Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Sitakuwa wa mwanzo kupendekeza hivi, ila sababu za kulipendekeza tofauti.
Kwa wale wasomaji wapya: mambo mawili Tanzania yanakuwa ni kama taboo kuyazungumza- mishahara ya viongozi na malipo yao ya uzeeni.
Lakini ukweli haufichiki. Yote mawili hayo yanawagharimu Watanzania matrilioni ya fedha zinazotolewa na watu ambao hata milo miwili kwa siku ni shida! Enough is enough.
Hivi sasa tumepata Rais asemaye ni mcha Mungu. Moja ya mambo ambayo M/Mungu anayachukia zaidi- haijalishi ni mfuasi wa dini gani- ni injustice, dhuluma.
Endapo rais wetu mcha Mungu hatalipatia ufumbuzi jambo hili basi atakwenda kuwa na wakati mgumu atakapokutana na Mungu, na ile ndoto yake ya kupewa uongozi wa kikosi cha Malaika....aisahau!
Hawa marais wetu waliostaafu, na Mawaziri wakuu lazima bonus zao za kustaafu ziangaliwe upya. Hasa hasa kuwekwe sharti kuwa kama kiongozi aliiba basi keshakula pensheni yake huko huko. Anyang'anywe heshima ya kupewa kiinua mgogo.
Haiwezekani wastaafu maskini wasumbuliwe miaka nenda wakati kuna marais wa zamani wenye hoteli Afrika Kusini, hawa wanapatiwa mabilioni ya fedha under your watch halafu useme wewe mcha Mungu! Najua suala hili lazima lipitishwe na Bunge, lakini rais ana jukumu la kuanzisha mjadala huu.
Kweli Mkapa ahitajia kiinua mgongo kinachotokana na fedha za mwuza nyanya sokoni au mwalimu, mwuguzi nk? Kweli watu kama JK, Lowassa, Sumaye, Msuya?
Kama ni hivyo, angalau kuwe na kigezo kwamba kama uliiba serikalini wakati wa madaraka yako basi ndiyo umeshakula chako! TISS na TAKUKURU watatusaidia.