Kombo, maoni yangu ni haya:
1. Ulinzi shirikishi ambao ni effective ni ule unaowashirikisha wananchi wote - kila mmoja anakuwa mlinzi wa jirani yake. Nchi nyingine kama Uingereza unaitwa ‘good neighbourhood'. Ulinzi huu unafanyika kwa namna hii: mwananchi anapomwona mtu anayemtilia mashaka sehemu alipo, anawajulisha watu wa nyumbani hapo ili wajiridhishe kama ni mgeni wao au la na waweze kuchukua hatua kama na wao wana mashaka.
Ulinzi wa aina hii una mafanikio kama kila mtaa utakuwa na utaratibu mzuri wa kupeana habari. Ulinzi unaohusu kikundi fulani cha vijana kama walinzi wa usiku (kama inavyoonekana ikifanyika hapa Tz) hauna tofauti na sungusungu, ambayo haikuleta mafanikio sana (walau sehemu ninakotoka mimi).
2. Kuhusu ulinzi shirikishi na kura shirikishi kama alivyo‘coin' mtu niliyem‘quote' alichokuwa anazungumzia ni kwamba ulinzi ukianza kuwa wa kikundi fulani cha vijana ni rahisi sana kuwa‘influence' na hasa wakati wa uchaguzi na hivyo kuanza kuvunja miiko ya utaratibu mzima wa ulinzi shirikishi.
Hii ndiyo changamoto ya ulinzi shirikishi kama inavyoonekana ikifanyika maana vijana watajiunga na vikundi vya ulinzi shirikishi wakiwa na matarajio fulani kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawana ajira (ni jobless) na huenda baadhi yao hawana rekodi nzuri mtaani kwao.