Ulishawahi kunusurika kifo? Ulijisikiaje vile unaona kabisa unaondoka

Nilipata ajali, 2017 nilikuja kufungua macho siku nne mbele. Nilichokua nakumbuka ni pale roli la mchanga lilipokua linakuja mbele yangu, Kutugonga tulikua kwenye gari ndogo, nakumbuka kuchomoka kwenye kiti kuvunja kioo cha mbele na kutoka kama mshale au kuruka, (kioo) cha mbele. Nikafikia barabara, nikabingirika nikakutana na yale machuma ya pembezoni mwa barabara, nikagonga mgongo, nikaunda mpaka pembezoni nikakutana na mti, nikaufikia na mgongo nao.
From there, kitu pekee nilisema Kaka yangu hayupo mbali na hapo, aitwe, na sikuweza ongea tena. Only that.
Fuso ilipiga upande wa dereva mbezi temboni opposite kilimani bar, nawashukuru sana enzi zile watu walikua fasta, niliambiwa kupitia siimu yangu kaka yangu alipigiwa akafika na kunipeleka bochi. Enzi hizo hospital bado mbichi. Pale kifo kilikua tayari ila moyo ulipigana sana.
Pole mkuu.lilifeli brake mpaka aje uelekeo wenu?
 
Nliparamiwa na gari nikarushwa mbali kinoma waliokua karibu wakawa wanasema "huyu ashakufa" Mimi nkawa nawaskia lkn kujibu siwezi kunyanyuka siwezii nikawaza huenda kwel nimekufa sema sijui, nlikuja kupata fahamu baada ya masaaa kadhaaa nakuta kila Dr anasema lake huyu nyuzi mwingine X ray
 
Wachawi nyie wasikieni tu tena wale wachawi wa zamani walikuwa na roho mbaya sana achana na hawa wanga wa siku hizi wanaodeal na mambo chuma ulete.

Niliwahi kuzimishwa na wachawi masaa matatu nyumbani kijijini huko kandaziwa watu wakajua nimeshavuta enzi hizo hata mochwali hakuna majirani wakaanza kukusanyika kufanya msiba bahati nzuri kulikuwa na Mzee mmoja alikuja pale nyumbani akaambiwa issue yangu akaomba baiskeli akaenda kwake kuchukua dawa ya kienyeji akanipulizia nikazinduka
 
Mgodini huko lwamgasa geita,nilikuwa shimoni nachoronga mwamba,kumbe huko juu kuna sehemu ilikuwa na ufa wa muda mrefu tu,kutokana na milipuko ya mara kwa mara hiyo sehemu ufa ukawa unazidi kutokea. siku hiyo nikapiga kaz mimi na jamaa yangu(rip mangu aka ntuzu man)ghafla udongo ukaanza kudondoka kidogo kidogo kiasi cha kutokuhofia chochote. Machale yakanicheza nikamwambia mshkaji wangu tupande,mi nikatangulia yeye akawa ananifata kwa juu,nikaivuka ile sehemu yenye ufa kwa umbali kama wa mita 4 hivi,ile nimevuka tu nikasikia muungurumo mkubwa sana kumbe ni ile aridhi inaporomoka,ikawa imeshuka na mshkaji wangu mpaka chini kama mita 35 kutokea pale,nilipanda juu kwa kasi ya 5g huku nikiwa nimerukwa na akili kwa kile nilichokiona.
Mkuu wewe ni blaster? Njoo mwime tufanye kazi.
 
Uliathirika, nilitibiwa kwa mwaka mmoja na miezi saba. Nililazwa kutoka july 2017 mpaka February 2018 bochi. Nikaanza physiotherapy nikiwa natokea nyumbani, ila siikuwa naweza kukaa wala kusimama tena, maana nilipata sana vidonda, uzuri sikuwahi kuwa mpweke wala kukata tamaa, i knew maumivu yakikata nitatembea tu. Nilikua napiga hadi chuma kama nafanya bench press nikiwa kitandani, after six months i was on my foot. Wakati natoka hospital ilikua ni Mungu tu mimi kuweza kusimama ila i was capable at 6 months na nikarudi lwenye shughuli zangu 2019. Nikiwa fiti kabisa.
Wengine uliokuwa nao kwenye gari nao vipi?
 
Mara ya kwanza nilinusurika kwenye mto nikiwa na miaka 7 tulikuwa jumla 4, wenye miaka 7 tulikuwa wawili wengine wadogo.
Kwa bahati mbaya tulimpoteza mmoja.

Mara ya pili maji hayo hayo mto huo huo nikiwa na miaka 12, nilinusurika tena.
Nilivyoona hakuna msaada, zile sekunde hatari chache za mwanzo nikajizamisha kabisa nikawa kama mtu aliyedhamiria kuogelea na nikafanikiwa kujiokoa ila nilikuwa hoi.

