Ulevi wamtia mashakani Michael Phelps

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716

Micheal Phelps ameshinda medali ya dhahabu mara 22 katika mashindano ya olimpiki



Muogeleaji bingwa wa Olimpiki nchini Marekani,Michael Phelps, amekamatwa kwa kundesha gari akiwa mlevi.

Polisi mjini Baltimore, katika jimbo la Maryland, wamesema kuwa Phelps alisimamishwa kwa kuendesha gari kwa kasi kupindukia Jumanne asubuhi akiwa mlevi.

Bwana Phelps hakukataa kushirikiana na polisi aliposimamishwa na kuchunguzwa ikiwa alikuwa timamu. Alishitakiwa na kuachiliwa.

Muogeleaji huyo anayesifika sana aliwaomba radhi mashabiki wake kupitiaTwitter.

"naelewa ukubwa wa kosa langu na ninawajibika sana,'' aliandika Phelps.

''Najua maneno haya huenda hayamaanishi chochote kwa sasa lakini ninawaomba radhi kwa yeyote ambaye nimemuangusha.''

Bwana Phelps, mwenye umri wa miaka 28, alijiuzulu kutoka kwa mashindano ya uogeleaji, baada ya kushinda medali yake ya 22 kwenye mashindano ya olimpiki, katika mashindano yaliyofanyika mjini London mapema mwaka huu.

Polisi walimkamata Phelps na kumshitaki kwa kosa la kuendesha gari kwa kasi akiwa mlevi.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa Phelps alishirikiana na polisi kutoka mwanzo hadi mwisho alipoachiliwa baada ya kushtakiwa.

Phelps ashawahi kushitakiwa kwa kosa lengine sawa na hilo mwaka 2004. Alikiri kosa na kuepuka kifungo cha nje ya miezi 18.

Source:
BBC

http://www.bbc.co.uk/swahili/michezo/2014/10/141001_phelps_mlevi
 
RUCCI, watu wengi maarufu waburudishaji walipata muda mchache sana wa kutafakari maisha ukizingatia wameshika fedha mapema sana. Wengi huko majuu huwa wanakuwa mamilionea hata kabla hawajafika miaka 30, wanasumbuliwa na ulimbukeni.
Hata hapa kwetu mastaa hawaishi vituko.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…