Ulinzi tanzania upo kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulinzi tanzania upo kweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nahavache, Feb 6, 2012.

 1. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  [h=2]Nimeisoma hii habari leo kwenye gazeti la Nipashe, :: IPPMEDIA kilichonishangaza ni ulinzi ulioko katika bandari zetu kama kweli kuna usalama. Kama meli iliingia ikapakua mafuta baadae sana ndio mafuta yakakamatwa, tuna usalama kweli watanzania?

  Meli yakamatwa ikipakua mafuta ya magendo Z`bar
  [/h]
  Meli ya mafuta na mizigo ya MV Mashallah imekamatwa ikishusha mafuta ya magendo katika Bandari ya Malindi mjini Zanzibar, ikiwa na shehena ya lita 81,000 yenye thamani ya Sh. milioni 162.
  Mafuta hayo yamekamatwa wiki moja tangu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kufanikiwa kukamata matukio matatu ya ukwepaji wa kodi katika Bandari ya Malindi, Wete na Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, na kusababisha maafisa 27 wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakiwemo askari wa forodha, kuhamishwa katika vituo vyao vya kazi.

  Uchunguzi wa NIPASHE mjini hapa umegundua kuwa mafuta hayo yalikamatwa juzi saa 8:00 mchana, yakipakiwa katika gari la kubebea mafuta, aina ya Iveco, lenye namba za usajili Z 676 BJ.

  Gari hilo linamilikiwa na mfanyabiashara, Abdallah Omar wa visiwani humu.

  Akizungumza na NIPASHE, Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji na Bandari wa Jeshi la Polisi Zanzibar, SP Martin Lissu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba tayari kazi ya uchunguzi imeanza kufanyika ikiwemo kuwasaka wamiliki wa mafuta hayo.

  "Ni kweli nimepokea taarifa kutoka kwa wasaidizi wangu, na baadaye Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), kuhusu kukamatwa kwa mafuta ya magendo yaliyokuwa yakishushwa ndani ya Bandari ya Malindi," alisema SP Lissu.

  Alisema kwa mujibu wa utaratibu, gari haliruhusiwi kuingia getini hadi likaguliwe na kufahamika malengo ya kuingia ndani ya bandari, lakini alisema uchunguzi wa kina unahitajika kufanyika ili kubaini ilikuwaje gari hiyo liliingia na kujaza mafuta bila ya kufuata utaratibu, hasa kwa kuzingatia kituo cha mafuta kinachotumika kujazia mafuta katika meli, kipo eneo la Mtoni.

  Akizungumzia tukio hilo muda mfupi baada ya kukamatwa kwa meli na gari lililokuwa likijaziwa mafuta hayo, Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Mohamed Hashim Ismail, alisema walipokea taarifa kutoka kwa raia wema na kufanikiwa kuikamata meli hiyo kabla haijamaliza kuteremsha mzigo.

  Alisema kwa mujibu wa sheria ya ZRB, mafuta hayo yatauzwa kwa makampuni yaliyosajiliwa kisheria na fedha zitakazopatikana zitaingizwa katika mfuko wa Hazina wa Serikali, kwa ajili ya kutumika katika shughuli za maendeleo ya wananchi wa Zanzibar.

  "Tumepokea taarifa na tumefanikiwa kuikamata meli ya MV Mashallah ikiwa inajaza mafuta katika gari la kubebea mafuta, na hii sio mara ya kwanza kukamata mafuta ya magendo, tunawashukuru raia wema kwa kutoa taarifa zilizotusaidia kukamatwa kwa meli hiyo," alisema Kamishna Hashim.

  Alisema biashara ya magendo ya mafuta kwa upande wa Zanzibar hivi sasa inakabiliwa na matatizo ya ukwepaji wa kodi, kutokana na vitendo vya baadhi ya watu kuuza bidhaa hiyo katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria, na ZRB kwa kushirikiana na vyombo vya dola, imekuwa ikiendesha operesheni mbalimbali za kudhibiti vitendo hivyo.

  "Kilichotushtua biashara ya magendo kufanyika mchana kweupe, tena ndani ya bandari, hawa watu wamejiamini kiasi gani kuingia ndani kutoa mzigo wa magendo na meli yenyewe kufunga gati, ndani ya Bandari ya Malindi," alisema Kamishna huyo.

  Hata hivyo, mmiliki wa gari hilo, Abdallah Omar, alisema yeye alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu na kumpa kazi ya kwenda kubeba mafuta kutoka bandarini na kuyapeleka sehemu ambayo angeelezwa baada ya mzigo huo kuanza kutoka.

  Lakini alidai baadaye alipokea taarifa kuwa gari lake limekamatwa na lipo chini ya ulinzi.

  "Hadi sasa simfahamu mhusika, nilipewa kazi kwa njia ya simu, na kabla ya kufanikisha kazi hiyo, nikapokea taarifa mafuta tuliyokuwa tunakwenda kuchukua ni ya magendo na yameingizwa bandarini kinyume cha sheria," alidai mfanyabiashara huyo anayemiliki gari hilo.

  Gari hilo lenye nembo ya kampuni ya United Petroleum, imeelezwa kuwa kabla ya kukamatwa lilikuwa limekodishwa kwa ajili ya kubeba mafuta ya kampuni hiyo na kuyasambaza katika vituo vyake mbalimbali kabla ya kumalizika kwa mkataba wake miaka miwili iliyopita.

  Kiongozi Mwandamizi wa united Petroleum, Ismail Omar Zanga, alisema UP haihusiki kabisa na mafuta hayo na ameshangazwa na wamiliki wa gari hilo, kutofuta nembo ya kampuni wakati mkataba wa kutumia gari hilo ulimalizika siku nyingi.

  Hata hivyo, alisema wameshachukua hatua za kuwataka wamiliki wa gari hilo kufuta nembo ya kampuni hiyo.

  [h=2]Meli yakamatwa ikipakua mafuta ya magendo Z`bar[/h]

  By Mwinyi Sadallah  6th February 2012

  [​IMG]
  Email  [​IMG]
  Print  [​IMG]
  Comments

 2. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Unashangaa hilo nenda pale kia twiga walisafirishwa kwenye ndege ya jeshi la Quatar bila hata ya mgambo kujua.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ulinzi utoke wapi na wewe bana??

  Mbona nyie watu wakati mwingine mnapenda uchokozi hivi wakati ujambazi wenyewe ni mradi rasmi wa baadhi ya viongozi wetu nchini tangu enzi za Ustaadh Mahita aka Ngunguli Mzee wa Visu, Mapanga na Tomato Sauce?
   
Loading...