamoja na ile kodi ya baiskeli!
Elfu 10 tu kwa mwaka mbona kidogo, lipeni bana, lipa Kodi Jenga nchi. Mi5 tena.
hata machinga wa kariakoo na wa Kigoma vijijini wote kitambulisho cha machinga wanalipia elfu 20😂 hakuna usawa duniani, lipeni kodiiiiii.Utalipaje 10,000 sawa na mtu wa masaki ambaye yeye nyumba yake anapangisha kwa mil 2, mimi kijijini hakuna hata wa kupanga labda mwalimu ambapo kwa mwezi haizidi 20,000.
Kabisa maana sasa ni kero kwa kweli. Kiwanja kilipiwe kodi, nyumba yenyewe ilipiwe kodi duuuhIfike mahali kodi ya kichwa irudi tu tujue moja.
Nyumba nyingi za vijijini pamoja na kuwa duni zimejengwa kwenye maeneo ambayo hayajapimwa ambayo ni maeneo yanayomilikiwa na ukoo au familia kama mashamba, hivyo hayana hati. Sasa hiyo kodi inayotozwa kwenye nyumba ya nyasi ambayo hata valuation yake haijulikani inakuwaje. Kama walivyochangia wadau huko juu ni kama kodi ya kichwa inarudi kwa utaratibu mwingine, maana hii ilikuwa haijali unaishi mjini au kijijini, maskini au siyo maskini, una kazi ya kukuingizia kipato au huna. Ila wakifanikiwa kuirudisha hiyo kodi ya kichwa, wasisahau kuondoa VAT kwenye bidhaa tunazonunua maana sasa tunarudi kwenye uchumi wa kijima tena......tumlazimishe!