Ulisikia wapi vijijini wanalipia kodi ya majengo?

Ulisikia wapi vijijini wanalipia kodi ya majengo?

Usijifanye una Akili kuliko Serikali kwanza Huna jengo wewe Utaratibu uliopo ndio Sahihi usimkosoe Rais Wetu Aliyeuweka
 
Utalipaje 10,000 sawa na mtu wa masaki ambaye yeye nyumba yake anapangisha kwa mil 2, mimi kijijini hakuna hata wa kupanga labda mwalimu ambapo kwa mwezi haizidi 20,000.
Elfu 10 tu kwa mwaka mbona kidogo, lipeni bana, lipa Kodi Jenga nchi. Mi5 tena.
 
Utalipaje 10,000 sawa na mtu wa masaki ambaye yeye nyumba yake anapangisha kwa mil 2, mimi kijijini hakuna hata wa kupanga labda mwalimu ambapo kwa mwezi haizidi 20,000.
hata machinga wa kariakoo na wa Kigoma vijijini wote kitambulisho cha machinga wanalipia elfu 20😂 hakuna usawa duniani, lipeni kodiiiiii.
 
Taarifa zinadokeza kwamba mpango wa kurejesha kodi ya kichwa uko mbioni kukamilika
 
Huko vijijini, wakati mnakula fedha za wajumbe hili hamkuliona? Lipeni kodi na mtaisoma namba
 
Ipo siku makaburi yalipo mjini yata takiwa kulipiwa kodi
 
Attachments

  • 2393313_IMG_20200501_071909.jpg
    2393313_IMG_20200501_071909.jpg
    15.5 KB · Views: 7
Hiyo ndio dalili ya serikali iliyoshindwa, hukimbilia kukusanya kodi mpaka kwa maskini
 
Mambo tafuatayo vijijini hawalipii

1. Maji
2. Kodi za majengo
3. Kodi za ardhi
Kabisa maana sasa ni kero kwa kweli. Kiwanja kilipiwe kodi, nyumba yenyewe ilipiwe kodi duuuh
 
Nyumba nyingi za vijijini pamoja na kuwa duni zimejengwa kwenye maeneo ambayo hayajapimwa ambayo ni maeneo yanayomilikiwa na ukoo au familia kama mashamba, hivyo hayana hati. Sasa hiyo kodi inayotozwa kwenye nyumba ya nyasi ambayo hata valuation yake haijulikani inakuwaje. Kama walivyochangia wadau huko juu ni kama kodi ya kichwa inarudi kwa utaratibu mwingine, maana hii ilikuwa haijali unaishi mjini au kijijini, maskini au siyo maskini, una kazi ya kukuingizia kipato au huna. Ila wakifanikiwa kuirudisha hiyo kodi ya kichwa, wasisahau kuondoa VAT kwenye bidhaa tunazonunua maana sasa tunarudi kwenye uchumi wa kijima tena......tumlazimishe!
 
Kweli kabisa, wakati wa kodi ya kichwa kulikua hakuna VAT.

Nyumba za udongo pekee ndio hazitalipiwa Kodi iwepo mjini au kijijini....

Hiyo inaitwa Kodi ya jengo hii haina tofauti na Kodi ya kichwa... Maana mmiliki wa jengo ndio kichwa...
 
Back
Top Bottom