YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,003
Niseme wazi kuwa mataifa ya Ulaya na marekani zilikuwa ni nchi zenye heshima kubwa (ROLE MODAL) kuanzia mitaani,vijijini,mijini na kila kona ya Tanzania.Ukisikia mtu katoka marekani au Ulaya ilikuwa ni kama umemwona mungu.
Sababu ya kupendwa ilikuwa ni zifuatazo
1.Wazungu walionekana kuwa ndio wenye huruma sana.Ndio walikuwa wakinunulia mitumba wanavijiji,Wakilea na kusomesha watoto wa maskini sana na yatima na watoa misaada isiyo na masharti kama miradi ya maji safi vijijini,kuwatibu bure kwenye hospitali nk
2.Tabia za wazungu hao wa zamani zilionekana ndizo bora.Watu waliiga staili za wazungu kuanzia kuchana nywele,kuvaa,kula,kuongea na tabia kwa ujumla kwani ilionekana wazungu ndio wenye tabia nzuri zinazofaa kuigwa na waswahili.
3.Wazungu walionekana ndio watu wa dini na wanaojua dini na kuifuata kuliko mtanzania yeyote kwani ndio walileta dini wakawafunza watanzania,wakawajengea makanisa,nk
Sasa hivi wazungu hao huruma hawana,tabia wako hovyo yaani kuanzia kuvaa,ushoga usagaji nk na dini hawana ni machakaramu fulani hivi kiasi kuwa sasa hivi ukitaja mzungu picha inayokuja kwa mtanzania wa kawaida ni ile ya mtu asiyekuwa na huruma mwenye tabia ya hovyo na asiye na dini.Na kwa sasa hata mswahili akienda ulaya au marekani watasema subiri uone akirudi atakavyokuwa kaharibika.Siku ya kwanza akiondoka kwenda ulaya au marekani utamkuta kavaa suti kapendeza.Siku ya kurudi ukienda airport kumpokea utakuta kavaa kikaptula ,nywele ziko kama za chizi na makobasi au ndala miguuni
Wazungu wakitaka kurudi kuheshimiwa wajitizame kwa nini sasa hivi hawatetemekewi kama zamani