Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,101
- 128,716
Wanabodi,
Hii ni makala yangu gazeti la Mwananchi la leo.
Wiki iliyopita, mwandishi wa makala hizi, alifanya kosa moja, akaliombea msamaha, lakini bado aliadhibiwa kwa adhabu mbili tofauti, kupitia sheria mbili tofauti, chini ya mamlaka mbili tofauti, zilizo chini ya wizara mbili tofauti!, hili ndilo kaburi kubwa kabisa la uhuru wa habari nchini Tanzania!. Nashauri, ni wakati sasa tasnia ya habari, kuwa chini ya sheria moja, wizara moja na mamlaka moja, vinginevyo Media ya Tanzania, hatuwezi kuwa Mhimili, tutaishia kuwa mediocre na machawa!.
Wiki iliyopita ilianza kwa mwandishi wa makala hii kupigwa rungu kwa kupewa onyo na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, JAB, kwa kutoa maoni yangu huru kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977. JAB ilinitaka nithibitishe, niliposhindwa niliomba radhi na kupewa onyo kupitia taarifa ya JAB kwa vyombo vya habari, lakini hakuna onyo lolote nililopewa, ila taarifa kuwa nimepewa onyo nimeiona na JAB pia wameni copy. Baada ya Onyo la JAB, likaja rungu la TCRA kuishukia online line media nilikotoa yale maoni.
Kama media kwa umoja wetu tutaendelea kunyamazia hivi vitendo vya ukiukwaji wa katiba, kunakofanywa na mamlaka za udhibiti, Media ya Tanzania kamwe haitakuja kuwa mhimili wa 4!, tutaishia kuwa mediocre, na machawa wa watawala na viongozi, kitu ambacho hakitasaidia taifa.
Waandishi majasiri na wa kweli wapo, na vyombo vya habari vya kiukweli na vya kijasiri vipo, na miongoni mwa waandishi majasiri na mimi nimo, kwenye kuusema ukweli, kiukweli kabisa mimi nimenyooka kama rula, sipindishi wala simuogopi mtu yoyote, hivyo hili lililotokea, nasimama nalo kwa ulalo ulalo mpaka lirekebishwe, uhuru wa kutoa maoni, uheshimiwe.
Vyombo vya habari vya kijasiri ka JF na Jambo TV, ila media ya Tanzania, tunapitia wakati mgumu sana, tunateseka sana, ila basi tuu, hatulalamiki, tunakufa kizungu na tai shingoni, tukifanya kosa moja, tunashukiwa kama mwewe na sio tuu kupigwa rungu, lingekuwa moja, ni kosa moja, tunapigwa marungu mawili kwa kuhukumiwa na ma Pilato wawili tofauti, wenye mamlaka mbili tofauti, kwa kutumia sheria mbili tofauti, zilizoko chini ya mawaziri wawili tofauti, hivyo mtu kwa kosa moja, kuhukumiwa adhabu mbili tofauti na mamlaka mbili tofauti kwa kosa lile lile moja, jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za natural justice!
Siku ya kuzinduliwa rasmi kwa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, JAB, niliandika makala kwenye gazeti hili kuipongeza, na pia nikaitolea angalizo. Leo ni mwaka mmoja wa uwepo wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, hivyo naandika makala nyingine kuipongeza kutimiza mwaka mmoja, ila sasa sio tuu kuipa angalizo, bali pia kuiomba isifanye uchawa kwa serikali na viongozi wa serikali kwa kutoa maonyo batili na maonyo vivuli, kwa waandishi wa habari, ambayo yako kinyume na Ibara ya 18 ya uhuru wa kutoa maoni, na wakati huo huo huo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, ikipiga rungu kwa chombo cha habari, hivyo mwandishi wa habari na chombo cha habari, kuhukumiwa mara mbili, kwa kupigwa marungu mawili, na kuadhibiwa mara mbili, na vyombo viwili vya udhibiti, kupitia sheria mbili tofauti, zilizo chini ya mamlaka mbili tofauti, Bodi ya Ithbati iliyo chini ya Wizara ya Habari inayotumia sheria ya habari, na mamlaka ya Mawasiliano, TCRA, inayopiga rungu lale kupitia Sheria ya Utangazaji, hivyo kukiuka kanuni ya pili na natural justice, inayosema, no one should be condemned twice for the same offence!, yaani mtu asihukumiwe mara mbili kwa kosa lile lile!.
