Hatimaye Waziri Mkuu Majaliwa, apiga marufuku mifuko ya Plastiki

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
40,796
Reaction score
46,910
Video ina maelezo kamili toka kwa Waziri mkuu mwenyewe, waziri mkuu, sio waziri kivuli marope. Hahahah

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia Juni mosi mwaka huu, itakuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote na matumizi yake yatakoma ifikapo Mei 31, 2019.

“Hivi karibuni nimemwagiza Waziri anayesimamia masuala ya mazingira ikiwemo kuzungumza na wadau mbalimbali, ikiwemo wenye viwanda vya kutengeneza mifuko ya plastiki kwa ajili ya kuhakikisha jambo hili linatekelezwa kwa haraka.”

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Aprili 9, 2019) Bungeni jijini Dodoma, kwenye mkutano wa 15 wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2019/2020.

“Kuanzia sasa tunatoa fursa ya viwanda kubadilisha teknolojia, wauzaji kuondoa mzigo uliopo, Ofisi ya Waziri wa Nchi, Makamu wa Rais itajiandaa kutumia kanuni chini ya Sheria ya Mazingira ili kulifanya katazo hili kuwa na nguvu ya kisheria. Tunachukua hatua hii ili kulinda afya ya jamii, wanyama, mazingira na miundombinu dhidi ya athari kubwa zinazotokana na taka za plastiki,” amesema.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua kwamba kuna baadhi ya bidhaa lazima zifungwe kwenye vifungashio vya plastiki na kwamba vifungashio kwa bidhaa hizo havitapigwa marufuku.

“Kwa msingi huo, katika hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, yatatolewa maelezo ya kina kuhusu katazo la vifungashio vya aina hii, hasa katika maeneo ya uzalishaji viwanda, sekta ya afya, na kilimo,” amesema.

Amesema ana imani kuwa utaratibu huo pamoja na kutunza mazingira, utatoa fursa ya kutengeneza ajira nyingi husasan za watu wa chini kupitia utengenezaji wa mifuko mbadala ya plastiki pamoja na kutumia kikamilifu fursa ya viwanda vya karatasi vilivyopo nchini ikiwemo cha Mgololo.

Amesema matumizi ya plastiki nchini yameendelea kuleta madhara makubwa ikiwemo vifo vya mifugo kwa kula plastiki, kuziba kwa mifereji, uchafuzi wa mazingira na kushindikana kwa kuozesha taka kwenye vituo vya kukusanya taka.

Bunge lilikubali kupitisha sh. 148,886,523,581/- kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake kwa mwaka 2019/2020. Kati ya hizo, sh. 86,290,355,000/- ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 62,596,168,581/- ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Vilevile, Bunge liliidhinisha sh. 124,182,537,600 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo kati ya hizo 116,573,026,000/- ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 7,609,511,600/- ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
 
tatizo la Tanzania tunaiga kila kitu, badala kuwekeza kwenye technologia ya ukusanyaji taka ngumu na kuziteketeza, tunapiga marufuku mifuko ya plastic wakati hata hiyo ya karatasi hatuna, inaweza kuwepo isiyotosheleza mahitaji ya walaji lakini tunapiga marufuku, huu ni ujinga.

Hizi sio zama za kuzuia matumizi ya technologia ni zama za kuwekeza kwenye technologia. kama serikali haiwezi inge out source hiyo huduma ya recycling kwa kampuni zi nazoweza.

Kuna wawekezaji mliwaita kutoka china wanatengeneza hiyo mifuko na uwekezaji haujafikia hata mwaka , unapiga marufuku sasa huko si kutafuta kesi zisizo na kichwa wala miguu?

