Ulishawahi kunusurika kifo? Ulijisikiaje vile unaona kabisa unaondoka

Mwezi wa 12 nilikuwa likizo maskani. Ghafla usiku nikiwa nimelala nikahisi pua na mdomo havifanyi kazi kule kuhangaika nilisimama, wima nikapita na kaneti.

Muungurumo nilioutoa nyumba nzima waliamka. Nikawa nalala kwenye kochi tu. Kama ndio roho huwa inatoka vile. Kazi ipo.
 
Ulitibiwa kwa muda gani, mgongo haukuathirika sana?
Uliathirika, nilitibiwa kwa mwaka mmoja na miezi saba. Nililazwa kutoka july 2017 mpaka February 2018 bochi. Nikaanza physiotherapy nikiwa natokea nyumbani, ila siikuwa naweza kukaa wala kusimama tena, maana nilipata sana vidonda, uzuri sikuwahi kuwa mpweke wala kukata tamaa, i knew maumivu yakikata nitatembea tu.

Nilikua napiga hadi chuma kama nafanya bench press nikiwa kitandani, after six months i was on my foot. Wakati natoka hospital ilikua ni Mungu tu mimi kuweza kusimama ila i was capable at 6 months na nikarudi lwenye shughuli zangu 2019. Nikiwa fiti kabisa.
 
Nilikuwa naongelea beach msasani na demu muholanzi mwenye asili ya Colombia Sasa tunaenda mbele ghafla nkatumbukia kama kwenye shimo hivi nikawa nazama najiona nakufa kbsa ,akaniokoa alafu baadaye akasema kwao wanafundishwa kuogelea wakiwa na miaka 5 ndomana akaweza kunisaidia ,wakati tukio linatokea yeye ana miaka 20 mim 15....mpaka Leo sijawai gusana na maji ya bahari
 
Uliathirika, nilitibiwa kwa mwaka mmoja na miezi saba. Nililazwa kutoka july 2017 mpaka February 2018 bochi. Nikaanza physiotherapy nikiwa natokea nyumbani, ila siikuwa naweza kukaa wala kusimama, after six months i was on my foot. Wakati natoka hospital ilikua ni Mungu tu mimi kuweza kusimama ila i was capable at 6 months na nikarudi lwenye shughuli zangu 2019. Nikiwa fiti kabisa.
Oh Glory to God, wewe ni mshindi, there is a big purpose satan wanted to stop.
 
Mgodini huko lwamgasa geita,nilikuwa shimoni nachoronga mwamba,kumbe huko juu kuna sehemu ilikuwa na ufa wa muda mrefu tu,kutokana na milipuko ya mara kwa mara hiyo sehemu ufa ukawa unazidi kutokea. siku hiyo nikapiga kaz mimi na jamaa yangu(rip mangu aka ntuzu man)ghafla udongo ukaanza kudondoka kidogo kidogo kiasi cha kutokuhofia chochote. Machale yakanicheza nikamwambia mshkaji wangu tupande,mi nikatangulia yeye akawa ananifata kwa juu,nikaivuka ile sehemu yenye ufa kwa umbali kama wa mita 4 hivi,ile nimevuka tu nikasikia muungurumo mkubwa sana kumbe ni ile aridhi inaporomoka,ikawa imeshuka na mshkaji wangu mpaka chini kama mita 35 kutokea pale,nilipanda juu kwa kasi ya 5g huku nikiwa nimerukwa na akili kwa kile nilichokiona.
Inatisha
Mwenzio hakuokoka?
 
Back
Top Bottom