Hapa naomba kutoa pongezi kwa mamlaka zote mbili, JAB na TCRA, kutoa nafasi ya mtuhumiwa kupatiwa haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa, kwa upande wa JAB ni unapigiwa tuu simu, bila barua yoyote ya wito, yenye tuhuma rasmi, na kutakiwa kufika ndani ya saa 24!, na baada ya kujieleza, unatolewa hukumu, ambayo wewe mtuhumiwa hupewi maandishi yoyote, bali unakuja kusoma tuu huku yako kwenye taarifa ya JAB kwa vyombo vya habari, hii mimi nimeiita hukumu kivuli. Ila kwa TCRA, angalau, wao walileta barua ya wito, yenye tuhuma specifi, ambayo imeletwa saa 5 asubuhi, na kutakiwa kufika mbele ya kamati ya maudhui saa 8 mchana, hivyo ndani ya saa 3, uwe na majibu ya maandishi!. Hivyo ndivyo sheria, taratibu na kanuni zinavyoelekeza?!.
Pamoja na JAB kufanya vizuri kwa kusajili wanahabari kadhaa, JAB bado ina changamoto zifuatazo
Kifungu cha 12(1) Waziri atateua wajumbe 7 kuwa wanabodi ya ithibati ya tasnia ya habari. Japo Bodi hii inauwakilishi wa wadau mbalimbali wengi wakitokea kwenye tasnia ya habari, wanabodi hao wote watateuliwa na Waziri. Ingekuwa vyema kama Sheria ingesema kuwa watu hao watachaguliwa na makundi wanayoyawakilisha. Kwa mfano, mwakilishi wa wahadhiri wa vyuo vya tasnia ya habari wangepaswa kuchaguliwa na wahadhiri wenyewe, vilevile, wawakilishi wa wanahabari pia wanapaswa kuchaguliwa na wanahabari wenyewe.
Mfumo huu wa kuchagua wawakilishi ndio bora zaidi na unaendana na demokrasia na utawala bora huku ukihakikisha kuwa maslahi ya kundi Fulani yanalindwa na hoja zao kufika bila kupindishwa. Mfumo wa wawakilishi kuteuliwa na wakilishwaji wenyewe umetumika kwenye sheria nyingi hapa nchini na hivyo ni vyema sheria hii ikarekebisha ili kuleta uwakilishi thabiti na kamili. Ikumbukwe kuwa tasnia ya habari ni tasnia nyeti inayohitaji uhuru na ueledi wa hali ya juu hivyo uwakilishi wa moja kwamoja wa makundi yote ya tasnia hii kwenye bodi ya ithibati ni muhimu.
Sheria ya Huduma za Habari ya 2016 kwa mapana yake ni sheria nyeti na inayosimamia tasnia nyeti na inayopaswa kuwa huru japo imejitahidi kuweka mazingira bora zaidi kwa wanahabari ikiwemo, Kutambua uhuru wa habari,
Kuwatambua wanahabari kama wanataaluma kwa kuwaundia Bodi ya Ithibati na orodha ya wanataaluma hao, ni jambo jema na zuri, swali ni kwanini mpaka sasa Baraza la Huru la Wanahabari halijaundwa?!. Kwanini mpaka sasa mfuko wa mafunzo ya wanahabari haujaanzishwa?! Kwanini mpaka sasa sharti kwa mmiliki wa chombo cha habari kuwakatia wanahabari bima ya kazi yao bado halijafanyika?!.
Hitimisho.
Kitendo cha vyombo vya habari Tanzania kuwa chini ya wizara mbili tofauti, chini ya mawaziri wawili tofauti, chini ya sheria mbili tofauti, na mamlaka mbili tofauti ni kaburi la uhuru wa habari Tanzania!. Ili tuwe uhuru wa kweli wa habari, lazima tufike mahali, tuwe na wizara moja ya Mawasiliano, Habari na Utangazaji, chini ya sheria moja, waziri mmoja, mamlaka moja.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.