Ulaji kwa watengeneza vikapu na mifuko ya khaki, mifuko ya plastic bye bye

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
40,792
Reaction score
46,909
Ni miaka takriban 10 sasa serikali imekua katika mchakato wa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki yenye athari kubwa katika mazingira na uchafuzi wa mazingira kwa ujumla, imefika mahala jiji lote la Dar linafanana kama dampo la takataka.
Ila kwa sasa kuna uwezekano mkubwa mchakato huo ukawa unaelekea kukamilika, hii ni nafasi na fursa kwa vijana wasio na ajira kuanza kutengeneza vikundi vya usukaji vikapu na uundaji wa mifuko ya karatasi na khaki, pia ubunifu wa aina zingine za vifungashio na vibebeo utahitajika. Kila la kheri.

===============================
Update: 09/04/2019
Mifuko ya plastiki imepigwa marufuku!

============================
 
kwanini unasema mchakato unaenda kukamilika, nini kimetokea?
 
Kwa maelezo niliyokuwa nikiyasikia katika mahojiano mbali mbali ya waziri wa mazingira mwaka huu unaelekea kuwa wa mwisho, kila mchakato lazima ufike mwisho, kilichotokea siwezi kuverify independently
 
Kwa jinsi heading inavyosomeka nikadhani ulaji uliokuwepo kwa watengenezaji wa vikapu na mifuko ya khaki na pia mifuko ya plastic umefikia kikomo. Kumbe ulaji unaofikia kikomo ni kwa wale wauzaji wa mifuko ya plastic tu.
 
Ni miaka takriban 10 sasa serikali imekua katika mchakato wa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki yenye athari kubwa katika mazingira na uchafuzi wa mazingira kwa ujumla, imefika mahala jiji lote la Dar linafanana kama dampo la takataka.
Ila kwa sasa kuna uwezekano mkubwa mchakato huo ukawa unaelekea kukamilika, hii ni nafasi na fursa kwa vijana wasio na ajira kuanza kutengeneza vikundi vya usukaji vikapu na uundaji wa mifuko ya karatasi na khaki, pia ubunifu wa aina zingine za vifungashio na vibebeo utahitajika. Kila la kheri.
Azimio la kimataifa nchi zote duniani zisitishe matumizi ya mifuko ya plastiki.
 
Unaenda sokoni, ukinunua nyanya unapewa mfuko, vitunguu unapewa mfuko, hoho unapewa, ...nk, ukifika home una mifuko kumi midogo midogo, kwa nini nchi isiwe chafu.

Tukijijengea utamaduni wa kwenda sokoni na vibebea mizigo, kama mifuko migumu ya nylon, vikapu au mifuko ya karatasi, nchi itakuwa salama.
 
Wazo zuri
 
Lakini tusiwe dampo la mifuko mengine badala yake tukaribishe wawekezaji watakaobadilosha mapakacha kuwa mifuko bora zaidi
 
Back
Top Bottom