Ulaji WA mafuta usio kawaida.

lameck59

Member
Joined
Mar 7, 2021
Posts
6
Reaction score
9
Habari zenu waungwana, naomben msaada wa kutatua changamoto katika gari, Nina Toyota ractis cc 1490 engine 1nz-FE, ina week tangu niitoe showroom, tatizo nililobaini NI kwamba inakula wese ambavyo sio kiwango chake kinachofahamika. Litre moja inatembea km 11. Je huu ulaji WA mafuta upo Sawa. Maana nlifanya service ya kubadili oil na oil filter tu. Naombeni mnisaidie Kwa mwenye uelewa na hili.
 
Kwa mtazamo wangu factor nyingi zinaweza fanya Gari ile Mafuta sana - uendeshaji wako wa kukimbiza sana Gari na kufunga sana breki, foleni, mizigo, kuwekewa Mafuta kidogo kwa kujaza Mafuta mchana na jua kali, friction, Milima nk

Ingawa 11km/L kwa Gari ya CC 1500 sio mbaya sana. Wenzako CC 2000 ni 7km/L

Alternatively unaweza kudowngrade to IST CC 1300 au Vitz CC 990.
 
Je nkishafisha engine Kwa kutumia motor flash, nkaeka engine ya Castrol ama total na nkabadil pug inawez kusaidia?
 
Sasa Bwana Lameck ulitaka Ractis yako inywe supu badala ya wese??kwa foleni za Dar Lita Moja kwa KM 11 ni sawa kabisa acha kulialia
 
Unajua lkn hio hio IST uliyoitaja inatumia engine iliyoko kwny hio hio ractis(1NZ-FE)?
 
Sisi tunaopiga 4.5 Km/ litre tusemeje 😂
 
Sababu za kula mafuta,anglia vitu vifuatavyo kama vipo sawa - air cleaner,spark plug,air flow sensor hii usibadili huwa inakuwa imejaa vumbi safisha. Oxygen sensor hii ni sensor ipo kwenye exhaust kazi yake ni kusensi air and fuel ratio kama ina shida gari itakula mafuta, la mwisho na kubwa zaidi kwenye exhaust kuna masega kama wametoa itakula mafuta.
 
Je nkishafisha engine Kwa kutumia motor flash, nkaeka engine ya Castrol ama total na nkabadil pug inawez kusaidia?
Hebu subiri kwanza, wewe Ulitaka upate km/L ngapi? Je, umewahi kumiliki gari kabla?
 
Hebu subiri kwanza, wewe Ulitaka upate km/L ngapi? Je, umewahi kumiliki gari kabla?
Hapan mkuu, nlihitj experience Tu nijue Kam gar IPO Sawa au vp. Maana skufanya service kubwa tangu ifike dar.
 
Hapo umedanganya...hiyo inakula 5km/l hadi 6km/l kwa tripu za ndani
 
Hata mikoani tutapata magari yakutembelea nyie wa Dar mnatuchukulia poa sana sijuii kwanini maana kuna mtuu anauliza hivi mikoani kuna vocha za simu
 
Ikikushinda madalali wapo kidongo chekundu, sinza na kinondoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…