King_Villa
JF-Expert Member
- Feb 6, 2012
- 575
- 378
Habari za siku wadau,
Bila shaka kila mtu yupo hapa duniani kwa malengo ya kuishi maisha mazuri.
Haifurahishi sana kuwa katika maisha ambayo hayakupi furaha na pia inaumiza sana kuona unaishi maisha yaleyale kila siku.
Binafsi nilijaribu kutoka kwa kila njia maishani ila nilishindwa kiukweli.
Nilijaribu kusoma engineering ila sikuona chochote kikiongezeka.
Nikajaribu kusomea uchumi ila hakuna kitu nilijikuta na drop kila kukicha.
Mwisho wa siku nikaamua kukata tamaa kabisa ya maisha na kuwa nafanya vibiashara vya kawaida ila navyo ni majanga. Mwisho wa siku nikaona muda unaenda afu nakuwa niko loose.
Nilitafakari nikaamua nikumbuke kutumia vitu nilivyoambiwa nilikuwa napenda kuvifanya nikiwa mdogo labda naweza nikatoka.
Nikakumbuka niliambiwa wakati nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana zile toys za magari lakini ilikuwa nikiletewa naharibu siku hiyo hiyo kwa kubomoa kwa jiwe nikitafuta anayeendesha ni nani.
Pamoja na kupigwa sana nilikuwa naweza kulia siku mzima nikidai kuletewa toys za gari. Na miaka ilivyoenda nilikuwa na interest na magari sana.
Nilipenda kufuatilia magari sana mifumo ya engine, nilipenda kusoma sana mwenyewe Juu ya viwanda vinavyotengeneza magari na nikafanikiwa kujua vitu vingi kuhusu magari na nikiwa mdogo mzee akisahau funguo anakuta gari nimeshamtolea ndani kwa reverse na hajui nimejifunzia wapi, ananipiga vibao viwili nalia kidogo ila sikomi.
Na miaka hiyo ni manual transimittion ndo zipo ila miaka ilivyokwenda sikutaka kuingia kwenye hiyo sector kwa kuhisi ni kazi za watu wasiosoma. Lakini nilivyokumbuka utotoni nikaona ngoja nikaendeleze hicho nilichokipenda utotoni labda naweza kutoka.
Mungu si athumani nilifurahia sana masomo yale! Nakumbuka siku nilipopata mechanical grade test! Sikulala kwa furaha. Baada ya muda mfupi nikafanya interview nikipambana na watu waliosemea mechanical engineering ilikuwa ni
kazi kukagua engine na nikalazimishwa kufanya bila vigezo na nilifanikiwa kupewa nafasi kama Vehicle Inspector baada ya watu wa Japan kuona kipaji hicho nikapata safari ya kwenda Japan kwenye viwanda vya pikipiki na nikatoa comment kwenye moja ya engine ARC Designer wa pale ndio ikawa chanzo cha maisha kuanza kuwa safi.
Nimefanikiwa kufanya kazi na sport racing company za nje na ndani. Pia nimefanikiwa kuwa kwenye body ya waundaji wa turbocharged engine ya company ya magari ya Marekani ya gari za supra. Niliitwa kwenye body ya uundaji wa engine za Toyota katika 4th generation ya s - FE series ambayo bado haijatoka.
Pia saivi nimesaini mkataba wa miaka 3 na kampuni ya usambazaji wa vipuri vya magari ya Marekani East Africa.
Nimefanikiwa haya pasipokuwa na cheti chotote cha usomi ila nilidhamini kile nilichoamini Mungu alikiweka ndani yangu bila mimi kujua.
Wadau tusikomae na maelimu jaribu kuangalia pia historia yako!