Ulifanyaje kipindi huna hela? Yaani maisha yamekupiga total knock out!

WAKUU EMBU TUJUZENI ULIPITIAJE KIPINDI UKIWA HUNA HELA MAISHA YAMEKUPIGA TOTAL KNOCK OUT AND HUNA KULA KULALA YA UHAKIKA ? .............




MIE NIMEJARIBU MISHE ZA UDALALI ILA HAILIPI KABISAA NA NI MAJANGA BIN VUUU .......SO HOW DO / DID YOU COPE WITH THIS SITUATION ?...............
Ilikuwa noma ndugu yangu noma sana yani niliona nimefika end of the road. Mimi huwa sina fikra za kujiua ila laiti ningekuwa nazo ningejiua maana nilikuwa nna stress si za nchi hii.
Ilipita kama miaka 2 kuanza kurecover hapo hata kodi ishanishnda kanibeba jamaa fulani aisee.
 
Unaamini uwepo wa mungu!?
Kama ndio, chukua hii.

Umasikini/kukosa pesa kunaumiza mnooo, ila ukikubali uhalisia basi utapambana vizuri bila kukata tamaa, usitamani maisha ya mtu.
Pambana kadri uwezavyo ila jua tu kila kitu ni riziki, usipotoboa ni vile mungu hajataka utoboe na wala si kwa uzembe wako, na ukitoboa ni vile mungu kataka na si kwa ujanja wako.

Pambana mzee, ni nyakati ngumu ila amini zitapita tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom