Ulanguzi wa mabati duka la jeshi Lugalo

Rosena

Member
Sep 11, 2012
51
4
Duka la Jeshi Lugalo umezuka mitindo ambao unafanywa na (vishoka) wakishirikiana na wahusika ndani ya duka hilo. Ukienda pale kwa ajili ya kununua mabati unaambiwa yamakwisha, ukitoka nje ya duka unakutana na watu kibao wanao kutangazia kuwa wao wana mabati wanauza kwa bei ya juu tofauti na ile ya ndani ya duka ambapo bati moja ni Tsh 23,000/ tu, wao wanauza kuanzia elfu 24,000/ na kuendelea juu kwa bati moja.

Mabati hayo ya ulanguzi endapo utakubali kuuziwa yanatolewa hapohapo kwenye stoo ya duka, sasa hapo huoni kuwa wahusika ndani ya duka wanaushiriki katika biashara hii haramu?

Tunasikitika sana kwa vitendo hivi ambavyo vinafanywa na baadhi ya wanajeshi mahali hapo. Wamegeuka madalali wa mabati hayo.
 
mkuu inawezekana wewe umeshindwa bei au kuna mtu kakuzidi kete ndo unaanza kulalamika.kwa nini hukuchukua hatua ya kuandika malalamiko yako na kupeleka pale kwa manager wa duka au mkuu wa kikosi maana hapo ndo ungepata jibu la haraka. by the way ni bati gani hizo zinauzwa hizo bei. kwa taarifa yako nenda pale mandela road after tabata relini kuna warusi wanauza bati bundle moja bei ni 216,000. zikakaa bati 16-18 za geji tafauti ukitaka za south pia ni bei cheap
 
Kwani wewe mwanajeshi???? lile duka ni kwa ajili ya wanajeshi tuuuu....
 
Mabati ya majeshi wewe unataka ya nini? nenda madukani usikwepe kulipa kodi. Wao wameondolewa kodi zote, sasa wewe yanakuhusu nini?
 
Duka la Jeshi Lugalo umezuka mitindo ambao unafanywa na (vishoka) wakishirikiana na wahusika ndani ya duka hilo. Ukienda pale kwa ajili ya kununua mabati unaambiwa yamakwisha, ukitoka nje ya duka unakutana na watu kibao wanao kutangazia kuwa wao wana mabati wanauza kwa bei ya juu tofauti na ile ya ndani ya duka ambapo bati moja ni Tsh 23,000/ tu, wao wanauza kuanzia elfu 24,000/ na kuendelea juu kwa bati moja. Mabati hayo ya ulanguzi endapo utakubali kuuziwa yanatolewa hapohapo kwenye stoo ya duka, sasa hapo huoni kuwa wahusika ndani ya duka wanaushiriki katika biashara hii haramu? Tunasikitika sana kwa vitendo hivi ambavyo vinafanywa na baadhi ya wanajeshi mahali hapo. Wamegeuka madalali wa mabati hayo.

ww ni mwanajeshi? kama ndiyo kawambie wakubwa wako mwamnyange, shimbo ni na siyo ulifuata nn huko? nenda Alaf au mwenge kanunue kihalali.
 
mkuu inawezekana wewe umeshindwa bei au kuna mtu kakuzidi kete ndo unaanza kulalamika.kwa nini hukuchukua hatua ya kuandika malalamiko yako na kupeleka pale kwa manager wa duka au mkuu wa kikosi maana hapo ndo ungepata jibu la haraka. by the way ni bati gani hizo zinauzwa hizo bei. kwa taarifa yako nenda pale mandela road after tabata relini kuna warusi wanauza bati bundle moja bei ni 216,000. zikakaa bati 16-18 za geji tafauti ukitaka za south pia ni bei cheap

naomba contact za hawa warusi
duka lao linaitwaje?
 
Watu hupenda kutetea vitendo viovu, maduka ya Jeshi yamesamehewa kodi ili wanajeshi wote tuweze kuhudumiwa kihalali sasa ulanguzi wa nini. Wauzaji hawana sababu ya kucheza mchezo mchafu ndani ya maeneo ya jeshi. Kama wanataka ulanguzi waende wafungue duka nje ya maeneo ya Jeshi wasitumie mwamvuli wa Jeshi kujinufaisha. Mkuu na wewe unafaidika na kamchezo kale nini mbona unatetea sana.
 
Duka la Jeshi Lugalo umezuka mitindo ambao unafanywa na (vishoka) wakishirikiana na wahusika ndani ya duka hilo. Ukienda pale kwa ajili ya kununua mabati unaambiwa yamakwisha, ukitoka nje ya duka unakutana na watu kibao wanao kutangazia kuwa wao wana mabati wanauza kwa bei ya juu tofauti na ile ya ndani ya duka ambapo bati moja ni Tsh 23,000/ tu, wao wanauza kuanzia elfu 24,000/ na kuendelea juu kwa bati moja. Mabati hayo ya ulanguzi endapo utakubali kuuziwa yanatolewa hapohapo kwenye stoo ya duka, sasa hapo huoni kuwa wahusika ndani ya duka wanaushiriki katika biashara hii haramu? Tunasikitika sana kwa vitendo hivi ambavyo vinafanywa na baadhi ya wanajeshi mahali hapo. Wamegeuka madalali wa mabati hayo.

Cc: Super Handsome.
 
Back
Top Bottom