Ndugu, Nimependa kukushirikisha jambo hili ambalo, kimsingi, katika ulimwengu wa sasa halikwepeki kabisaaa...
Jambo hili ni kama kichwa cha mada hii kinavyosema hapo juu. Nina amini kuwa umeshawahi kusikia hili neno "ELECTRONICS", na kwa ulimwengu wa sasa siyo neno geni kabisa, kwa sababbu kama hujasikia mtu akisema, basi utaona maduka yameandikwa, tunauza vifaa vya electronics na umeme. n.k.
Labda nianze kufafanua, nini maana ya neno hili Electronics?
Kwa maneno machache sana, Electronics ni sayansi inayohusu uundaji wa saketi za umeme ambazo ndani yake kuna vifa ambovyo vinauwezo wa kuuongoza mtiririko wa umeme huo katika tabia mbalimbali. Zingatia; kuna tofauti kati ya saketi za umeme kawaida na zile za electronics. Hebu tufuatane, angalau ufahamu tofauti hiyo.
Kwanza, neno lenyewe electronics, linatokana na chembe inayoitwa electron ambayo ni mojawapo kati ya chembe tatu zinazopatikana katika atom zilizomo kwenye mada mbalimbali. (neutron, proton na electron). Kila kitu tukionacho kwa macho au tusichokiona kwa macho haya, kimeundwa na chembe ndogo sana iitwayo atom, chembe hii ni ndogo kiasi kwamba huwezi isagasaga ikatoa chembe nyingine tena. Sasa, atom inaundwa na hizo chembe ambazo zina chaji tofauti, kama; Neutron haina chaji, Proton ina chaji chanya (+) na Electron ina chaji hasi (-). Zingatia lengo letu hapa ni kumzungumzia huyu "ELECTRON"
Hii electron ni chaji hasi (-) ambayo yenyewe hupatikana nje ya atom. Hii chembe inatofautiana kitabia kati ya mada moja na nyingine. Mada zenyewe ziko katika hali tatu, yaani ;- mada ngumu, kimiminika na gesi. Electron zilizopo kwenye mada ambazo hazijafungamana sana huwa na uwezo wa kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine. na Mada hizo huitwa ni vipitisho vizuri vya electrons. wakati electron zinatIririka katika mada hiyo ambayo inatengeneza kama njia ya mtririko wa hizo electron, mtiririko huo unaitwa UMEME.
Kwa leo naishi hapa kwanza nitaendelea wakati ujao. samahani nimetumia kiswahili inawezekana maneno mengine yasieleweke vizuri ila ni kutaka angalau Wabongo waelewe. byeeee....
"Yesu akamwambia, Mimi ndimi, njia, na kweli na uzima, mtu hawezi kuja kwa Baba ila kwa njia ya Mimi
. Yohana 14:6."