Ulisikia wapi vijijini wanalipia kodi ya majengo?

Ulisikia wapi vijijini wanalipia kodi ya majengo?

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,262
Reaction score
18,706
Serikali lazima iweke uwazi, kodi za majengo zinatakiwa zilipwe kulingana na thamani ya jengo husika na thamani ya majengo huongozwa na hadhi ya sehemu husika.

Mfano jengo la Kariakoo haliwezi kuwa sawa na jengo lilipo kijiji cha Nyanshozi.

Kwa miaka yote kodi za majengo ziliishia kwenye halmashauri za wilaya na miji.

Sijawahi kusikia kodi za majengo kwa halmashauri za vijiji.

Jafo anatakiwa kujua , tangazo lako litaishia kumchafua mh Rais.

Tunaomba bunge liingilie kati,

Mwananchi wa kijijini amejipiga kanunua bati 5 kajenga nyumba yake ya tofali za kuchoma leo mnamtaka alipie 10,000.

Hizo kodi chukueni huko mijini, vijijini tuacheni kabisa na hatuta lipa labda mtufunge.
 
Washafika na huko..?!
Halafu korosho na mazao mengine soko wameua, hiyo pesa ya kulipia majengo inatoka wapi?

LITAKE LISITAKE milele daima.. si ndio bandugu...
 
Boss ni kweli kuwa kijijini kodi ya jengo haikuwepo enzi za Mkapa na Kikwete ,ila Magu alivyokuja walianza kuyatambua sema wakusanyaji tu walikuwa hawafiki.

Nachojua ni kwamba kijiji hakuna kodi ya ardhi kwa sababu kule ardhi ni kwa ajili ya kilimo na ufugaji.
 
Mbona wenzenu tunalipa? Nyinyi kwanini msilipe wakati tupo nchi moja? Siku hizi vijijini ndio Kuna mijumba ya maana!
 
Elfu 10 tu kwa mwaka mbona kidogo, lipeni bana, lipa Kodi Jenga nchi. Mi5 tena.
 
Hapa naona serikali ndo inataka kuharibu kabisa....

Yaani mwananchi wa kawaida kutoka kijijini huko,... Liwale ndanindani au Misenyi hukooo... Aanze kulipia nyumba?

Hili halikubaliki!!!
 
Back
Top Bottom