Nyamsusa JB
JF-Expert Member
- Jul 9, 2015
- 567
- 1,565
Hakuna ubishi Marekani wana uwezo Kivita kulinganisha na Uwezo wa Iran Kivita. Takwimu zinaonyesha Marekani Hatakiwi hata Kepeleka Full Kikosi ili Kuichapa Irani, yaani kuichapa Iran Marekani Hapeleki Full Packege ya Mziki mzima wa Kijeshi.
Yaani Marekani Ikiamua kabisa kwa dhati kumpa Kichapo Irani, wanaweza kumpa Kichapo mara tano kwa siku yaani Itawapa Muda wa Kuswali Wa-Irani Swala tano na kila baada ya Swala kichapo kinaanza mpaka Muda mwingine wa Swala.
Wataaramu wa Vita wanasema kama Marekani ikiamua Kuidhibu kivita Irani kwa Moyo Mkunjufu kabisa basi wanaweza kuingamiza Navy yote ya Irani kwa Siku Si zaidi ya Mbili tu. Kinachoweza Kuisaidia Iran kurefusha Vita Kidogo kwa Muda labda ni Iran kutumia Human Shield yaani kuwachanganya Civiliani wa kawaida kwenye Vita na Hivyo kuichelewesha Marekani Kusort Out nani ni Civilian na nani ni Army.
Sasa Nini Basi Kinaichelewesha Iran Kupewa Kichapo chake?
Iran pamoja na kua haina Mlingano au Uwiano wa Karibu wa Nguvu za Kijeshi na Marekani wana Jeuri kubwa ya Kumfanya Marekani asifikiri hata Kumgusa Iran Kijeshi pamoja na Kiburi anachokionesha Iran kwa Sasa.
Kinachompa Kiburi Iran Asiguswe Kimapigano na Marekani na Washilika Wake ni ule Usemi “ Niguse Ninuke”. Yaani Irani ukimgusa tu anaweza Kunuka Dunia Nzima.
Iran Atanukaje Sasa?
Wachambuzi wabobezi wa mambo ya Vita wanasema Marekan kujaribu kumgusa Iran Kimashambulizi ama Kivita ni Kusababisha Machafuko Makubwa ya Amani katika Ukanda wote wa Mashariki ya Kati tena ya Muda Mrefu Usiopimika.Hii Itatokana na Nchi zote za Kiarabu zisizo Upande wa Marekani kumuunga Mkono Irani na kuzishambulia Nchi za Kiarabu zilizo Upande wa Marekani zikiwemo Saud Arabia, Afughanista, Iraq bila kumsahau hasimu mkuu wa Iran Taifa Teule Israel.
Unukaji mwingine wa Iran ni kuwa anaweza asijihusishe yeye moja kwa moja na kutumia makundi ya Kiharakati na ya Kigaidi dhidi ya Saud Arabia, Iraq, Israel na sehemu yoyote Duniani yenye Masilahi ya Marekani.
Hoithi kundi la Uasi la Yemeni linalofadhiliwa na Iran litatumika kuhujumu Miundombinu ya Mafuta ya Saud Arabia kwa kutumia Makombora na Drones na hivyo kuharibu kabisa Miundo Mbinu ya Saud Arabia na kusababisha Mlipuko Mkubwa wa Bei ya Mafuta Duniani na Uchumi wa Dunia Kuyumba na Haswa Uchumi wa Marekani Kudorora na hata Kuanguka Kabisa na Ukawa ndio mwisho wa Uchumi Mkubwa wa Marekani.
Jeshi la Shiite litatumiwa na Iran kuifanya Iraq isipate utulivu na hivyo kuilazimu Marekani kuhusika kwa kiasi kikubwa na Ulinzi wa Iraq.
Hezbollah kundi la Kigaidi linalofadhiliwa na Irani litatumika kuishambulia Israel na Sehemu yoyote Duniani penye Masilahi ya Marekani na kuleta Taharuki kuu Duniani. Yaani Dunia Itasimama kwa Tishio la Matukio ya Hezbollah.
Kufupisha Habari ndefu kua fupi ni kwamba Kivita Marekani ana Kifua Kipana na Pumzi ndefu Kuliko Iran Lakini Irani nae ana Uwezo wa Kugusa Maslai ya Marekani na Hata Dunia Nzima kwa Ujumla. Pia Iran ni kama mwenye Funguo za Amani ya Mashariki ya Kati kumgusa tu Akinuka basi Mashariki ya Kati Hakutokua na Amani na Utulivu kuliko ilivyo sasa.
Hii ndio Ukisikia “Niguse Ninuke” basi ndio inayomsaidia Iran kukabidhiwa Kichapo Chake.