Ulimwengu wa programu - changamoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulimwengu wa programu - changamoto

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Jan 11, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jan 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Key Explorer , Licence Watch and zingine nyingi hizi ni baadhi ya programu chache ambazo zinamwezesha mtu kuweza kuangalia leseni za programu ambazo zimeingizwa katika computer Fulani , mfano kama uliwahi kuingiza programu ya Adobe photoshop na umepoteza leseni yake basi ukitumia programu hizo unaweza kuona leseni hiyo tena .

  Hii ina maanisha nini ? Maana yake wengine wanaweza kutumia leseni hizo kuuza kwa watu wengine ambao wana miliki demo au trial editions za programu mbali mbali ambazo zinamruhusu mtumiaji kuweka leseni hiyo bila kuwa katika mtandao yaani Offline

  Nafikiri hii ni changamoto kubwa kwa mwaka huu kwa watengenezaji wa programu hizi waandae mpango mpya kwa ajili ya kulinda programu zao na wateja wao kuhusu suala hili

  Niliwahi kujaribu jambo moja , wakati Fulani nilikuwa na programu ya CUBASE 4.1 nikaingiza katika computer 2 tofauti moja ikawa katika mtandao nyingine hakuna nikaweza kutumia leseni moja kwa wakati mmoja ila ingine nilipoongiza tu wakati wa kufanya updates ndio nikaelezwa kuhusu hujuma hiyo hiyo ilikuwa ni majaribio tu lakini .

  Pamoja na mgongano huo wa leseni kuna ujio wa programu ambazo ni portable kwa sasa umeshika kasi sana , wiki iliyopita nilikuwa natafuta cubase katika mtandao nilipata version ya kisasa zaidi lakini ilikuwa na ukubwa wa zaidi ya mb 120 hiyo ni kubwa kwa kweli halafu nilitakiwa kuinunua .

  Unafikiria ukubwa wa programu yenyewe , spidi zetu za mtandao hapa nyumbani na gharama utakazo tumia kudownload , ikabidi nitafute portable programu ya kisasa kama hiyo hivyo .

  Nilipata ilikuwa ni mb chini ya 30 ilikuwa iko licenced tayari nilitakiwa kufanya extraction na kutumia tu ,.

  Ndugu msomaji ukiwa na programu ambayo ni portable huhitaji kufanya installation unaitumia kama ilivyo unaweza kuhifadhi ndani ya flashdisk , cd au popote katika computer yako lakini haiwi installed .

  Moja ya faida yake ni kwamba mtu hawezi kuiba licence kwa kutumia programu ingine kwa sababu haiwi installed , mbili ni ngumu kuharibiwa na virus au programu zingine halafu mwisho kabisa haihitaji wewe kuwa mtaalamu au kwenda masomo yoyote kama programu zingine unahitaji kumwita mtaalamu aweze kukusaidia kuinstal .

  Kwa leo ndio hiyo tu

  Nafikiri hii ni changamoto kuu kwa mwaka huu wa 2009 katika mambo ya programu na usalama wake

  Kumbuka haya ni mawazo yangu tu – Sio lazima niwe sahihi kwa kila kitu
  Yona maro
  Techtz@gmail.com
   
Loading...