Wakishitaki mnaanza kulia lia ohoo nchi hii ina sharia zake, wakati nyie mnaiga vitu bila kukumbuka mlio waleta kutoka china kuwekeza kwenye hilo eneo la vifungashio na vingi kama sio vyote ni plastiki.
 
tatizo la Tanzania tunaiga kila kitu, badala kuwekeza kwenye technologia ya ukusanyaji taka ngumu na kuziteketeza, tunapiga marufuku mifuko ya plastic wakati hata hiyo ya karatasi hatuna, inaweza kuwepo isiyotosheleza mahitajoi ya walaji lakini tunapiga marufuku, huu ni ujinga. Hizi sio zama za kuzuia matumizi ya technologia ni zama za kuwekeza kwenye technologia. kama serikali haiwezi inge out source hiyo huduma ya recycling kwa kampuni zi nazoweza.
Kuna wawekezaji mliwaita kutoka china wanatengeneza hiyo mifuko na uwekezaji haujafikia hata mwaka , unapiga marufuku sasa huko si kutafuta kesi zisizo na kichwa wala miguu? Wakishitaki mnaanza kulia lia ohoo nchi hii ina sharia zake, wakati nyie mnaiga vitu bila kukumbuka mlio waleta kutoka china kuwekeza kwenye hilo eneo la vifungashio na vingi kama sio vyote ni plastiki.
Hoja dhaifu sana umetoa.
1.) Tanzania haiigi kila kitu, tunaiga mazuri na kukataa mabaya, mfano tulikataa ushoga.

2.)Unajua madhara ya sumu zitokanazo na hiyo kuteketeza taka za plastic?

3.)Aliesema hatuna mifuko ya karatasi / mbadala ni nani?

4.)Hao wawekezaji wamepewa muda wa kuboresha mitambo yao ili kutengeneza vibebeo mbadala, (na vilivyopigwa marufuku ni vibebeo vya plastiki, sio vifungashio vya platiki kama vya kufungasha mikate) mfano vikapu vigumu vya aina mbali mbali, mifuko ya vitambaa, mifuko ya karatasi nk.
 
tatizo la Tanzania tunaiga kila kitu, badala kuwekeza kwenye technologia ya ukusanyaji taka ngumu na kuziteketeza, tunapiga marufuku mifuko ya plastic wakati hata hiyo ya karatasi hatuna, inaweza kuwepo isiyotosheleza mahitajoi ya walaji lakini tunapiga marufuku, huu ni ujinga. Hizi sio zama za kuzuia matumizi ya technologia ni zama za kuwekeza kwenye technologia. kama serikali haiwezi inge out source hiyo huduma ya recycling kwa kampuni zi nazoweza.
Kuna wawekezaji mliwaita kutoka china wanatengeneza hiyo mifuko na uwekezaji haujafikia hata mwaka , unapiga marufuku sasa huko si kutafuta kesi zisizo na kichwa wala miguu? Wakishitaki mnaanza kulia lia ohoo nchi hii ina sharia zake, wakati nyie mnaiga vitu bila kukumbuka mlio waleta kutoka china kuwekeza kwenye hilo eneo la vifungashio na vingi kama sio vyote ni plastiki.
Unapoita maamuzi ya kijinga nakuona wewe ndio mjinga zaidi. Hauelewi madhara ya hii mafuko kwa afya na mazingira.

Afya
Jambo moja tu hapa nakupa. Hii mifuko ndo wamegeuza kifungashio cha chakula cha haraka - fast food. Chips na kuku wa moto, wali au ugali ndio vifungashio. Je unatambua madhara ya huu ujinga unafanywa na wananchi mjini na vijijini? Kingine, watu wanapika viazi, mihogo na wali wanafunike na hayo maplastic. Kansa nje nje hapa.

Mazingira
Hii mifuko imeenea mijini na vijijini. Je kwa uelewa na ujinga wa watanzania wengi ni nani anawaza ku recycle hii kitu zaidi ya kutupa na kufukia ardhini! Kwa ujinga wa watu wengi suala la recycle halipo. Sio suala la kupayuka tu mdomoni ni kitu inahitaji ustaarabu fulani vile.

Naunga mkono hoja ya Waziri mkuu kwani wawekezaji katika mifuko hiyo walipewa notice ya miaka 3 wabadili mfumo wa viwanda, kama waliendelea kuwekeza shauri yao
 
Naunga mkono hoja...
 
Hoja dhaifu sana umetoa.
1.) Tanzania haiigi kila kitu, tunaiga mazuri na kukataa mabaya, mfano tulikataa ushoga.

2.)Unajua madhara ya sumu zitokanazo na hiyo kuteketeza taka za plastic?

