Uliijuaje JamiiForums?

Mtu mbalimbali

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
315
413
Habari za muda huu waungwana, wanachama na wapenzi wa Jamiiforum,

Ikiwa leo ni zaidi ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa Jamiiforums, mtandao huu umekuwa kwa kasi sana miongoni mwa Watanzania na wanajamii ya East Africa kwa kuwa Mtandao wa huru na wa haki.

Binafsi naweza sema ni Mtandao wangu pendwa kuliko yote, kwani imekuwa kama kilevi kila nikiwa na bando lazima nichungulie Jamiiforums kuna nini.

Licha ya Mtandao huu kuwa mkubwa hadi kufikia kuwa na watumiaji takribani 632,335 (kwa taarifa za saa 14:20 06/04/2023), bado sio maarufu miongoni mwa Watanzania wengi na hivyo kuwa kama Mtandao fulani wa kisiri ama usiokuwa na wafuatuliaji wengi (unaweza thibitisha hili kwa kuangalia watu wanaokuzunguka na ufahamu wao juu ya Jamiiforum).

Lakini pia miongoni mwetu tunao members waliokuwa bega kwa bega toka miaka ya 2008 na wamesimama na Jamiiforums kwa kipindi chote, huku kila mmoja anahistoria yake ya namna alivyoijua Jamiiforums na hadi kufikia kuwa member kindakindaki.

Uzi huu ni maalum kwaajili ya kuchangia ni kwa namna gani tulikutana na Jamiiforums na hadi sasa tunanufaika vipi, je tunajivunia?

Nianze na mimi Rashmane;

Nakumbuka ilikuwa mwaka 2017 nikiwa na simu yangu ya kibatani, sina bando, nimeboeka nikaingia freebasics bana walau nipate kuijua dunia.

Wakati naperuzi huku na huku nikakutana kwa mara ya kwanza na JamiiForums na zaidi nilivutiwa na nyuzi za Jamii Intelligence na Educational Forums.

Mwaka 2018 nikafungua account hadi sasa tuko pamoja kuisapoti JF paka iwafikie Watanzania wote kwa ujumla, kwani huu ni Mtandao super hapa Tanzania.

Karibuni kwa maoni na mchango wenu.

Uliijuaje JamiiForums?🎤

NB:
Kama kuna member unatamani kufahamu alifikaje JF waweza kumtag

Mshana Jr
 
Mwaka 2008 nilifundishwa na luten nyingo (now ni kanal na yupo kozi akiwinda kuwa brigedia)
Aliniambia niangalie list ya matajiri kwa kupitia Google katika orodha ikatokea na jamii forum akafurahi saana kuona habari za kiswahili japo walikuwa wanachangia watu 3 mpaka 10 tu

Mwaka 2010 nikajiunga officially ila sikuwai kuchangia zaidi ya kusoma tu
Kuchangia rasmi nilianza mwaka 2016

Mpaka sasa Nina I'D 34 ila nyingi zao sikumbuki password zake
 
JF haiko popular kwa watu wengi sababu ya uendeshaji wao. Kuna baadhi ya mambo ya msingi hawayazingatii, wanaendesha hii forum kizamani sana.

Hata hiyo idadi unayosema ya members 632335 sio idadi halisi, we are far less than that. Kama wangekuwa wanaruhusu account deletion kama ilivyo mitandao mingine ungeweza nielewa.
 
Nilikuwa nasoma gazeti nafikiri ni Rai au Raia Mwema lilikuwa na safu ya malalamiko ndipo nilikutana na jamaa akiitwa "Malaria Sugu" akilalamika kupigwa Life ban Jamiiforums.

Ndipo nilianza kuitilia maanani Jf though nilikuwa member humu kabla.
 
Mwaka 2008 nilifundishwa na luten nyingo (now ni kanal na yupo kozi akiwinda kuwa brigedia)
Aliniambia niangalie list ya matajiri kwa kupitia Google katika orodha ikatokea na jamii forum akafurahi saana kuona habari za kiswahili japo walikuwa wanachangia watu 3 mpaka 10 tu

Mwaka 2010 nikajiunga officially ila sikuwai kuchangia zaidi ya kusoma tu
Kuchangia rasmi nilianza mwaka 2016

Mpaka sasa Nina I'D 34 ila nyingi zao sikumbuki password zake
Duh
 
Back
Top Bottom