FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 40,823
- 46,943
Kwa maelezo niliyokuwa nikiyasikia katika mahojiano mbali mbali ya waziri wa mazingira mwaka huu unaelekea kuwa wa mwisho, kila mchakato lazima ufike mwisho, kilichotokea siwezi kuverify independentlykwanini unasema mchakato unaenda kukamilika, nini kimetokea?
Azimio la kimataifa nchi zote duniani zisitishe matumizi ya mifuko ya plastiki.Ni miaka takriban 10 sasa serikali imekua katika mchakato wa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki yenye athari kubwa katika mazingira na uchafuzi wa mazingira kwa ujumla, imefika mahala jiji lote la Dar linafanana kama dampo la takataka.
Ila kwa sasa kuna uwezekano mkubwa mchakato huo ukawa unaelekea kukamilika, hii ni nafasi na fursa kwa vijana wasio na ajira kuanza kutengeneza vikundi vya usukaji vikapu na uundaji wa mifuko ya karatasi na khaki, pia ubunifu wa aina zingine za vifungashio na vibebeo utahitajika. Kila la kheri.
Wazo zuriUnaenda sokoni, ukinunua nyanya unapewa mfuko, vitunguu unapewa mfuko, hoho unapewa, ...nk, ukifika home una mifuko kumi midogo midogo, kwa nini nchi isiwe chafu.
Tukijijengea utamaduni wa kwenda sokoni na vibebea mizigo, kama mifuko migumu ya nylon, vikapu au mifuko ya karatasi, nchi itakuwa salama.