3.)Aliesema hatuna mifuko ya karatasi / mbadala ni nani?

4.)Hao wawekezaji wamepewa muda wa kuboresha mitambo yao ili kutengeneza vifungashio mbadala, mfano vikapu vigumu vya aina mbali mbali, mifuko ya vitambaa, mifuko ya karatasi nk.
Kwa mfano mtu akifa atafungiwa na nn

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tatizo la Tanzania tunaiga kila kitu, badala kuwekeza kwenye technologia ya ukusanyaji taka ngumu na kuziteketeza, tunapiga marufuku mifuko ya plastic wakati hata hiyo ya karatasi hatuna, inaweza kuwepo isiyotosheleza mahitajoi ya walaji lakini tunapiga marufuku, huu ni ujinga.

Hizi sio zama za kuzuia matumizi ya technologia ni zama za kuwekeza kwenye technologia. kama serikali haiwezi inge out source hiyo huduma ya recycling kwa kampuni zi nazoweza.

Kuna wawekezaji mliwaita kutoka china wanatengeneza hiyo mifuko na uwekezaji haujafikia hata mwaka , unapiga marufuku sasa huko si kutafuta kesi zisizo na kichwa wala miguu?

Wakishitaki mnaanza kulia lia ohoo nchi hii ina sharia zake, wakati nyie mnaiga vitu bila kukumbuka mlio waleta kutoka china kuwekeza kwenye hilo eneo la vifungashio na vingi kama sio vyote ni plastiki.
Wewe utakuwa unafanya biashara ya mifuko hiyo bila shaka

Nayapongeza sana maamuzi ya Waziri mkuu lau tunechelewa mno Tanzania kutoa maamuzi haya bora kwa mazingira yetu na afya za Watanzania na viumbe vingine pia. Jambo hili limezungumzwa miaka kadhaa bila ya utekelezaji na Waziri mwenye dhamana ya mazingira. Wakati umefika sasa hatuhitaji stories ila tunachosubiri ni utekelezaji wa agizo la Mh. Waziri Mkuu. Mifuko ya Plastiki imeleta adhali nyingi za kimazingira katika nchi yetu ambapo pia imesababisha financial burden kubwa kwa mfano vifo vya wanyama, samaki, maafuliko na damages za aina mbalimbali. Lakini pia kwa faida ya wasomaji wa uzi huu, Mifuko hii inapofungia chakula au kuchomwa huwa chanzo mahususi cha saratani kwa mwanaadamu. Isitoshe pia ni chanzo cha land pollution kwa sababu inapotupwa haiwezi oza ardhini.

Kwa hiyo basi tumefikika mahali hatuhitaji hadithi tena. Wenye viwanda na wafaidika wengine wa mifuko hiyo wakubali matokeo na kujipanga upya. Wenye viwanda wengi hapa nchini wanatoka kwenye nchi zao ambako mifuko hii haikubaliki tena. Enough is enough, lt is time now TO SAY NO TO PLASTIC BAGS IN TANZANIA’’
 
tatizo la Tanzania tunaiga kila kitu, badala kuwekeza kwenye technologia ya ukusanyaji taka ngumu na kuziteketeza, tunapiga marufuku mifuko ya plastic wakati hata hiyo ya karatasi hatuna, inaweza kuwepo isiyotosheleza mahitajoi ya walaji lakini tunapiga marufuku, huu ni ujinga.
Hizi sio zama za kuzuia matumizi ya technologia ni zama za kuwekeza kwenye technologia. kama serikali haiwezi inge out source hiyo huduma ya recycling kwa kampuni zi nazoweza.
Kuna wawekezaji mliwaita kutoka china wanatengeneza hiyo mifuko na uwekezaji haujafikia hata mwaka , unapiga marufuku sasa huko si kutafuta kesi zisizo na kichwa wala miguu?
Wakishitaki mnaanza kulia lia ohoo nchi hii ina sharia zake, wakati nyie mnaiga vitu bila kukumbuka mlio waleta kutoka china kuwekeza kwenye hilo eneo la vifungashio na vingi kama sio vyote ni plastiki.
Unajua madhara ya hizi takataka mkuu?
 
Back
Top Bottom