ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,589
HABARINI MABESTITO:
Nimekuja kivingine kabisa kwa wale walionizoea watashaangaa kuona ladyf leo vipi kaja na kaswali ndani yake
watashangaa kulikoni leo mswahiba wetu kaingia spidi haina gavana kwa kututandika kaswaili ,
mabestito wangu wala msihofu kuna wakati tunakuja kwa kuwatia moyo, kuna wakati tunakuja kwa kuwakandamiza
wale wote wasioweza kujirekebisha tabia zao hususani WANAUME na kuna wakati mwingine tunakuja kuchemsha bongo pia. Leo Mfundaji wenu nimekuja na kitu ambacho nimekiweka kama swali ila kimenikera sasa naona nije kuwaelemisha
na kuwafunda wale ambao wanatabia hii waiache mara moja kwani haipendezi kwa jamii
ULIONA WAPI?
Bestito uliona wapi Mwanaume mzima umekuwa tegemezi kwa mkeo,? wewe kila kukicha huna pa kueleweka
kikazi, kibiashara wala kishughuli yoyote unakinga mkono hutadhani wale tunaowasaidia ambao hawana
uwezo wa kujisaidia? Hunashindwa hata kufanya biashara ndogondogo familia yako ikapata kitu toka kwako
Je uliomuolea nini binti wa watu mpaka unamchosha kwa kwa kuwa tegemeizi , Mwanamke huyohuyo atafuta
pesa, huyohuyo aijali familia, huyohuyo tena awalee watoto uliompa, huyohuyo tena awaangalie wazazi wa pande
zote mbili, huyohuyo tena akupe mahitaji yote ya kifamilia. Jamani si unamchosha mtoto wa watu na unamzeesha
bure kabla ya wakati wake. Kwanini usijitume nawe ili familia yenu iwe bora na yenye kustawi?
Upande wapili nao tena
Uliona wapi Mwanamke mwenzangu nawe unakaa tu unasubiri eti baba alete maakuli ndipo ukinge kwenye bakuli
uanze kula, Baba achakarike huko kwa kila hali nawe umekaa huna chochote cha kukuingizia kipato jamani mwanamke
mwenzangu kwanini wakati kuna shughuli nyingi za kufanya kuna kusuka mikeka, kushona, kufanya kile kitu halali cha
kukuingizia kipato kwanini unakaa tu unasubiri jioni mzee akija akurushie alichopata huko hujui kuwa amefanyaje mpaka
akapata hayo manoti, au vitu . Mwanamke mwenzangu usiniangushe wanawake tunaweza muombe mumeo hela ya
kuanzisha biashara kama huna kitu cha kufanya mshirikishe, muombe kwa kumbembeleza sana ili akupe msingi nawe
usiwe golikipa uweze kuiwezesha familia yako.
MABESITO NAWAASA NA KUWAFUNDA
Kwa nguvu na umoja wa pande zote mbili utasababisha familia kuendelea na hakutakuwa na huhitaji labda ule wa lazima kama familia , Mabestito wangu msimu ndo ushazimika wa mwaka huu 2014 tujitume kwa biidii zetu tusiwe watu wa kumfanya mwenzio hahuzunike kwa wewe kutokufanya kitu cha kuleta maendeleo ndani ya ndoa yenu
Kwa nguvu zote tunaweza kuleta mabadiliko ndani ya ndoa na ndoa zetu zikapona na watoto wakaiga mfano wa wazazi wao
namalizia kwa kwa swali langu pale juu ULIONA WAPI mtama ukakua na kuchanua na kuleta utofauti ndani ya ndoa?
Wasaalamu,
Ladyf
cc: Mamndenyi, Kongosho, @Mtambuzi Asprin, KakaKiiza, Jiwe Linaloishi, Kipaji Halisi, Paloma, mwallu, Chocs, Erickb52, Arushaone, Lady doctor, Passion Lady, charminglady, utafiti, Husninyo, watu8, @Mentor, Asnam, amu, Ntuzu, muuza ubuyu, Excel, @Ben Mugashe, Filipo, Chachu Ombara, sister, Heaven on Earth, Kokutona na marafiki zangu wote karibuni