Ulimbokanization in Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulimbokanization in Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mlachake, Aug 8, 2012.

 1. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  [h=3]Askari Aliyejinyonga Aaacha Ujumbe Mzito[/h]

  [​IMG]

  [​IMG]


  Baadhi ya wananchi na maaskari wakijadiliana jambo kwenye mwili huo wa Afande Dunga
  --


  Na Danstan Shekidele
  Siku chache kabla ya kifo chake askari polisi mwenye namba F 3276, Donald Mathew (33), aliyejinyonga juu ya mti katika daraja la Shani, mkoani Morogoro alimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani kueleza kinachodaiwa kuwa ni ufisadi unaofanywa na vigogo wa polisi nchini, imebainika.


  Polisi huyo aliyefahamika sana kwa jina la Dunga aliwahi kutoa tuhuma nzito dhidi ya maofisa, wakaguzi na polisi wa kawaida, mkoani Morogoro mwaka jana lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya maofisa hao.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fustine Shilogile, jana alisema jeshi hilo, lilipokea taarifa za kujinyonga Mathew jana asubuhi.


  Alisema askari huyo, aijinyonga kwa kutumia vipande vya kamba ya kanga ambavyo viliunganishwa na hakuacha ujumbe wowote unaoeleza sababu ya kuchukua uwamuzi huo.


  Alisema askari huyo kabla ya kufanya tukio hilo, alionekana mitaani akinywa pombe katika Baa ya Shani.


  Alisema baada ya kuonekana amelewa, Mathew aliamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu, kitendo kilichofanya baadhi ya askari polisi waliokuwa eneo hilo, kumfuata na kumsihi avae nguo.


  Alisema marehemu, alihamishiwa mkoani Singida kikazi, lakini Novemba, mwaka jana aliamua kuacha jeshi.


  “Pamoja na kwamba marehemu aliacha kazi mwaka jana, sisi kama jeshi bado tunamtambua kama askari mwenzetu… kwa msingi huo tutasafirisha mwili wake Agosti 8, mwaka huu kwenda nyumbani kwake mkoani Kilimanjaro,” alisema Kamanda Shilogile.


  Alipoulizwa kama kifo cha Mathew kimesababishwa na baadhi ya askari waliohusishwa kwenye tuhuma za kuhusika na biashara za dawa za kulevya, Kamanda Shilogile alisema uchunguzi unaendelea, na kwamba ikibainika kama kuna askari aliyehusika atachukuliwa hatua kali.


  Hata hivyo, askari huyo mwishoni mwa mwaka jana, alitoa tuhuma mbalimbali ambazo zilichapishwa katika moja ya magazeti linalotoka mara mbili kwa wiki, zikiwatuhumu askari 9 wa kikosi cha kupambana na majambazi wa kutumia silaha kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.


  Tuhuma nyingine alizotoa ni polisi kukamata majambazi wenye silaha, lakini huachiwa baada ya kupewa fedha na mali mbalimbali, hivyo kushindwa kuwafikisha kituoni.


  Alisema tuhuma nyingine ni polisi kuwakamata wafanyabiashara wa pombe haramu aina ya gongo na bangi bila kuwachukulia hatua zozote baada ya kuhongwa.


  Tuhuma nyingine, zinazodaiwa kufanywa na askari hao ni kushirikiana na matapeli, kutapeli raia wa kigeni na kushirikiana na majambazi kuvunja maduka na kuiba mali za wafanyabiashara nyakati za usiku
   
 2. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  haya madai ya huyu bwana marehemu mbona yapo clear kabisa, kama kuna mtanzania ambaye hayajui, basi ni yule ambaye hajawahi kuingia kwenye 18 za hawa askari wetu. yaani sheria huwa hazifuatwi, ni namna askari mwenyewe anavyotaka jambo liishe, ama kwa rushwa ya PESA au NGONO. vyovyote tu. and no one cares. Kwa Tanzania amani yetu ni kwa sababu Mwenyezi Mungu kaamua kutuhifadhi waja wake. siamini eti polisi ndo wanadumisha amani ingawa wao ndo wanadai hivyo.
   
 3. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Ameshakufa Tunaishia hapo, Hii ndio bongo. Kama ni nchi nyingine nakwambia mambo mengi sana yangefichuka.

  In tZ nobody cares. subiri uone
   
 4. S

  SASTONI Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hakuna tofauti na wale watu wanao bambikiza kesi au kutumia hisia kuwahukumu watu wasio na hatia.haiwezekani polisi wote wako kama unavyodhani bado unahitajika kufanya utafiti bila polisi hali itakuwa mbaya na mmojawapo ni wewe utasumbua sana
   
 5. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,924
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  wanakula hata 200
   
 6. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Huu ni Ujumbe mzito unahitajika kufanyiwa kazi, Japo mnyoror wa wahusika unarudi mpaka kwa wakuu wenyewe
   
Loading...