Ulimbukeni wa Dini Na Siasa Za Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulimbukeni wa Dini Na Siasa Za Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WaMzizima, Jul 9, 2012.

 1. W

  WaMzizima Senior Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa kweli inasikitisha sana hali nchi yetu iliyofikia, hivi sasa ni nadra kufungua gazeti au chombo cha habari bila kuona kiongozi fulani yuko mara na kanisa hili au msikiti ule kuufanyia harambee. Kwangu mimi hii ni hali ya kusikitisha halafu tunalalamika kuhusu udini. Angalia utitiri wa thread humu JF kuhusu masuala ya dini pia, hii yote ni ishara ya udini unavyoanza kupenya kwenye jamii yetu. Kila mmoja anaona kama mwenzake anapata zaidi ilhali hii nchi ni maskini na tunayo mambo ya msingi tunayaacha ambayo yatatuletea maendeleo tunaendekeza malumbano yasio na maana kwenye masuala ya kidini ambazo wala si asili yetu.

  Nawaonea huruma wakristo na waislamu wote wa nchi hii, mmechotwa akili zenu na dini ambazo zililetwa ili kuwapumbaza akili babu zenu nanyi mnaendelea kuzikumbatia na kutengana...kwa kweli mashujaa wetu wa kweli kina Kinjekitele na Mkwawa na wenzao wanatikisika makaburini maana walipigana na kutoa mhanga maisha yao ili sisi wa sasa angalau tufunguke macho na kuwa na upeo wa kuheshimu mila na dini zetu asilia sio kufuata hizi za waarabu na wazungu/wayahudi.

  Angalieni huku zilipoanzia kwenyewe kuna machafuko yasioisha kila siku wanazozana na kuuwana, je nasi hiyo ndio kweli njia sahihi ya kufuata? Tufunguke akili zetu na kuukataa huu ushabiki na uzindina usio na maana.

  Kihistoria hizi dini zilitumika kutukandamiza na kutunyanyasa zikahalalisha utumwa wetu kwao, zikahalalisha sisi watu weusi kuwa raia wa chini tena kwenye nchi zetu wenyewe, na kuhalalisha kuwa tuwaone waarabu/wazungu kuwa wao ni bora zaidi yetu, hadi leo dhana hii bado inaendelea, wakristo wanajiona wao bora na waislamu hivohivo. Hizi dini ni za kibaguzi sana toka enzi hadi sasa hilo halijabadilika wala halitobadilika kamwe.

  Tufungukeni macho na mioyo yetu tuone ukweli tufuate asili zetu, huu uislamu na ukristo ni ulimbukeni wa hali ya juu!! na sasa mnabishana na kuzozana, Shame on you...angalieni wenzenu wachina, wajapani, wahindi kwao wanaabudu dini zao miaka yote hawana huu ulimbukeni toka mashariki ya kati...waachieni waarabu na uislamu wao, na wazungu/wayahudi na ukristo wao sisi tuna dini zetu asilia na matambiko yetu, tuyafuate na kujikomboa kifikra!

  Waafrika wazamani pia walikuwa na Mungu mmoja nae anaitwa Mola, jina asilia na Mola halina uwingi ni mmoja tu!

  Nasema imetosha sasa tuache huu ulimbukeni...bila hivyo hii laana itatupeleka pabaya.
   
 2. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Hili nalo neno lets think outside the box wananchi hizi dini hizi zina walakini... Naomba mtu anambie imani ni nini ? Halafu tuendelee kujadili.
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Hili la udini kuna wapuuzi wachache wanaolitumia ku divert attention ya watanzania katika kujadili mambo ya msingi,hili linatumika kuwagawa watanzania ambapo wengi bila kutafakari kwa kina wanajitumbukiza kichwakichwa, na serikali inahusika moja kwa moja kwa kulilea hili jambo kwani haichukui hatua zozote za makusudi kulikemea matokeo yake imekuwa SCORE kwa wapotoshaji!, tutambue tu kuwa udini ukilelewa hakuna atakayekuwa salama nchii hii
   
Loading...