Tangu hapo sikuwahi kuogelea tena maji ya mto, ziwa wala bahari.
 
Sikujua namna nilivyohama seat iliyoondoka na watu karibia wote baada ya ajali, Mungu yupo , Tena ana uwezo kuliko akili zetu

Mungu awalaze mahari pema peponi wale ndugu, they were the best compared to me, sijajua kwa Nini nilibaki, ila Mungu huyu anajua sababu,

Kama anasoma comment hii huyu Mungu ajue it sounds like prayers,awafunulie Hawa wasioamini mambo aliyonifanyia Mimi ili wamwamini kama Mimi,japo Bado Huwa natenda dhambi ilaa asinichoke,.

Guys Mungu anatupenda sana, nilijifunza kitu kufa au kuishi ni kwa neema tu, anapokufa mtu usihoji sababu ya kufa kwake,Kuna watu kibao wanatakiwa kufa ila wanaishi, alafu wanaokufa unaona kabisa kama wangeishi hiviii ila ndio wamekufa, MIMI NI NANI MPAKA NIWEPO HADI LEO!!???
 
Mimi nliwahi nusurika kuzama baharini,pale coco beach.
Kipindi nasoma nna kama miaka 17
nliingia na wenzangu kwenye maji ila upande wangu sikushika boya nliingia kama nlivyo,usawa wa magoti
sababu Sina nguvu maji yakanizidi nguvu yananisukuma kwenda ndani.nkitaka kurudi ufuoni Yale mawimbi yanayorudi toka ufuoni (ufukweni) yananisukuma na kunirudisha kwenda ndani zaidi.nlipoteza nguvu sababu ya kushindwa kupumua vema,nkajikuta nimekaa kitako chini ya maji.
Akili ikaniambia unaenda kufa Binti fumbua macho utoke nje sio mbali sana.maana nlipoteza uelekeo sijui niende kulia au kushoto,sijui ufuoni kuko upanda gani tena.nkichelewa ntazimia Kwa kukosa pumzi.nlkua naenda huku najiona,najiambia ndo basi Tena.
nlivofumbua macho naona upande mmoja uko deep giza kunatisha,upande wapili angalau Kuna mwangaza Kwa juu nkaanza kutambaa Kwa kushikilia miamba chini maana nkisimama nguvu Sina wimbi litaanirudisha Tena kulekule.
Hatimaye nikatokea nje.huku nimechubuliwa miguu inavuja damu.
Mpaka Leo sigusi kamwe maji.

Kama huna nguvu usiingie kwenye maji.
Mimi niseme tu namshukuru MUNGU kwa zaidi ya second chances anazo nipa, nimechomoka ktk ajali nyingi na kuwa ktk sintofahamu nyingi za kiimani, uchawi , vurugu mechi nyingi. matukio ni mengi ya kuogofya, lkn yale machache yasio amsha memories mbaya nitashare nanyi kama ifutavyo.

1. Kuna siku,nimetoka zangu kuzurula usiku. Kijana wa watu single, sina majukum sio mtu wa club wala pombe but i loved kuwa road night, music , sauti ya upepo nikishusha viooo vya gari ( Nahisi Raha). Zaidi ya yote ni kuomba ktk gariz una drive unazunguka DSM Ktk huku unaomba, nalihisi kuwa connected sana na MUNGU.

Siku ya mkasa ilikuwa ni ligi na Magari ya magazeti, kwa mara ya kwanza nakutana nayo usiku, sifa zao ngoja nizione ni za kweli??

Jamaa walikuwa kama watatu au wanne, nikaunga nao. Kumbe wao wanatabia za kubeti nani atawahi kuvuka point fulani. Nimeenda nao fresh kabisa, niko mkiani au akizembea namuacha mmoja wao.

Jamaa wakafanya ni personal sasa. Kuna mmoja akiwa mbele yangu, akatoa ishara ya ku overtake lori la mbele. Kosa langu lilikuwa kutembea na macho ya dereva mwenzangu, kumbe yeye ameshaikadiliq lori linalokuja atakuwa amesha rudi ktk site before kukutana nalo uso kwa uso.

Ametoka, nimetoka naye ( ligi). Ile anarudi tu, ghafla naona lori hilo mbele ikiwa lile ninalo overtake sija limaliza bado. So kushoto lori, Kulia ni unaingia darajani, mbele Lori, ni MUNGU alinitoa hapo bila mchubuko wa gari wala mwili.

MUNGU tu connect wote akili, mimi nikajikuta nimekaa ktk mstari mweupe wa kati ( wa kutengesha Lane). Kila lori likabana upande wa kushot ktk njano, nikwa Sandwiched. Yaan niki kata hata kidgo nakutana na Lori.
Hapo ziliembea honiiiiii tuuuuu.

Nilivuka na kumshukuru MUNGU
 
Back
Top Bottom